Vigogo wapigana vikumbo harusi ya binti Lowassa

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
KIKWETE ATIA DOA BAADA YA KUSHINDWA KUTOKEA UKUMBINI, DK SHEIN, MWINYI, KARUME, NAHODHA, DK SALIM, WARIOBA, WATINGA


Ramadhan Semtawa

EDWARD Lowassa, ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu kutokana na kashfa ya mkataba wa kifisadi kati ya kampuni ya Richmond Development (LLC) na Tanesco, juzi alitikisa Jiji la Dar es Salaam baada ya sherehe ya kumuaga bintiye anayeitwa Dk Anna kuvuta vigogo wengi akiwemo makamu wa rais, Dk Ali Mohamed Shein na rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Sherehe hiyo kubwa iliyofanyika Desemba 8 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, ilianza majira ya 12:30 jioni na kumalizika saa 7:30 usiku, lakini Rais Jakaya Kikwete alishindwa kuhudhuria na kutoa udhuru dakika za mwisho.

Wingi wa vigogo hao waliohudhuria sherehe hiyo unaweza kuzidi hata idadi ya vigogo waliohudhuria sherehe za miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kesho yake kwenye Uwanja wa Uhuru.

Wakati mawaziri wa zamani na vigogo wengine hawakuhudhuria sherehe za uhuru, hali ilikuwa tofauti kwenye sherehe ya kumuaga binti Lowassa ambazo zilihudhuriwa na vigogo wengi wa CCM na serikali, ukiacha Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Samuel Sitta na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe.

Vigogo ambao Mwananchi iliwaona wakitinga kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee ni pamoja na Mzee Ruksa, Dk Shein, Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha na Dk Mohamed Ghalib Bilal ambaye aliwahi kuwa waziri kiongozi.

Vigogo wengine walioshuhudiwa na Mwananchi ni pamoja na mawaziri wakuu wastaafu, Dk Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Warioba, ambao hawakuhudhuria sherehe za miaka 48 ya Uhuru Desemba 9.

Dk Salim aliondoka eneo la tukio saa 6:20 usiku baada ya kuondoka viongozi wakuu, akiwemo Dk Shein aliyeondoka saa 5:56 na kufuatiwa na Rais Karume na Nahodha.

Sherehe hizo ambazo ziliwekewa mfumo imara wa ukaguzi, ulinzi na usalama wa hali juu ikiwemo pia mawasiliano ya kisasa, zilihudhuriwa pia na vigogo wengine wa juu serikalini akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi (CS) ,Philemon Luhanjo ambaye aliondoka saa 6:06 usiku.

Vigogo wengine waliohudhuria ni Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu, ambaye aliondoka ukumbini mnamo saa 6:17 na mawaziri Sophia Simba wa Ofisi ya Rais (Utawala Bora) aliyeondoka saa 6: 18 usiku akiwa kwenye gari moja na waziri mwenzake wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia.

Mawaziri wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Dk Batilda Burian kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) aliyeondoka saa 6:18, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Juma Kapuya (saa 6:26), Naibu Waziri wa Ulinzi, Emmanuel Nchimbi (saa 6: 20) na Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohamed Aboud (saa 6:17)

Wengine ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Jeremia Sumari (saa 6:19) na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga (saa 6:15) aliyekuwa anachechemea.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka ukumbini baada ya kutoka kwenye lango kuu majira ya saa 3:40 usiku wakati sherehe ikiwa imeanza kupamba moto na kufuatiwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe.

Katika sherehe hizo ambazo mkuu wa Kanisa la Kilutheri, Askofu Alex Malasusa alikuwa mzungumzaji wa familia, pia walikuwepo vigogo wengine kadhaa akiwemo waziri wa zamani wa fedha na uchumi, Zakhia Meghji aliyeondoka saa 6:31 usiku, Andrew Chenge, aliyekuwa waziri wa Miundombinu ambaye aliondoka saa 6:21 na mke wa rais mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Anna Mkapa aliyeondoka saa 6:05 usiku.

Wengine ni Nazir Karamagi, ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini kabla ya kujiuzulu kutokana na kutajwa katika kashfa ya Richmond, aliondoka saa 6:04, Basil Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi na ambaye aliondoka saa 6:06 usiku na mzee Kingunge Ngombale Mwiru, anayetajwa kuunga mkono kundi la watuhumiwa wa ufisadi, ambaye aliondoka saa 6:06.

Mbunge wa Kawe, Ritha Mlaki na katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni walikuwa miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo na ambao waliondoka ukumbini hapo majira ya saa 6:25 usiku.

Katika sherehe hizo ambazo zilipambwa na makampuni mawili ambayo ni Monica Agency na Creative Option Tz iliyo maeneo ya Makumbusho mkabala na MMK, pia zilihudhuriwa na watendaji wengine mbalimbali wa mashirika, akiwemo Ole Madeje ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Dk Charles Kimei, mkurugenzi mtendaji wa CRDB aliyeondoka ukumbini saa 6:15 usiku.

Wengine waliohudhuria ni katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, mwenyekiti wa CCM mkoani Dar es Salaam, John Guninita na mbunge wa viti maalumu Janeth Masaburi, ambao waliondoka kwa nyakati tofauti kati ya saa 6:15 na 6:18, usiku.

Awali, uchunguzi wa kina wa Mwananchi ulibaini kwamba ukumbi huo wa Diamond ulifungwa mashine 15 za viyoyozi aina ya Hitachi ambazo ziliufanya kuwa na baridi tofauti na siku zote ambazo hutumia mapangaboi na kuwa na joto kidogo.

Lakini, siku hiyo Mwananchi ilibaini kwamba ukumbi huo ulikuwa pia umefungwa mashine za kisasa za usalama kwa ajili ya ukaguzi wa watu waliokuwa wakiingia.

Ukumbi uligawanywa katika sehemu kuu tatu; ya kwanza iliyoonekana mithili ya boma la Wamasai, sehemu ya wageni, ikiwemo meza kuu na eneo la chakula.

Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo, Askofu Malasusa alimtaka binti huyo kuheshimu kile alichokiita heshima kubwa ambayo baba yake alipewa na umati huo akisema inatokana na kuishi na watu vizuri.

Kwa mujibu wa Malasusa, heshima hiyo haikuja bure bali ilitokana na kile alichokiita upendo wa Lowassa, uvumilivu wake na kumwachia Mungu kila jambo.

"Kila ninayemjua leo (Desemba 8) yupo hapa, asiyekuwepo ni kwa sababu ya udhuru, hii ni kutokana heshima kubwa ambayo amepewa baba yako. Ni vema ukathamini heshima hii ili nawe uweze kuilinda huko mbele ya safari; thamini watu hawa waliokuja hapa," alifafanua Malasusa.

Naye Makamba, ambaye alifananishwa na Yohana Mbatazi kutokana na kupewa jukumu la kusafisha njia kwa Askofu Malasusa, alimtaka binti huyo kuwa na subira katika mitihani yote ambayo itampata akiwa katika maisha yake ya baadaye.
Huku akitumia nukuu za vitabu vya dini, Makamba alisema: "Imeandikwa sana katika Koran kwamba Mwenyezi Mungu siku zote yuko na mtu mwenye kusubiri, nawe uwe na subira."
 
SHEREHE YENYEWE IMEKAA KISIASA!,
mliohudhuria mseme huyo dk anna alikuwa anaagwa KWANI ANAKUFA?....au anatoka nje ya nchi?
 
Zote hizo ni pesa za Walipa Kodi wa Taifa hili na pia hii ni dhambi sana katika taifa letu na pia kama tungekuwa tunawekeza katika rasilimali zetu na michangi hii kweli tungekuwa mbali sana, Jaribu kupiga hesabu hapa ni zaidi ya mamilioni ya shilingi
 
Zote hizo ni pesa za Walipa Kodi wa Taifa hili na pia hii ni dhambi sana katika taifa letu na pia kama tungekuwa tunawekeza katika rasilimali zetu na michangi hii kweli tungekuwa mbali sana, Jaribu kupiga hesabu hapa ni zaidi ya mamilioni ya shilingi

kwanini msituambie DHIMA HALISI YA HIYO SHEREHE?!
 
[/QUOTE]Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo, Askofu Malasusa alimtaka binti huyo kuheshimu kile alichokiita heshima kubwa ambayo baba yake alipewa na umati huo akisema inatokana na kuishi na watu vizuri. [QUOTE]
Waarabu wa Pemba hawa
 
Matokeo yake wakalewa, kesho yake hangover haikuwaruhusu kwenda kwenye sherehe za Uhuru!
Nani aliwaambia Uhuru day hakuna Pombe, na nyama za kuku?
 
Hata mimi sijui maana kuna ulazima wa kujua kuwa mambo haya na kuona kisiasa zaidi maana kila mtu ana lake
unajua nimeshangaa nilipokuwa nasomoa gazeti sijui lako sijui umekopi,nao hawakuwa open!

lakini huyu anna mimi namfahamu,last time nimona akiwa anagraduate masterz pale mzumbe!

sasa sijui hiyo sherehe walikuwa wanamuaga kivipi!......fuatilieni
 
unajua nimeshangaa nilipokuwa nasomoa gazeti sijui lako sijui umekopi,nao hawakuwa open!

lakini huyu anna mimi namfahamu,last time nimona akiwa anagraduate masterz pale mzumbe!

sasa sijui hiyo sherehe walikuwa wanamuaga kivipi!......fuatilieni
Haya kaka maana unajua mzee mkubwa alikuwa anapima kama kweli bado ana watu kibao maana LS yeye ana watu kibao japo watu wanajaribu kuona kama ni mtu ambaye watu wake wa karibu wamemkimbia, but yupo makini sana
 
Lowasaa ana mbinu nyingi. Akiwakosa kwenye majukwaa atawalainisha kwenye wine na kahawa. Lazima asafishwe kwa hudi na uvumba. Kama alivyosema Mama Sophia Simba EL ni mwanamme nambari moja kwa ukajanja!
 
Lowasaa ana mbinu nyingi. Akiwakosa kwenye majukwaa atawalainisha kwenye wine na kahawa. Lazima asafishwe kwa hudi na uvumba. Kama alivyosema Mama Sophia Simba EL ni mwanamme nambari moja kwa ukajanja!
Ndio maana sisi tunapa shida sana katika kujua kuwa watu wapo upande gani na pia mimi najaribu kurudi nyuma katika kujua na kutafakari katika kujua pengine utabiri wa Shehe Yahaya utatimia maana alisema kuwa EL atarudi katika uongozi wake
 
Ndio maana sisi tunapa shida sana katika kujua kuwa watu wapo upande gani na pia mimi najaribu kurudi nyuma katika kujua na kutafakari katika kujua pengine utabiri wa Shehe Yahaya utatimia maana alisema kuwa EL atarudi katika uongozi wake

mbado....kurudi tena?.mbado...kusafishwa?....mbado...utabiri?...mbado

ila ninachomkubali lowasa is a friendly man. on personal level sio mbaya kivile kama watu wanavyofikili....ila bwana kimasilahi...
 
Hapo kwenye milo utawaona wengi lakini wengi wao iwa wanakuja kujionyesha si mmeona hapo kwenye sherehe za Uhuru wakala kona lakini kwenye milo mamisosi ndo hao duh .
 
Kwani kuna ubaya gani mtu kushiriki katika sherehe/au kualikwa na rafiki yake? Mimi sioni shida hapa.
Kwani kujiuzulu kwa EL katika uongozi kulimaanisha awe nauadui marafiki zake na viongozi aliowahi kufanya nao kazi?
Napata shida kidogo hapa kama mtu akijiuzulu, basi anatengwa na marafiki zake.
 
Matokeo yake wakalewa, kesho yake hangover haikuwaruhusu kwenda kwenye sherehe za Uhuru!
Nani aliwaambia Uhuru day hakuna Pombe, na nyama za kuku?

Nani alikwambia wao wanajali hayo? Tanzania ni aidi ya uijuavyo!!
 
SHEREHE YENYEWE IMEKAA KISIASA!,
mliohudhuria mseme huyo dk anna alikuwa anaagwa KWANI ANAKUFA?....au anatoka nje ya nchi?
Binamu alikuwa wanamsend OFF kwenda kufanya PHD, si unajua tena mambo ya masomo, elimu haina mwisho.
 
Back
Top Bottom