Sishangai kabisa kuona hayo majina. Bei ya hivyo viwanja ilikuwa ni Tshs 12,000,000/=, mwananchi gani wa kawaida angemudu hiyo bei?
Vigogo wagawiwa viwanja Dar
Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.
Nimelia sana nilipo ona jina la Khalfani Kikwete kwasababu Viwanja vilivyotolewa mara ya Kwanza niliomba naye huyu mtoto lakini yeye alibahatika akapata kiwanja kikubwa, lakini mimi nilikosa japo kuwa mimi ni mtu mzima kuliko yeye na nina uwezo wa kulipia pia sikuumia sana kwasababu ana haki pia. Safari hii nimeomba tena amebahatika yeye tena, hivi jamani huu ni ubinaadam kweli kitoto kidogo kurundikiwa viwanja ili vimfae akikuwa halafu mimi mtu mzima nikose pa kujenga sitaki Kumzungumzia Miraji kwasababu na yeye hiki ni cha kwanza nitaumia iwapo awamu ya pili watampa Miraji tena kiwanja cha pili ilihali mimi nataka kimoja tu sipati. Nina hasira sana sina cha kuifanya hii Serikali
Kama wamefuata masharti na ni watanzania, sioni tatizo.
waacheni wanajiandalia mji wao........
Thats why i hate ccm na system yao......
Bado kuna kigogo kachukua viwanja 30 na jina lake wameliminya.......
sishangai kabisa kuona hayo majina. Bei ya hivyo viwanja ilikuwa ni tshs 12,000,000/=, mwananchi gani wa kawaida angemudu hiyo bei?
Orodha hiyo ni ya zamani tulishajadili mpya bado hawajaweka kwenye mtandaohii hapa
ndug freema agyeman: Huu ni uongo ulio wazi mkuu. Mita moja ya mrabaa kwa viwanja vya makazi ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 6000 na kiwanja kidogo kabisa walau kilikuwa na size ya mita 400 za mraba ambazo ni sawa na shilingi 2,400,000/= . Sasa wewe ni nani amekudanganya mabo haya. Kama huna uhakika au hujui ni vyeam ukawasikiliza wenye kuelewa masuala hayo la sivyo waweza ingia katika matatizo ya uchochezi. Cha msingi cha kusema ni kwamba pamoja na hayo bado bei ni kubwa
Khaaaaaa mkuu vyote hivyo anavifanyia nini? Hii nchi balaa!