Vigogo serikali waanza kuyanyemelea majimbo

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Hekaheka za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 zimeanza kwa kasi katika majimbo saba yaliyopo mkoani hapa kwa baadhi ya vigogo wa taasisi za serikali kuanza kujiimarisha kiasiasa kwa jipitisha kwa wananchi kwa kutoa zawadi na fedha.

Vigogo hao ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamekuwa wakitumia misiba kama mitaji yao ya kujitangaza kwa watu wanaoishi kwenye majimbo hayo na kuweka wapambe na wapigadebe katika vitongoji na vijiji.

Imebainika kuwa wapambe na wapigadebe hao wamekuwa wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maeneo hayo na kutoa taarifa kwa wanachama hao ambao ni wazaliwa wa Mkoa wa Mbeya.

Inapotokea wanapata taarifa za misiba, wanachama hao ambao wameanza kujipanga kupambana na wabunge wa CCM kwenye kura za maoni za chama hicho, hujitokeza haraka haraka kwenye maombolezi na kutoa rambirambi na zawadi kama njia ya kuwashawishi wananchi ili wawachague.

Majimbo yaliyoanza kuvamiwa kwa kasi na wanachama hao ni la Mbeya Mjini linaloongozwa na Mbunge Bensony Mpesya, Rungwe Magharibi, Profesa David Mwakyusa, Rungwe Mashariki, Prof.Mark Mwandosya, Mbeya Vijijini, Luckison Mwanjali, Mbozi Magharibi, Dk.Luka Siame, Songwe Dk.Guido Sigonda na Lupa, Victor Mwambalaswa wa CCM.

Wanachama hao wamekuwa wakionekana wakifanya ziara za siri na kutoa misaada kwa wakazi wa majimbo yao huku wakieleza bayana kuwa lengo lao la kutaka kugombea ubunge.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Albert Mgumba alipoulizwa na Nipashe alisema wanachama hao wanakiuka utaratibu wa chama hicho kwa kuanza mapema kujipitisha kwa wananchi kwa kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika.

Source: NIPASHE
 
Back
Top Bottom