Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Ndio bei yake ilikuwa hivyo? Kweli akina siye tusingeweza.....

Ndio bei za viwanja vya serikali hiyo siku hizi mkuu.. yaani kiwanja kidogo kabisa ni around 4m! sasa hapo mfanyakazi wa kawaida atamudu vipi kununua kama sio kutaka watu waibe tu?
 
Mkuu tusiongopeane,hao walioandikwa kwenye gazeti ni wachache lakini ukisoma list kama alivyoiweka Edson,
asilimia kubwa ya majina ni ya viongozi au watoto wa viongozi,madiwani karibu wa manispaa zote za Dar,kwa
watu wa chini ni wachache,kwa taarifa yako hata wafanyakazi wa manispaa ya Temeke wenyewe ambao hawakuwa
na kigogo wa kuwapigia debe wamenyimwa,na majina yaliyotoka this time mengi yamejirudia waliouziwa awamu iliyopita.

Wafanyakazi wa manispaa wanalalamika kwa sababu walizoea kuzoa viwanja wao safari hii kuna taarifa kwamba wamebanwa na ndio wanaoipaka matope manisapaa, wapo waliokuwa wanachota hadi viwanja 10.

Nimeambiwa safari hii manisapaa ilikataa kuwapa viwanja wafanyakazi wake ambao walipata kwenye miradi iliyopita na kuvipeleka kwa wananchi.
 
Viwanja zaidi ya 1800. Shida ni kwamba utayaona majina hayahaya au ya ndugu zao kila kutakapopimwa viwanja. Hili litatufikisha pabaya. Halafu eti wanasema tuache kuwatukana kwenye mitandao! Watufunge tu.

weka majina hapa na sisi tuone maneno matupu hayavunji mfupa.
 
Mara nyingi walalahoi wanaopata hivyo viwanja ni wale wenyeji - ambao huwa lazima wapewe. Hivyo, katika viwanja 1,000 vilivyotangazwa, kuna idadi si haba ambayo inatengwa kwa ajili ya wenyeji ambao wanapewa kipaumbele. Hao wenyeji, kwa kuwa hawana uwezo wa kulipia, huwa wanafanya re-sale kwa bei juu kidogo zaidi ya ile ya manispaa ili nao wapate chochote. Kama una pesa kuanzia milioni 8 utapata kiwanja kutoka kwa hao wenyeji. So ukiondoa wale wenyeji, idadi kubwa ya wanaopata viwanja ni aidha vigogo, au wana connection na vigogo au wametoa mzigo mkubwa manispaa. Ndo TZ yetu hiyo!!

ambatisha na kaushaidi kadogo basi
 
Sishangai kabisa kuona hayo majina. Bei ya hivyo viwanja ilikuwa ni Tshs 12,000,000/=, mwananchi gani wa kawaida angemudu hiyo bei?
Lakini si unalipa kidogo kidogo? na hata hao huwa wanachukua then wanaviuza hata mara 4 ya bei waliyonunulia
 
Tatizo ni kwamba wana viwanja vingine tayari.Kwa nini wasituachie sisi ambao hatuna?Unakubali kuwa Mkama au Ludovick hawana kiwanja/viwanja vingine???


Viwanja vilikuwa vingapi? Hapo huu waliotajwa ni 39 tu. Ina maana viwanja vilikuwa hivyo tu au gazeti limeamua kuorodhesha vigogo tu? Nao si watanzania na hivyo wanastahili kupata viwanja hivyo? Tafadhali tupate na walalahoi waliopata ili kuona uwiano uliopo ndipo tuweze kutoa maoni yetu.
 
Labda ulikuwa hujajua maana halisi ya CCM na Viongozi wake,Chukua Chako Mapema na ndicho kinachofanyika na hii imefanya kila mradi uwe na harufu ya Ufisadi kwa maana nyingine Hakuna mradi unaoweza ukafanywe na serikali hii ya ccm bila watu kujinufaisha na ukikuta kelele basi hao hawakupata mgawo wao, na ukikuta watu wanakwamisha kuanza kwa mradi ujue wanaulizana mi nitapata nini kama hapati atazusha zengwe mradi usitekelezeke, CCM wamebaki na kazi moja 2 nayo ni kuiba kwa kadri wanavyoweza 2
 
Wananchi Tumeanza tambua haki zetu, lakini bado hatujaanza kupambana,
Mjenzi mkuu wa Kigamboni, ni Serikali ya Marekani,

Atajenga Kituo kukubwa, cha Kijeshi chenye, Bandari kubwa, Uwaja mkubwa wa ndege,
Hospitali kubwa, na nyumba za kuishi askari zaidi ya 200,000.

Trilion 16?!! Serikali ya CCM itazinya wapi?? Ili safari ya Mzee Kichaka rais wa Marekani, na zawadi ya vyandarua sijui vya $ M5,
faida yake ni kumegewa kipande cha ardhi, mtakoma na bakuli lenu la umataonya.

Lakini kuna mshiko mkubwa wa karibu $1000,000,000.00 kila mwaka, zitalipwa kama ada ya kunajisi ardhi yetu,
Kuna watu account zao USWIZI zitafura kishenzi.

Mmepigwa sementi ya macho safari hii si changa tena.
 
Hii ni list ya awamu ya kwanza. Awamu ya pili leteni hapa maana naona wesite ya manispaa hawajaweka. Hivi hizi webisite ni za nini kama hazitumiwi ipasavyo.

Why wasting time kwenda kusongamana kusoma vikaratasi vya ukutani while some people can access internet facilities.

Boresheni huduma acheni kukalia rushwa kitengo cha ardhi na tathmini manispaa ya Temeke.
 
Nilicho amini sasa ni kuwa sisi walalahoi tuendelee na viwanja vyetu vya kienyeji...vile vya kuhesabiana miguu na waheshimiwa waendee na viwanja vyao rasmi.

Hii itaendelea kutunyima fursa ya kupata dhamana ya mikopo mikubwa katika asasi za kifedha kwani hatuna hati za kutumika kama dhamana.Anko BEN alijaribu kuja na MKURABITA ambao nao naona ilikuwa nyimbo ngeni isiyoimbika wala kuchezeka huku kwetu maana hakuna kitu ukipate bila kitu (takrima).

Ila nawaza vile watanzania tunavyojitahidi kujenga vibanda vyetu kwa pesa za kuunga-unga katika maeneo yasiyo na miundo mbinu ya maji wala umeme na pindi wakipatamani wanakuja na miradi yao ya miji ya kisasa na fidia uchwara inazidi kuongeza wigo baina yetu na wao.

Hii ndio Tanzania ijengwao na wenye moyo na kuliwa na wachoyo
 
ihs Mkuu mimi vya safari hii sikuviomba nilijua nia yao ni kuchukua tuu pesa za wananchi, huwezi amini vile vya kwanza kuna mtu alinishauri nijaze form nyingi kwa majina tofauti tofauti yakiwemo ya ndugu zangu huenda nitabahatisha kimoja, nilijaza form nane(8) nilifanya hivyo na ghalama za form zilikuwa ni elfu20 kila form nikalipia Jumla Tshs160,000,

Cha ajabu siku walipotoa orodha sikupata hata kimoja nikajaribu kuangalia kama kuna mlalahoi mwenzangu tulie omba naye kama amepata sikuweza kumuona, sana sana niliwaona watu kadhaa waliopata viwanja tena low density kama vile Hawa Ghasia, Mark Mwandosya, Khalfani Kikwete na wengine ambao majina yao sio maalufu nikaambiwa ni mabalozi ni mabalozi au makatibu wakuu au wanausalama. Nikaapa sitakuja kuomba serikali iniuzie kiwanja.
 
Hii ni list ya awamu ya kwanza. Awamu ya pili leteni hapa maana naona wesite ya manispaa hawajaweka. Hivi hizi webisite ni za nini kama hazitumiwi ipasavyo. Why wasting time kwenda kusongamana kusoma vikaratasi vya ukutani while some people can access internet facilities. Boresheni huduma acheni kukalia rushwa kitengo cha ardhi na tathmini manispaa ya Temeke.
Hawawezi kuweka kwasasa wanasubiri kwanza watanzania watulie kidogo kama ilivyozoeleka
 
Tunaongozwa na wezi na sisi pia tuwe wezi ili ngoma iwe droo?
 
Ni vigogo,vimada,wafanyakazi wa halamashauri na ndugu zao kudada da deki...
 
Back
Top Bottom