Vigogo Chadema wahamia CCM

Kama ni kweli nina wasiwasi na nia ya hawa watu kwani huko ccm walikuwepo kabla, nini kiliwatoa na leo nini kinawarudisha? Hivi mtu atapike matapishi yake halafu kabla hayajakauka anayarudia. Hao hawafai kuwa viongozi katika jamii hata katika familia zao nina wasiwasi wamezitelekeza kwa kuogopa kuwajibika. Tuwe makini kuwatambua hawa watu.
 
Halafu mapoyoyo kibao, wanajifanya wasomi kumbe hata maana ya neno KIGOGO kwa maana ya kisiasa hawajui. Wanajua viongozi wa ngazi ya taifa pekee ndiyo vigogo. Hata balozi wa nyumba kumi ni kigogo pia, kigogo wa eneo lake la utawala.

Huenda huko kwenu CCM kila mtu anajiita na kujiona KIGOGO wa chama..Huenda hii ndio sababu,kila mtu ktk chama chenu anajiona anaweza kugombea urais mwaka 2015 achilia mbali ubunge ama udiwani.
Hao jamaa hawawezi kuwa VIGOGO iwe kwa tafsiri ya BAKITA ,TUKI ama hata kwa kiswahili cha MTAANI.Hapana.
 
Huenda huko kwenu CCM kila mtu anajiita na kujiona KIGOGO wa chama..Huenda hii ndio sababu,kila mtu ktk chama chenu anajiona anaweza kugombea urais mwaka 2015 achilia mbali ubunge ama udiwani.
Hao jamaa hawawezi kuwa VIGOGO iwe kwa tafsiri ya BAKITA ,TUKI ama hata kwa kiswahili cha MTAANI.Hapana.

Na wewe si unamadaraka makubwa katika familia yako? Ni kigogo wa familia.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi kimepata pigo la kuondokewa na viongozi wake wawili, akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya,Hassani Mkopi na katibu wake,Saadati Kamalu.

Viongozi ambao wameachia ngazi na kujiunga na CCM kwa madai ya kushindwa kukitumikia vema chama hicho tangu walivyokabidhiwa madaraka kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Katibu wa muda wa Chadema, Jordani Membe alisema juzi kuwa Mkopi alijiondoa Chadema na kujiunga na CCM mwishoni mwa mwezi uliopita wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal katika Kijiji cha Chiumbati, Kata ya Naipanga.

“Tukiwa katika mkutano huo katika Kijiji cha Chiumbati, ghafla mwenzetu aliamua kujivua gamba la Chadema na kulivaa lile la CCM kwa kumpatia Dk. Bilal kadi yetu ya Chadema,” alisema Membe.

“Katibu wetu Kamalu amedai ameamua kujiuzulu baada ya kushindwa kukitumikia vema
chama kama alivyokabidhiwa na wanachama wakati wa uchaguzi uliopita,” alisema akinukuu kauli yake.

Kutokana na kujiuzulu kwa Kamalu, Kamati ya Utendaji kwa kushirikiana na Baraza la Wazee wa Chadema waliamua kufanya uteuzi mdogo wa kuziba nafasi hiyo, ambapo Diwani wa Kata ya Nkotokuyana, Likolovero Hassani alichaguliwa nafasi ya uenyekiti, na yeye Membe aliteuliwa kushika nafasi ya ukatibu wa muda.

Membe alisema viongozi hao watashikilia nafasi hizo hadi Uchaguzi Mkuu wa Chadema utakapofanyika mwaka 2013, badala ya 2014 kutokana na mabadiliko mafupi yaliyofanyika kwa lengo la kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za vijiji, vitongoji na mitaa

HABARILEO

Naelewa mashabiki wenzangu hampendi kuona hii,lakini ndio uhuru wa habari ulivyo

Hapana Bwana, ni haki ya hao jamaa kuhamia chama cho chote kile. Eneo hilo hata ukiniambia Mwenyekiti wa mkoa kahamia CCM siwezi kushangaa kwa kuwa ni watu wenye dhiki. Ni wepesi kubadilishwa sana na pesa. Naamini hao wengine watafanya kazi. Nawashukuru wamekuwa wawazi kwa kusema wameshindwa kazi. Chadema inahitaji wachapa kazi sio wanaosubiri posho tu. CCM ndiko watu wanakimbilia posho kwa kuwa pesa zinachotwa katika kila wizara na kumwagwa huko. Hao mabwana wawili wako very strategic kwa kuwa wanajuwa ccm itaanza uchaguzi hivi karibuni kwa hiyo pesa zitachotwa sana. Lets wait and see.
 
fikra hasi na mgando,na upo uwezekano kuwa huna kadi ya CDM wala bendera,umekuwa vuvuzela lisilo na madhara na hata ktk daftari la wapiga kura haumo,lakini ndani ya JF kelele kibao tena zisizo eleweka kama bubu vile mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh,lalalalalalala,Hueleweki mkuu
POle sana ndugu yangu, wewe unafiria kuwa kadi na bendera ndo inapiga kura? 2010 wana ccm na bendera zao waliipigia CDM kura wakisema ccm wamekuwa wasanii sana. Ndo maana leo hii wabunge wengi wa upinzani wameongezeka. Naomba uamke. Sikatai wewe kuendelea kuwa mwana ccm lakini ktk mambo yenye maslahi na nchi tafadhali uwe very analytical.
 
Back
Top Bottom