Vigogo walionunua magari ya wizi kujulikana leo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Date::5/26/2009

Vigogo walionunua magari ya wizi kujulikana leo

Na Sadick Mtulya

Mwananchi
WIZARA ya Mambo ya Ndani leo inatarajia kutangaza majina ya vigogo walionunua magari ya wizi kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Japani.

Habari zinadai kwamba zaidi ya magari 350,000 yalishaibwa nchini Japan yakiwa mapya na kwamba baadhi ya magari hayo yamuzwa zaidi ya mara moja kwa watu tofauti.

Taarifa zilizopatikana jana zilidai kazi ya kuwataja wahusika hao ilikuwa ifanyike jana, lakini ilishindika kutokana na baadhi ya nyaraka muhimu kuhusu watu hao kutofika Wizarani

Hivi karibuni polisi wa Kimataifa (Interpol) kwa kushirikiana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na ubalozi wa Japan nchini waliendesha msako wa kukamata magari hayo ya kifahari.

Hali hiyo ilielezwa kuwaweka matumbo joto watu wanaomiliki magari kutokana na kutojua kitakachofuata .

Kuendeshwa kwa msako huo kunafuatia taarifa za kuwepo wimbi kubwa la wizi wa magari ambayo yanadaiwa kuwa yanauzwa katika nchi za Kiarabu na Afrika, ikiwemo Tanzania.

Habari zaidi zinasema kuwa magari hayo ya kifahari yakiwemo Toyota Land Cruiser, Prado, VX, GX, Lexus pamoja na Toyota Rav4 yamekuwa yakiibwa katika harakati za kupelekwa sokoni mara baada ya kuundwa na mengine yakiwa katika maeneo ya kuuzia magari.

Habari zinadai kuwa zaidi ya magari 350,000 yameshaibwa nchini Japan hadi sasa, yakiwemo magari ambayo wamiliki wake waliyauza na baadaye kusingizia yameibwa ili walipwe bima.
 
(1)Alex Masawe
(2)David Mosha
(3)Kizaizai super Tall

wadau watajeni wengine kwa tunawajua tunaishinao
 
1)Alex Masawe
(2)David Mosha
(3)Kizaizai super Tall
(4) johnson lukaza
5)benson lukaza
6)RIDHIWANI KIKWETE.J
7)MMILIKI WA RIKI HILL HOTEL PALE KARIAKOO HUYU AMELETEWA MAJUZI TU RANGECRUISER 2...ZILIKAA SANA NDANI BILA KUTEMBEA...
 
1)Alex Masawe
(2)David Mosha
(3)Kizaizai super Tall
(4) johnson lukaza
5)benson lukaza
6)RIDHIWANI KIKWETE.J
7)MMILIKI WA RIKI HILL HOTEL PALE KARIAKOO HUYU AMELETEWA MAJUZI TU RANGECRUISER 2...ZILIKAA SANA NDANI BILA KUTEMBEA...

Mkuu Pdidy haya "nyekundu" ni magari gani tena au ulimaanisha Landcruiser?
 
Sijui na langu la wizi? maana mhh hatuaminiki siku hizi na jamaa wanavyopenda ujiko lazima tutolewe runingani.
 
Mkuu Pdidy haya "nyekundu" ni magari gani tena au ulimaanisha Landcruiser?

HAPANA MKUU NI RANGEROVER
 
Mkuu BAK hii issues watu waliijua (siri zilivuja kwa baadhi ya vigogo hasa wale wanaoshirikiana na po..... ) wakaficha magari ndani??? Kuna ma Rangerover kibao yamefungiwa. Wenye zao wanasubiri hali ya hewa iwe conducive wayatoe nje!!!!

Ila sasa wenye hao magari ni wenye mihela yao!!!! Sasa hapo kuna kesi kweli??? Ushahidi wa kumfunga third party ni mgumu kidogo!!!!!
 
Back
Top Bottom