Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Wana haki lakini pale inapotokea miradi ya viwanja inapotokea yanakuwepo majina yaleyale lazima tuwe na mashaka.

wengi walipata nafasi, ila ilipofika kwenye malipo ndio hapo ikawa hakuna jinsi ila kwa mwenye nazo.

Viwanja vilikuwa low density hadi Tshs milioni kumi na mbili na high density vilikuwa around Tshs millioni 6.
 
Hili gazeti limepotoshwa umma; Vigogo waliopata viwanja ni 39 ama 2.16% ya watu 1,800 waliopata viwanja. Wasio vigogo ni wengi kuliko vigogo. Watz msiwe na kasumba ya kubwabwaja pasipo kuingia ndani kwa hoja
 
Ni wizi wa hali ya juuu, nadhani kwa isu ya temeke lazima tuwape wabunge wa upinzani hii hoja... kwa mpano wamekusanya fedha za form 12,000 ambapo kila moja waliuza 30,000/= hapo wanapata zaidi ya 360,000,000/=. wamegawa viwanja 1,040 tu na tu fanye assuption ya kuwa vyote vimeuzwa kwa bei ya chini kabisa ambay ilikiwa Tsh 4,800,000 wanepata 4,992,000,000 sasa hii nidhuruma kabisa

Kaka Mwananchi wameandika form zilizo uzwa ni 20,000
 
MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.
Majina hayo ambayo gazeti hili iliyaona jana, yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo wa manispaa hiyo, ili wananchi walioomba viwanja hivyo waweze kuangalia kama wamo katika orodha ya waliopatiwa viwanja hivyo.
Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.
Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.
Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.
Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.
Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.
Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.
Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.
Mkurugenzi apatwa kigugumizi
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.
“Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo,” alisema Nyalile.
Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.
Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.
Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Wananchi walalama
Baadhi ya wananchi walikuwa wakiangalia majina hayo katika ubao huo walidai kuwa, baadhi ya maofisa wa halmashauri hiyo wamedaiwa kupewa rushwa wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo.
“Walitangaza kama kiini macho, lakini tayari walikuwa na majina yao ili waweze kuwapatia na jambo ambalo limejionyesha wazi kwenye majina ya watu waliopewa viwanja hivyo,” alisema mwananchi mmoja (jina tunalihifadhi) na kuongeza:
“Kutokana na hali hii, hatuna imani na viongozi wowote wa Serikali kwa sababu inaonyesha wazi kuwa, kila mmoja anaangalia masilahi yake na si wananchi wasio na kipato”.
Aliongeza kuwa, wananchi hawana imani na viongozi wao, hivyo Serikali inapaswa kuingilia kati kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha matatizo.
Mwananchi mwingine aliyekuwa akifuatilia jina lake alisema: “Wewe unachokiona ni nini hapo kama siyo yaleyale ya ubinafsi! Wewe unaamini kabisa kwamba kweli hawa viongozi wetu hawana nyumba au hawana viwanja hapa Dar es Salaam.
Aliongeza: ”Kama manispaa walitangaza viwanja ili wajiuzie wangesema tu badala ya kuchukua fedha zetu Sh30,000 halafu viwanja wakajigawia wenyewe.”
Mgawo wa Viwanja
Mapema mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza kwamba imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji Viwanja.
Fomu za maombi ya kununua viwanja hivyo zilianza kutolewa Juni 11 na kila mwombaji alipaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha Sh30,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.
“Fedha hizo hazitarejeshwa na mwombaji atajaza nakala mbili za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana,” linasomeka tangazo rasmi la manispaa hiyo.
Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la mradi ambao walikuwa wametambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, pia walitakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule.
 
Hili gazeti limepotoshwa umma; Vigogo waliopata viwanja ni 39 ama 2.16% ya watu 1,800 waliopata viwanja. Wasio vigogo ni wengi kuliko vigogo. Watz msiwe na kasumba ya kubwabwaja pasipo kuingia ndani kwa hoja
Mkuu tusiongopeane,hao walioandikwa kwenye gazeti ni wachache lakini ukisoma list kama alivyoiweka Edson,
asilimia kubwa ya majina ni ya viongozi au watoto wa viongozi,madiwani karibu wa manispaa zote za Dar,kwa
watu wa chini ni wachache,kwa taarifa yako hata wafanyakazi wa manispaa ya Temeke wenyewe ambao hawakuwa
na kigogo wa kuwapigia debe wamenyimwa,na majina yaliyotoka this time mengi yamejirudia waliouziwa awamu iliyopita.
 
Waligawana nyumba za serikali zilizokuwa na viwanja vikubwa tu. Hivi havikuwatosha! Wanagawana fedha na rasilmali nyingine za TAIFA hili kila siku. Hili nalo haliwatoshi. Wanagawana AJIRA nzuri zote serikalini na taasisi zake. Nalo hili haliwatoshi. Wanaanzisha makampuni ili kufanya biashara na serikali na taasisi zake. Hili nalo dogo. Wanagombea, wanateuana na kurithisha vyeo kwenye serikali, kwenye vyama vya SIASA, NGOs,..., nalo hili haliwatoshi! Tunahitaji UAMSHO kama ule wa nchi za KIARABU? Bahati mbaya kabisa na wapinzani wamo kwenye orodha hii. Tukimbilie wapi?
 
Jamani viwanja 1800, viwanja vya wanaolalamikiwa ni viwanja havizidi 50 inamana 1750 wamepewa walalahoi sasa malalamiko ya nini? mbona tumegeuka kama wale jamaa wanaolalamikia kilakitu? mi ningekuwa mojawapo ya wanaolalamika kama wangechukua viwanja 500.
 
Inasikitisha sana kusikia kuwa vigogo wengi wameendelea kuwanyonga walala hoi kwa kujigawia viwanja lukuki. Si kwamba hawa vigogo si watanzania lahasha! bali kuna shahidi mbalimbali zinazoonyesha jinsi vigogo walivyo na mashamba makubwa na viwanja vingi maeneo mbalimbali ya nchi. sasa inapotokea kila viwanja vinapopimwa tunaona majina ya vigogo wale wale au ndugu zao inakua inatia shaka sana!.
Naomba wahusika watufikirie na sisi walala hoi hasa has namsihi mkuu wa nchi atuangalie maana swala kama hili linazidi kutufanya walala hoi tuichukie serikalii
 
Viwanja vilikuwa vingapi? Hapo huu waliotajwa ni 39 tu. Ina maana viwanja vilikuwa hivyo tu au gazeti limeamua kuorodhesha vigogo tu? Nao si watanzania na hivyo wanastahili kupata viwanja hivyo? Tafadhali tupate na walalahoi waliopata ili kuona uwiano uliopo ndipo tuweze kutoa maoni yetu.
Viwanja zaidi ya 1800. Shida ni kwamba utayaona majina hayahaya au ya ndugu zao kila kutakapopimwa viwanja. Hili litatufikisha pabaya. Halafu eti wanasema tuache kuwatukana kwenye mitandao! Watufunge tu.
 
Jamani viwanja 1800, viwanja vya wanaolalamikiwa ni viwanja havizidi 50 inamana 1750 wamepewa walalahoi sasa malalamiko ya nini? mbona tumegeuka kama wale jamaa wanaolalamikia kilakitu? mi ningekuwa mojawapo ya wanaolalamika kama wangechukua viwanja 500.
Kwa nini watu walewale na ndugu zao kila inapotokea fursa ya viwanja, nyumba za serikali kuuzwa, NHC wanapojenga na kuuza nyumba, mashamba yote yanayoizunguka Dar,..., inaudhi na kukerehesha ati.
 
Viwanja vilikuwa vingapi? Hapo huu waliotajwa ni 39 tu. Ina maana viwanja vilikuwa hivyo tu au gazeti limeamua kuorodhesha vigogo tu? Nao si watanzania na hivyo wanastahili kupata viwanja hivyo? Tafadhali tupate na walalahoi waliopata ili kuona uwiano uliopo ndipo tuweze kutoa maoni yetu.

Mara nyingi walalahoi wanaopata hivyo viwanja ni wale wenyeji - ambao huwa lazima wapewe. Hivyo, katika viwanja 1,000 vilivyotangazwa, kuna idadi si haba ambayo inatengwa kwa ajili ya wenyeji ambao wanapewa kipaumbele. Hao wenyeji, kwa kuwa hawana uwezo wa kulipia, huwa wanafanya re-sale kwa bei juu kidogo zaidi ya ile ya manispaa ili nao wapate chochote. Kama una pesa kuanzia milioni 8 utapata kiwanja kutoka kwa hao wenyeji. So ukiondoa wale wenyeji, idadi kubwa ya wanaopata viwanja ni aidha vigogo, au wana connection na vigogo au wametoa mzigo mkubwa manispaa. Ndo TZ yetu hiyo!!
 
Waligawana nyumba za serikali zilizokuwa na viwanja vikubwa tu. Hivi havikuwatosha! Wanagawana fedha na rasilmali nyingine za TAIFA hili kila siku. Hili nalo haliwatoshi. Wanagawana AJIRA nzuri zote serikalini na taasisi zake. Nalo hili haliwatoshi. Wanaanzisha makampuni ili kufanya biashara na serikali na taasisi zake. Hili nalo dogo. Wanagombea, wanateuana na kurithisha vyeo kwenye serikali, kwenye vyama vya SIASA, NGOs,..., nalo hili haliwatoshi! Tunahitaji UAMSHO kama ule wa nchi za KIARABU? Bahati mbaya kabisa na wapinzani wamo kwenye orodha hii. Tukimbilie wapi?

Naamini huu ndio ufumbuzi wa matatizo ya nchii hii.
 
hii list uliyoweka ni ya awamu ya kwanza,ilitolewa zaidi ya miaka 2 iliyopita,humo ndani kuna Marehemu wengi tu.kwa viongozi wa serikali kupata less than 5% ya idadi yote ya viwanja sio kitu kibaya kama wengi wetu tunavyofikiria,kwani si wengi wenye uwezo wa kulipia hizo 15M kupata low density.
Upendeleo LAZIMA uwepo,ndio maana sehemu nyingi kunakuwa na VIP areas,stadiums,banks,airlines etc...,and most likely huwezi kumkuta asiye na uwezo maeneo hayo.kwa maslahi ya wabunge,mawaziri,kuweza ku-afford kiwanja cha 15M is like pocket change.Tupambane kuwe na transparency kwenye selection process,like first come first served basis mode of selection etc...,lakini mwisho wa siku mwenye pesa ndio ata-afford viwanja vingi etc...,nitashangazwa kama nitakuta waziri amechukua high density.lakini sitamlaumu.
 
Jamani viwanja 1800, viwanja vya wanaolalamikiwa ni viwanja havizidi 50 inamana 1750 wamepewa walalahoi sasa malalamiko ya nini? mbona tumegeuka kama wale jamaa wanaolalamikia kilakitu? mi ningekuwa mojawapo ya wanaolalamika kama wangechukua viwanja 500.

Vigogo, ndugu zao na marafiki wao ni zaidi ya nusu kwenye ile orodha. Tofauti ni hivi, mimi nikiomba kiwanja nitaambiwa vimekwisha lakini kigogo yeye hakosi na kigogo akipeleka orodha ya majina yake lazima yapate. Usiangalie majina unayoyafahamu tu, kuna shemeji zao, wajomba zao na rafiki zao. At the end rasilimali za nchi zinamilikiwa na familia chache
 
Ni wizi wa hali ya juuu, nadhani kwa isu ya temeke lazima tuwape wabunge wa upinzani hii hoja... kwa mpano wamekusanya fedha za form 12,000 ambapo kila moja waliuza 30,000/= hapo wanapata zaidi ya 360,000,000/=. wamegawa viwanja 1,040 tu na tu fanye assuption ya kuwa vyote vimeuzwa kwa bei ya chini kabisa ambay ilikiwa Tsh 4,800,000 wanepata 4,992,000,000 sasa hii nidhuruma kabisa

wamegawa viwanja 1440 kwa waliopata baada ya kuomba na viwanja 451 kwa waliokuwa na mashamba Gezaulole ni sawa jumla ni viwanja 1801 majina yote yapo kwenye ubao.
 
hapa katiba inabid ifanye kazi ya kuwafutia hati wenye site zaidi ya tatu.nimeona Smbody SUNZU,hv ni mTZ kweli huyu?
 
katika viwanja 1800 kama vigogo wamepata viwanja 100 ni haki kwani 1700 viwekwenda kwa watu wengine na isingewezekana wote walioomba wapate.

jambo la msingi, Manispaa waeendelee kupima kwa kasi ili kukidhi kiu ya wananchi wanaotaka kupata viwanja vilivyopimwa
 
Hili gazeti limepotoshwa umma; Vigogo waliopata viwanja ni 39 ama 2.16% ya watu 1,800 waliopata viwanja. Wasio vigogo ni wengi kuliko vigogo. Watz msiwe na kasumba ya kubwabwaja pasipo kuingia ndani kwa hoja

well said
 
Back
Top Bottom