Vigogo mafisadi H/W Rombo wapandishwa kizimbani

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Daniel Mjema, Moshi | Mwananchi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), leo inatarajia kuwaburuza kortini vigogo watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za ufisadi.

Ripoti ya ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Setikali (CAG) kati ya Julai 2007 na Juni 2009, ilibaini wizi na ubadhirifu wa zaidi ya Sh900 milioni.

Mkuu wa Takukuru wilayani Rombo, Chuzela Shija, alithibitisha jana kuwa watumishi hao watafikishwa mahakamani leo kwa tuhuma mbalimbali zinazohusiana na makosa ya jinai.

"siwezi kukuambia watashtakiwa kwa makosa gani, lakini ni kweli kesho (leo) tutawafikisha mahakamani hapa Rombo watumishi wengine watano wa halmashauri," alisema Shija.

Kufikishwa mahakamani kwa watumishi hao kunakuja mwezi mmoja tu tangu vigogo wengine saba wa halmashauri hiyo kuburuzwa kortini kujibu mashtaka 120 ya wizi na kughushi nyaraka.

Watuhumiwa hao ni Mhandisi Felician Msangi (49, Emannuel Masele (40) ambaye ni Mhasibu, Rachel Mshangila (48) ambaye ni Ofisa Ugavi Msaidizi na Silvia Shirima (46) ambaye ni Ofisa Ugavi.

Wengine ni Pere Muganda (50) ambaye ni Mhasibu, Joseph Ngoseki ambaye alikuwa ni Ofisa Elimu wa Halmashauri na Mkuu wa Sekondari ya Rongai na Mussa Mruma (54).


My take;
tunataka watu wa namna hii wafungwe sio waishie kufikishwa mahakamani tu.haki ionekane ikitendeka,sio itendeke kwa maneno.
 
Naiomba serikali iweke muda maalumu wa kusikilizwa kwa kesi za namna hii ili zijulikane mbichi na mbivu in a specific period of Time and not undefined period of time.
 
Back
Top Bottom