Vigogo wahusishwa na kufyatua Noti bandia

Kuna haja ya watu kwenda makanisani na misikitini ili tuombee nchi hii, manake inaonekana kama haina mwenyewe na wale tunaowategemea wamekuwa sehemu ya uozo Mungu ibariki Tanzania
 
Usalama wa Taifa my ass.. What are they doing? Inflation imefika 12%...This govt has really EFFD up.

They are now playing new role. Make sure CCM wins elections. Mambo ya msingi katika usalama wa raia na maendeleo yao kwao hawa si priority, priority ni kulinda viongozi wabinafsi ili waendelee kuwa madarakani kwa vyovyote. They need to change now na kufanya kazi wanayotakiwa kuifanya kwa mujibu wa uwepo wao.
 
Tumekwisha? No! Tulishakwisha.

Hata niitwe mbaguzi lazima nisema kwamba ktk nchi yoyote ukiwaona wahindi wanastawi kwa wingi kama hapa kwetu, basi fahamu inakwisha. Maana yake inaongozwa na corruption.

Unapowaingiza kushika uchumi wa nchi, unawaingiza ktk siasa (maamuzi ya nchi), nini unategemea ktk nchi? Bahati mbaya hawana social interactions na sisi ili tufahamu upuuzi wao. Wachache wanaowasiliana nao, ni kwa ajili ya pesa chafu kama hizo tu basi! Hata sitting room zao hawajawahi kufika.

U-Mafia huo huo hufanywa pia na Korea ya Kaskazini ili kupambana na vikwazo vya US na wanafanikiwa sana!! Tofauti, Korea ni Government deal. Eti hapa kwetu ni deal ya chama tawala na akina fulani! Banana republic.
 
Vigogo wahusishwa kufyatua noti bandia
• Wamo wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa

na Mwandishi Wetu Source.Mtanzania Daima


amka2.gif

BAADHI ya wafanyabiashara maarufu hapa nchini na makada wa chama kimoja kikubwa cha siasa wanahusishwa katika kashfa ya kutengeneza noti bandia ambazo zimepenyezwa katika mzunguko wa fedha hapa nchini kwa muda mrefu sasa.
Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili, imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zinabainisha kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakijihusisha kufadhili na kudhamini shughuli mbalimbali kwenye jamii kiasi cha kujizolea umaarufu.
Fedha hizo zinachapishwa na makampuni ambayo yanamilikiwa na baadhi ya wafanyabiashara matajiri (tycoons), ambao faida yake wamekuwa wakiitumia kwa wanasiasa, viongozi wa dini na watendaji wa serikali kila wapatapo nafasi ya kujumuika na makundi hayo.
Chanzo hicho kilidokeza kuwa noti zinazotengenezwa na wafanyabiashara hao ni zile za sh 5,000 na sh 10,000, ambazo zimekuwa na viwango vya hali ya juu, kiasi cha kumfanya mtumiaji asiweze kubaini kuwa ni bandia.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, mzunguko wa fedha hizo ni mkubwa kiasi cha taasisi zinazojishughulisha na fedha kujikuta zikishindwa kuzizuia, kwa hofu ya kuingia hasara kubwa.
Noti hizo ambazo baadhi yake Tanzania Daima Jumapili imeziona, zinashabihiana kwa kiasi kikubwa na hata baadhi ya wafanyakazi wa benki wamejikuta wakizitumia.
Vituo vya mafuta na mabasi ya abiria ni miongoni mwa sehemu ambazo gazeti hili limebaini kuwa fedha hizo chafu zinatumika kwa kiwango kikubwa, ambapo huchanganywa na nyingine ambazo ni halali.
Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa baadhi ya vigogo wanaotengeneza fedha hizo wamekuwa wakizitawanya sehemu mbalimbali hapa nchini, huku wakiwapa ‘kamisheni’ mawakala wao wanaozisambaza fedha hizo.
Ili kuzuia matumizi ya fedha hizo kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeamua kuchapisha noti za sh 500, 1,000, 5,000 na 10,000 ikizitumia kampuni za kimataifa za utengenezaji wa fedha hizo.
Oktoba mwaka jana, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, akiwa katika Ofisi Ndogo ya Bunge, jijini Dar es Salaam aliwaambia wanahabari kuwa tayari serikali imeshatoa zabuni ya kuchapisha noti hizo.
Katika mchakato wa kuchuja na kupata kampuni itakayokidhi haja hiyo, Cren Currency ya nchini Sweden ilishinda na kupatiwa zabuni ya kuchapa noti za sh 500, 2,000, 5,000 na 10,000, wakati noti za sh 1,000 pekee zitachapwa na Kampuni ya De-rarue ya nchini Uingereza.
Hadi sasa BoT haijawa tayari kutoa taarifa kuwa ni kiasi gani kitatumika mpaka zoezi hilo litakapofikia kikomo.
Tanzania Daima Jumapili iliwasiliana na kitengo cha mawasiliano cha BoT, juu ya mbinu zinazotumika kudhibiti fedha bandia, ambapo kitengo hicho kimesema utengenezaji wa noti mpya utazingatia alama za usalama (Security features) zitakazoendana na teknolojia ya kisasa.
Ofisa wa kitengo hicho, John Kimaro, alisema wamezingatia zaidi teknolojia ya kisasa ili kuwepo na tofauti kubwa kati ya noti halali na bandia, kwa lengo la kumuwezesha mtu kuzitambua kwa urahisi zaidi.
“Tumezingatia maendeleo ya teknolojia zinazotumiwa na watu wanaotoa noti bandia, sisi tutakuwa juu zaidi na tuna uhakika noti zitakazokuja zitakuwa za viwango vya hali ya juu kiasi cha watu kushindwa kuzitengeneza zinazofanana nazo,” alisema ofisa huyo.
Pamoja na baadhi ya watu wanaomiliki mitambo kukamatwa na Jeshi la Polisi, BoT imesema kuwa haina taarifa ya kuwapo baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki teknolojia hiyo ya kuchapa noti bandia na kutaka taarifa zitolewe haraka kwenye vyombo vya habari.
BoT imeongeza kuwa ipo tayari kushirikiana na vyombo vya dola na wananchi kuwashughulikia wale wote wanaozitengeneza noti bandia kwa kuwa wanahujumu uchumi wa taifa.
Tatizo la uwepo wa noti bandia hivi sasa linaonekana kuwa kubwa zaidi, ambapo Septemba mwaka jana, mkoani Dar es Salaam msikiti mmoja uliopo Mburahati ulipewa msaada wa kiasi cha sh milioni mbili na mfanyabiashara mmoja (jina tunalihifadhi), ambazo baadaye zilibainika kuwa ni bandia.
Katika sakata hilo, mfanyabiashara huyo alidai kuwa fedha hizo alizichukua dukani kwake kwa lengo la kutoa msaada katika msikiti wakati wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Uwepo wa noti hizo mara kwa mara umekuwa ukiwafanya baadhi ya wafanyabiashara hasa ndogo ndogo kupata hasa mara wabainipo kuwa hawana fedha halali.
“Kwenye maduka huwa naona sh 5,000 na 10,000 zikiwa zimebandikwa na hazitumiki, nikiuliza naambiwa ni feki, wafanyabiashara ndogo wengi hawazijui na inawakata mitaji wajasiriamali ambao mitaji yao ni midogo,” alisema Mwanaidi Hamis, mkazi wa Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo, nguvu za Jeshi la Polisi zimekuwa zikigonga mwamba kwani pamoja na misako inayoendelea ya mara kwa mara ikihusisha mbinu shirikishi, bado tatizo hilo linaendelea.
Aprili mwaka jana, mkoani Ruvuma, Abel Mgaya (26), mkazi wa Iringa alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia zenye thamani ya sh 520,000.
Mei, mwaka jana, jeshi hilo lilimshikilia Marko Sayi (26), mkazi wa Nyahanga, wilayani Kahama kwa kukutwa na vifaa mbalimbali vya kutengenezea noti bandia.
Shaibu Ibrahim alitaja vifaa hivyo kuwa ni karatasi zilizokatwa ili kutengenezea fedha bandia, wino na pamba. Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amewapa watu mbalimbali kiasi cha sh milioni 2.5, ambazo ni bandia ili wazitumie kununulia mazao na mifugo kutoka kwa wananchi. Hayo yamekuwa ni baadhi ya matukio yanayotoa picha halisi ya namna ambavyo biashara hii inavyoshamiri siku hata siku, licha ya jeshi hilo kujitapa kuwa linadhibiti hali hiyo na BoT ikitoa matamshi ya kukabiliana na matukio ya namna hiyo.


My Take: If this is true,then we are doomed! Hii ni grave damage ktk uchumi wetu.Nowonder pia sarafu yetu inazidi kudidimia,yaaani jamani uzalendo umekosekana namna hii?hizi ni mbinu chafu ambazo kimsingi zinatumiwa na maadui wa nchi nje ya mipaka,but sasa watanzania tena vigogo wamehusika?mbinu hizi zinatumiwa na mataifa hasimu kwani wanajua ni madhara kiasi gani yanasababishwa na mbinu hizo kiuchumi.Mfano Pakistan wanatuhumiwa kuifanyia umafia huu India,Bangladesh na Thailand

Pia,kila zinapotoka noti mpya BOT wamekuwa wakitoa matumaini kwamba itakua ngumu kwa watu kughushi

Kwa kumalizia,Waandishi wa habari nao sijui ni kwa nini hawatoi taarifa kwa vyombo vya usalama maanke inaonekana wanakuwa na dataz.Hili si jambo la mzaha,mwananchi wa kawaida ndiye anaumia zaidi jamani!



Hiyo Bold juu inaeleza mengi ambayo tunajidai kufumbia macho. Hebu tuguess ni nani hao? Bila shaka mafisadi sio wahusika kutokana na maelezo hayo. Labda ni wale wa upande wa pili (yaani wapiganaji)
 
kweli mwalimu na hivi walipoingiza hizi trilioni moja nyingine katika stimulus package yao tuliwahoji hapa.. sasa tunavuna tunashangaa mabua?

Mkuu,

Stimulus package ingesabbabisha inflation ingekua ni kama kazi na dawa.Kwani stimulus package lengo lake ni kushtua uchumi,hiyo ni mbinu nzuri ya kutanua soko,ajira na kuwapa uwezo wa kununua(purchasing power) raia ili viwanda viendelee kuzalisha.

Government expenditure ya aina hii ni nzuri kama iko well planned.Labda kuhoji vipaumbele kwa mapana zaidi maanake ilionekana kama kulikuwa na kufuata mkumbo kwa aina flani.Na inabidi hata sasa hivi tuhoji matumizi na manufaa yake,usishangae hata kwenye bajeti ya mwaka huu wakafanya yale yaliyozoeleka ya kufunika kombe kimazingaombwe
 
-Siku hizi hadi Us Dollars,EURO zinatengenezwa na kusambazwa.Zikiingizwa bongo watu wengi watalizwa ukizingatia kwamba hazijazoeleka sana

-Yale maduka ya kubadilishia hela ambayo hayako active kiteknolojia watatumika kama agents wa huu umafia

-Usijekuta hata hao vigogo wanashirikiana na maofisa usalama wa taifa letu na hata maofisa usalama wa nchi jirani ambao wako sponserd na gvnmt zao.i'm just wondering!
 
-Siku hizi hadi Us Dollars,EURO zinatengenezwa na kusambazwa.Zikiingizwa bongo watu wengi watalizwa ukizingatia kwamba hazijazoeleka sana

-Yale maduka ya kubadilishia hela ambayo hayako active kiteknolojia watatumika kama agents wa huu umafia

-Usijekuta hata hao vigogo wanashirikiana na maofisa usalama wa taifa letu na hata maofisa usalama wa nchi jirani ambao wako sponserd na gvnmt zao.i'm just wondering!


Hakuna Afisa usalama mkuu au mkubwa kuliko amiri jeshi mkuu, yaani Rais wa nchi. Hebu angalia, tunaye afisa usalama wa nchi hapa kwetu?
 
Siku hizi idara ya inteligency ni hovyo sana vitu hivi vyote vinatakiwa vinaziwa mapema visije vika tikisa Taifa mbaya zaidi nchi ndio imeshikwa na mafisadi na hii ni uzembee wa viongozi wetu wa kuingiza uongozi na Biashara, Jamani tunaelekea wapi sasa.Mungu bariki Tanzania
 
Hao vigogo ni akina nani? Kune mtu mwenye majina tafadhali? Amwage jamvini

mimi namtaja rostam azizi ... it has to be him. Kuanzia biashara ya utumwa hadi ya wizi wa mabilioni ya watanzania kupitia dowans. The guy is everywhere.
 
kuongezea kitafunwa hapo juu ^^^^^^ .. hadi kwenye uchaguzi wa kyela koh koh koh koh .. the guy is everywhere.
 
Usalama wa taifa ni kila nani jadilini hoja sio kusingizia wewe mwananchi chukuwa nafasi yako kutetea na kuendeleza nchi yako sio usalama wa taifa
 
-Siku hizi hadi Us Dollars,EURO zinatengenezwa na kusambazwa.Zikiingizwa bongo watu wengi watalizwa ukizingatia kwamba hazijazoeleka sana

-Yale maduka ya kubadilishia hela ambayo hayako active kiteknolojia watatumika kama agents wa huu umafia

-Usijekuta hata hao vigogo wanashirikiana na maofisa usalama wa taifa letu na hata maofisa usalama wa nchi jirani ambao wako sponserd na gvnmt zao.i'm just wondering!

Naomba kuelimishwa kidogo.
Zikishaingizwa hizo dola feki ktk maajenti na hao maajenti watazipeleka wapi baadae? tuseme bank ok na benki wakizipokea baadae watazipeleka wapi?
 
Back
Top Bottom