Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Vigogo 23 kortini kwa kutotangaza mali zao
Imeandikwa na Na Halima Mlacha; Tarehe: 11th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 55; Jumla ya maoni: 0
VIONGOZI wa Umma 23 wanatarajiwa kusimama mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwa ajili ya kujitetea kutokana na kukiuka Sheria Namba 13 ya Maadili ya Viongozi
wa Umma kwa kutowasilisha tamko la rasilimali na madeni yao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Miongoni mwa viongozi hao wamo watendaji wakuu wa Ofisi ya Rais Ikulu, wakuu wa taasisi nyeti nchini, wakuu wa wilaya, mahakimu, madiwani, wakaguzi wa hesabu wa ndani na wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za wilaya.
Kwa mujibu wa orodha ya Sekretarieti hiyo kwa Baraza la Maadili, vigogo hao wanaotajwa kuitwa na watahojiwa ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini, John Mongella na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa
Ndani wa Ikulu, Hammad Ntungwabona.
Wengine ni Mhasibu Mkuu wa Ikulu Joseph Sanga, Mwandishi wa Habari Mkuu wa Waziri Mkuu, Said Nguba, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Ndani wa Shirika la Majisafi na Majitaka
Dar es Salaam (Dawasco), Rosemary Lyamuya na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Ndani wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Guido Leshabari.
Aidha, orodha hiyo pia imewataja Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Gabriel Mirumbe, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Endasak Katesh mkoani Manyara, Anthony Hamza, Hakimu Mahakama ya Mwanzo Mbulu Tharcisiusy Mwalulefu, Hakimu Mahakama ya Mwanzo
Mpanda Adam Mteru, Hakimu Mahakama ya Mwanzo Geita, Geraz Mulugilwa na Hakimu Mahakama ya Mwanzo Geita, Sabato Bwire.
Viongozi wengine watakahojiwa ni madiwani wa kata ya Nkome Geita, Kalema Chilatu, wa Rorya Yamo Kagose, Shinyanga Joseph Shoto, Mondo Kishapu John Ndama na diwani kutoka Halmashauri ya Monduli Arusha, Dorah Kipuyo.
Aidha, tayari Baraza hilo limeanza kuwahoji baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kutorejesha fomu za tamko la rasilimali na madeni yao ambao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Mbulu, Simon Mayeye, Mkuu wa Wilaya ya Singida Paschal Mabiti na Mbunge wa Rorya, Lameck Airo.
Msaidizi wa Rais katika masuala ya Siasa, Rajab Luhwavi hakutokea katika kikao hicho Jumatatu, na Baraza limetoa amri ya kukamatwa kwake na Polisi na kufikishwa mbele yao kwa ajili ya mahojiano baada ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi kutoa ombi hilo kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Akijitetea mbele ya Jopo la majaji watatu wastaafu ambao ni Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji mstaafu Damian Lubuva, Jaji mstaafu Balozi Hamis Msumi na Katibu Mkuu mstaafu Jaji
Deodatus Tibakwetura, Mabiti alikiri kutowasilisha fomu ya tamko lake la mwaka 2009 na kuliomba baraza hilo limsamehe kwa kuwa hatorudia tena.
Mimi ni kiongozi wa siku nyingi na naomba nitamke mbele ya baraza hili tukufu kwa ukweli wangu kuwa, tamko la mwaka 2007 na 2008 nilijaza na kuwasilisha kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Maadili Kipacha, na tamko la 2009 kwa kweli nilipitiwa sikuliwakilisha,
alisema Mabiti.