Vigogo ‘urais’ 2015 wakimbilia Kanisa; Samuel Sitta, Edward Lowassa, Frederick Sumaye

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1]Vigogo ‘urais’ 2015 wakimbilia Kanisa[/h]
Mwandishi Wetu


main215.jpg



Samuel Sitta, Edward Lowassa, Frederick Sumaye


Wayatumia kisiasa, nao watumika kifedha


MTANDAO wa makanisa nchini, yakiwamo yale makubwa, sasa yameanza kujinufaisha na wanasiasa; kama ambavyo wanasiasa hao wanavyolenga kukidhi matarajio ya kisiasa kupitia makanisa hayo, Raia Mwema limeelezwa.
Wakati hali hiyo ikishika kasi; huku wanasiasa na hasa kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), wakianza kupigana vijembe kupitia majukwaa ya makanisa, kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki ametolea ufafanuzi hali hiyo akisema: “Si dhambi viongozi au mtu yeyote kualikwa kusaidia jamii kwa hali yoyote”.
Kiongozi mwingine kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye kama ilivyo mwenzake wa Kanisa Katoliki, hakutaka kutajwa jina kwa sababu si wasemaji rasmi wa makanisa hayo, ameeleza: “Ni vigumu kujua nia iliyojificha ya mtu anayetoa msaada, lakini jambo la kuangalia ni wema wa tukio lenyewe la kusaidia jamii au kanisa.”
Gazeti hili limefuatilia nyendo za wanasiasa kadhaa na kubaini kuwa ingawa wamekuwa wakipewa mialiko ya kushiriki shughuli mbalimbali za makanisa na hasa uchangishaji fedha (maarufu kama harambee), wanasiasa hao wamekuwa wakitumia majukwaa hayo “kupigana vijembe” dhidi ya mahasimu wao wengine wa kisiasa.
Akiwa mkoani Singida kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Amani, Sabasaba, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa, alitumia fursa hiyo kupiga vijembe wenzake ikiwa ni siku chache baada ya kukamilika kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi.
Ni katika vikao hivyo ambamo Lowassa anatajwa sasa kuwa alipata wakati mgumu kisiasa ikiwa ni pamoja na kushinikizwa ajiuzulu nafasi zake chamani, kwa sababu ya tuhuma za ufisadi zinazotajwa kumuandama.
Akitumia jukwaa hilo la kanisa ambako alialikwa kuongoza harambee, Lowassa alipiga vijembe vya kisiasa akisema: “Wale wanaofuatilia siasa za nchi yetu kuna maneno mengi saana, lakini Bwana ni mwema na mwaminifu hatimaye tumeshinda.”
Lowassa, ambaye ni mbunge wa Monduli, alisema kuwa maneno mengi aliyoyaita ya kisiasa yamekuwa yakisemwa juu yake lakini kimsingi maneno hayo ni siasa mwendelezo wa kuchafuana.
Hata hivyo, maelezo hayo ya Lowassa yametafsiriwa kuwa ni mkakati wa kujisafisha dhidi ya tuhuma zinazomkabili na kwamba mwelekeo wa mkakati wake ni kugeuza shutuma hizo kutoka za ufisadi hadi za kisiasa na zaidi, inadaiwa kuwa ni kuhusisha siasa hizo na mbio za kuwania urais 2015.
Lakini baada ya kufikisha ujumbe wake wa kisiasa aliokusudia kwenye harambee hiyo KKKT-Singida, Lowassa alisema: “Nimekuja kwenye harambee sio kupiga maneno ya kisiasa.”
Katika harambee hiyo, Lowassa alifika kwa mwaliko wa Askofu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kati, Mchungaji Eliufoo Sima, ambaye naye hakuingia moja kwa moja kwenye mtego wa kisiasa; bali alihimiza juhudi za pamoja miongoni mwa wananchi kukabili hali ya umasikini iliyopo.
Lakini wakati Lowassa akiwa katika jukwaa hilo na mengine aliyowahi kuyafikia kwa daraja la harambee, hasimu wake, ambaye anatajwa kuwa ni kinara wa kupambana na ufisadi, Spika wa zamani na Waziri wa sasa wa Uhusiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, aliibukia Kanisa Katoliki mkoani Arusha, Parokia ya Mtakatifu Theresa.
Akiwa hapo mwisho mwa wiki iliyopita Sitta katika kile kinachoelezwa kujibu mapigo ya Lowassa kuwa kuna watu wanamchafua kisiasa na si kwa ufisadi, Sitta hatarajii kutumia jukwaa hilo kuomba radhi au kujisafisha kwa sababu hana sababu ya kufanya hivyo; kwani yeye ni mwaminifu na wananchi wanatambua hilo.
Baadhi ya magazeti yalimnukuu Sitta akisema: “Wananchi wanatambua viongozi wenu ambao ni waadilifu na pia mnawatambua wale wengine, sitarajii kulitumia jukwaa hili kwa kufanya hivyo ingawa ninayo mambo mengi ya kisiasa ya kuzungumza. Wananchi mnatujua hata tukisemaje.”
Katika hatua nyingine taarifa ambazo limelifia gazeti hili zinaeleza kuwa Waziri Mkuu mwingine wa zamani, Frederick Sumaye, naye amealikwa kwenye moja ya hafla za moja ya makanisa nchini mwishoni mwa wiki hii.
Ingawa taarifa hizo hazijaeleza rasmi atakachozungumza Sumaye, lakini ni dhahiri kuwa anaweza kufafanua baadhi ya maelezo ‘yaliyochomekewa’ kwake kuwa katika kikao kilichopita cha NEC-CCM aliwatetea watuhumiwa wa ufisadi, na hasa wale ambao CCM kimepanga kuwahoji kupitia Kamati yake ya Maadili ili kuchukua uamuzi wa ama kuwafukuza au kuwaacha kubaki katika chama hicho kikongwe nchini.
Hata hivyo, ingawa wanasiasa hao wamekuwa wakitajwa kuwa na ndoto za kutaka kuwania urais na hasa kwa tiketi ya CCM, lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyekwishatangaza nia hiyo.



Si






 
naona tunataka kuwa kama kenya mpaka kwenye misiba, lakini naona jambo hili likemewe, (lipigwe marufuku) maana yatanza ya makanisani baadae yatafika kwenye misikiti nk nk
 
naona tunataka kuwa kama kenya mpaka kwenye misiba, lakini naona jambo hili likemewe, (lipigwe marufuku) maana yatanza ya makanisani baadae yatafika kwenye misikiti nk nk
Kila mmoja ana shida zake kwa mwenzie. Maaskofu wanashida sana ya pesa, na hao 'jamaa' wanashida sana ya 'kusafishwa'. Wacha tuendelee kuangalia maigizo tu. Hapo hamna kitu cha maana! Rais mtarajiwa nahisi atakuwa mwanamama 2015. Ngoja tuone!
 
mbona huzungumzii waliokimbilia Misikitini????? Wote uliowasema ni Wakristo ulitaka waende Misikitini??????
 
hawa wote ni Wakristo tatizo liko wapi kwani wanakwenda kutangaza nia ya uraisi makanisani au ni mwiko kwa kiongozi wa juu kuhudhuria kanisani na kushirikiana na wakristo wengine

tusiwe biased kihivyo wakuu
 
Udini wa CCM unajionesha wazi kabisa kua upo kwenye Chama chao tizama hali ilivyo sasa sabbu awali walisema CDM ndio wadini lakn inajionesha wazi kua wao ndio wadini zaidi
 
mbona huzungumzii waliokimbilia Misikitini????? Wote uliowasema ni Wakristo ulitaka waende Misikitini??????
Habari hii imechukuliwa kutoka kwenye gazeti la Raia Mwema. Sasa unamlaumu muanzisha uzi kivipi? Acheni huo UDINI wenu!
H
 
Back
Top Bottom