Vigogo 60 serikalini kuhakikiwa mali zao, yumo Samuel Sitta

Sugu na Mnyika?hapa sidhani kama hawa wako seriously nilitegemea watu kama hawa wawe wa mwishoni maana uhakiki wao utakua mwepisi ukilinganisha na Lowasa,chenge,Sumaye,Mkapa,Mwinyi,Mboma,Mwamunyange,mkuchika,dr.nchimbi,brandina nyoni,kalamagi,msabaha,Jairo,Ruhanjo(aliyekua katibu kiongozi),endeleza list hapo...........
 
Hizi kamati uchwara zinazoanzishwa kila siku kwa ajili ya kujinufaisha zinazidi kutuletea maudhhi. Swala la mali za viongozi ni zoezi ambalo Watanzania tupo tayari kujitolea bila kulipwa chochote tuweke mambo wazi. Hatuhitaji list toka kwa kurugenzi yoyote kazi itafanyika kwa ukweli na uwazi zaidi. Baada ya hapo tutawawajibisha wenyewe...hizi kamati hazina lolote uozo mtupu....WATZ. TUNAYO MAMLAKA UWEZO NA JUKUMU LA KUWAFICHUA WEZI SUGU WA MALI YA WATZ. hatutaki mahakama wala mjomba wake hakimu bana tumechoshwa na hizi ngonjera za kila siku kibwagizo ni hicho hicho tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Eti tume ya maadili ya uongozi na uozo huu wote nchini; my foot!!!!!!!!!

What a waste of time and money katika zoezi lililokwisha feli kabla halijaanza!! Hiyo tume iliwahi kufanya wapi kazi zake kwa mujibu wa sheria na zikapata kuheshimika na wote bila maswali kujitokeza kwa wingi zaidi kuliko majibu???

My foot; bure kabisa na wala hatutegemei chochote humo.
 
Nawashangaa! Kwa nini kina wanachotaka kufanya watangaze? Kwa nini wanatoa orodha ya VIGOGO? Kwani wakiwafuatilia na kuwachunguza watutangazie majibu itakuwaje? Mwaka jana waliwakagua kina Mukandara (VC UDSM), matokeo yake tuliambiwa? Wanapoteza watu maboya ili waangalie na kujadili ORODHA ya VIGOGO baadae WASAHAU! Haya viwanja vya Burka, wako wapi VIGOGO walioripotiwa kujinyakulia viwanja? Kwa mujibu wa taarifa magazetini wiki hii HATUWAONI wale walotajwa mwanzoni! Kuna ni hapa?
 
kwa nini wasiwakague watumhumiwa wa ufisadi kwanza mfano Mh Lowassa uwezo wake kifedha ni questionable sana kwa mwanasiasa ambaye hadi 1989 alikua na maisha ya kawaida leo ana nyumba zaidi ya 10 dar, na nyingi zingine Arusha hizi ni nyumba tu ranch ya mifugo kubwa, machimbo ya madini, telecom co., maghorofa ya biashara mawili matatu hapa mjini..hata kama ni zoezi la kila mwaka sasa kama kuna watuhumiwa na chama chao tena kwa nini wasiwe focus ya mwaka/wakati huu? hii nchi kweli ni clown country
 
Kwenye Msafara wa ng'ombe 100 wanaopelekwa machinjioni lkn wanaokusudiwa kuchinjwa ni wawili tu
 
Back
Top Bottom