Leon BahatiMAKAMISHNA watatu wa Idara ya Uhamiaji nchini, wamesimamishwa kazi ikiwa ni siku 20 tangu Waziri wa Mambo ya Ndani , Shamsi Vuai Nahodha atangaze kufanya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya idara hiyo.
Januari 17 mwaka huu, Nahodha alitangaza kufanya mabadiliko katika idara hiyo ili kuongeza tija na kukabiliana na mambo mbalimbali ikiwemo kudhibiti uingiaji nchini wa wahamiaji haramu.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi, umebaini kwamba makamishna hao watatu (majina tunayo) jana walipewa barua za kuondoka kwenye nafasi zao na kutakiwa kuripoti wizarani ili kupangiwa kazi nyingine.
Hata hivyo, baadhi ya watumishi wa idara hiyo wamechukulia uamuzi huo wa kusimamishwa kazi makamishna hao kama wa kisiasa."Uamuzi huu umefanywa kisiasa.
Nafikiri hawa wakubwa wana watu wao ambao wanataka kuja kuwaweka kwenye nafasi hizo," alisema mmoja wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji, kwa ombi la kutotajwa gazetini.
Source: Mwananchi