Vigogo CCM waliowahi kwenda upinzani wakarudi tena CCM

Wana JF,

Kwa kuwa historia ya nchi yetu huwa haindikwi vizuri, mimi ninaomba nisaidiwe kufahamu vigogo wa CCM waliowahi kutimukia upinzani tangu tuanze mfumo wa vyama vingi 1992 na baada ya mambo kuwa magumu wakarudi tena CCM. Je hao vigogo walikuwa wanasimamia msingi ipi? au walikuwa ni Political opportunist. Haya ni mambo muhimu sana ya kutafakari, kwani kutokana hali inavyo kwenda ndani ya CCM huenda CDM 2015 ikapata mafuriko ya "WAKIMBIZI wa kisiasa" kutoka CCM.
  1. Steven Wassira (NCCR)
  2. John John Guninita (CDM)
  3. Abass Mtemvu (NCCR)
  4. Adam Malima (NRA)
  5. Samuel Sitta (CCJ)
  6. Nape Nnawiye (CCJ)
  7. Dan Makanga (UDP)
  8. Dr. Amani Warid Kaborou (CDM)
  9. Dr. Masumbuko Lamwai (NCCR)
  10. Chief Abdallah Fundikira (UMD)
  11. Tambwe Hiza (CUF)
  12. Ibrahimu Msabah (CUF)
  13. Nalaila Jidawi (CUF)
  14. Dr. Ngunangwa (NCCR)
  15. Makongoro Nyerere (NCCR)
  16. Gulamhussein Kifu (NCCR)
  17. Daniel Nsanzugwako (NCCR)
  18. Sambweee Shitambala (CDM
  19. Deo Lwekama (TLP)
  20. Thomas Ngawaiya (TLP)
  21. Anna Senkoro (TPP Maendeleo)
  22. Prince Bagenda (NCCR)
  23. Dr. Festus Limbu (NCCR)
  24. Amani Nzugule Jidulamabambansi (UDP/RIP)
  25. Thomas Nyimbo
  26. Frank Magoba (CUF)
  27. Evodius mmanda
  28. Thadeus Mtembei
  29. Justine Salakana (CDM)
  30. Kilimbah
  31. Shaibu Ally Akwilombe (CUF)
  32. Njelu Mlagala Kasaka (CUF)
  33. Fatuma Maghimbi (CUF)
  34. Clement Mabina

Pale pekundu nimepapenda, nakuona ni kama mtabiri mashuhuri usiyevuma lakini umo! Ulitabiri mwaka 2012 na utabiri umetimia mwaka 2015, hongera sana Mkuu.
 


Pale pekundu nimepapenda, nakuona ni kama mtabiri mashuhuri usiyevuma lakini umo! Ulitabiri mwaka 2012 na utabiri umetimia mwaka 2015, hongera sana Mkuu.

huyu jamaa hatari sana,nashukuru tu akutabiri kama je itashinda CDM, hivyo CCM itabaki madarakani
 
Huyu John John Guninita kwenye miaka ya 80 ulianzishwa usafiri wa wanafunzi Dar na yeye alikuwa ndiye msimamizi na wakati ule alikuwa Katibu wa Vijana wa CCM wa Mkoa wa Dar,waliufilisi mradi ule baadae akakimbilia CDM akaona hafaidiki CDM akarudi tena CCM sasa hv tena anakimbilia tena CDM asipopata maslaj atahama tena,ni changudoa wa kisiasa huyu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom