Vigogo waliokopa CIS wajisalimisha

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Vigogo waliokopa CIS wajisalimisha

na Mobini Sarya
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SIKU chache baada ya wenye makampuni yaliyokopa kwenye mfuko wa Commodity Import Support (CIS), kupewa siku saba wajitokeze kueleza namna watakavyolipa madeni yao kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria, wamiliki wa makampuni zaidi ya 150, yakiwemo yanayomilikiwa na vigogo, wamejisalimisha kwa wakala aliyepewa kazi ya kukusanya madeni hayo.

Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msolopa Investment Ltd, Ibrahim Msolopa, iliyopewa jukumu la kukusanya madeni hayo, alisema jana kuwa tangu atoe tangazo la notisi ya siku saba kwenye vyombo vya habari kuwataka wenye madeni hayo kujisalimisha, wengi wamejitokeza.

Alisema amekuwa akipokea simu kwa watu mbalimbali wakiuliza namna ya kulipa madeni yao, wengine wakifika katika ofisi yake iliyopo Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam ili kujua kiasi cha pesa wanachodaiwa na kueleza namna watakavyozilipa.

“Miongoni mwa watu walioonyesha ushirikiano katika suala hilo ni vigogo, wenye nyadhifa serikalini ambao wamesema wapo tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanalipa madeni yao,” alisema Msolopa.

Kwa mujibu wa Msolopa, tayari kuna watu walioanza kurejesha pesa hizo zilizochukuliwa na makampuni zaidi ya 980 kuanzia mwaka 1988 kwa ajili ya kununulia bidhaa nje, lakini baadaye walishindwa kurejesha fedha hizo.

Kwa mjibu wa mkurugenzi huyo, amekabidhiwa jukumu la kukusanya deni la sh bilioni 191 kutoka kwenye makampuni hayo ambayo yanamilikiwa na watu binafsi pamoja na serikali.

Hata hivyo alisema kazi hiyo inaweza kuwa ngumu kwani baadhi ya makampuni yalishakufa na mengine kubadili wakurugenzi, hivyo wanahitaji vielelezo na mikataba ndipo walipe, huku wengine wakishindwa kueleza mahala ofisi zao zilipo.

Ametoa muda wa miezi sita kwa wakopaji wote wa fedha hizo wawe wamejitokeza kulipa madeni yao, vinginevyo hatua itakayofuata ni kutangazwa kwa majina yao kamili kwenye vyombo vya habari, kisha kufikishwa mahakamani ili kupata kibali cha kuwafilisi.

Wakati wakala huyo akitoa muda huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willbrod Slaa alikaririwa hivi karibuni akisema kuwa kitendo cha serikali kuteua kampuni ya kukusanya madeni ni cha kisanii kwani huo ni utaratibu wa kawaida wa kukusanya madeni na kwamba uchunguzi wa kina unatakiwa ufanyike kubaini ufisadi wa kupindukia katika mfuko huo.

Dk. Slaa ambaye ndiye alikuwa akilia na serikali juu ya ufisadi huo kupitia mfuko wa CIS, alisema hatua ambazo serikali imezichukua haziwezi kubaini ufisadi huo kwani zaidi ya sh bilioni sh 800 zimefujwa na makampuni hewa.

Dk. Slaa alidai kuna vigogo wengi wanaodaiwa kuhusika na ufisadi huo kwani waliuza hati zao kwa matajiri, jambo lililowawezesha baadhi yao kufungua makampuni hewa.
 
Msolopa investment ni nani? na je kampuni hii ina historia gani kiutendaji? na je, commission yake atalipwa vipi katika ukusanywaji wa deni hilo la Ths 191bil?

Usije ukawa ni usanii, anakusanya 191bil analipwa 200bil (bilioni mia mbili)! Mkataba wa Msolopa lazima uwekwe wazi, na pia ufanisi wa kampuni hii lazima tuuelewe vizuri, vinginevyo yatakuwa yale yale ya EPA!
 
Hizo hela hazirudishwi mana kuanzia 1988 mpka leo walikua wapi yaleyale kma tume y maadili
 
utakujaskia wadaiwa sugu mafaili yao yaliishia kwa dpp ....
...na kutupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi na walalamikaji.
 
Back
Top Bottom