Vigezo. . .

Lolzzz BAK. . . usasa unatuchosha wenyewe tunauleta na kuuendekeza. Demands ziko juu kama mlima Kili.

...We acha tu Lizzy wengine hushindwa kupata wenzi wao wenye kufikia vigezo vyao wakija stuka muda nao umeshawatupa mkono.


 
Last edited by a moderator:
Tofauti na zamani siku hizi vigezo vya mwanamke kumkubali mwanaume ili awe mume na baba watoto wake vimeongezeka maana wadada wanajanjaruka siku hadi siku. Zamani muhimu ilikua 1. Anatoka kwenye familia nzuri. 2. Hawana matatizo ya akili/magonjwa ya kurithi 3. Ana kashamba kake kama sio kanyumba hata ka udongo na mengine yangejiset baadae.

Siku hizi bana vigezo vinatofautiana kuendana na aina fulani ya wanawake.

a) Miss dependent
1. Uwe 'mwanaume' hata kama ni kwa muonekano tu.
2. Uwe na pesa.
3. Uwe tayari ku-act kama mzazi wake maana anakuhitaji kwa kila kitu.

b) Miss independent (Miss Jeuri. .sio mjeuri). . .maana sio tegemezi kifedha, kihisia wala kifikra.
1. Uwe mwanaume kamili. . .hataki tabu.
2. Kichwani kuwe na kitu cha maana. . .
3. Muonekano wa kumridhisha (yaweza kuwa vyovyote) . . .
4. Uwe na heshima kwake. . .
5. Usiwe mgomvi
6. Uwe mwaminifu
7. Uwe tayari kukosolewa/kuwekwa sawa.
8. Uwe na maisha yanayoeleweka.
9. Uwe mwelewa.
10. Uwe safi kitandani.
11. Uwe msikilizaji mzuri.

c) Miss Erotica (@Erotica haki zimehifadhiwa mwaya)
1. Be good in bed. . .
Mengine mbele kwa mbele.

d) Miss Desperate.
1. Mwambie "NTAKUO/NATAKA KUKUOA".
2. Kuwa na kanyumba ka kumweka hata kama ni cha kupanga.
3. Ongelea maswala ya kumpa mimba.

e) Miss Certificate
1. Kuwa na degree
2.Kuwa na PhD. . .
3. Itwa Dr. , Eng. , Prof. Fulani
4. Kuwa na vijisenti kidogo
5. Ongea kiingereza

f) Miss 'Born again'
1. Uwe mkristo.
2. Ujiite mlokole.
3. Upende maongezi yamhusuyo Mungu.
4.Upende kwenda kanisani na shida/mapungufu yako yote yataonekana ni 'mpango wa Mungu'.

JB WISER. . .there you go . . .
Mh hakuna type nyingine? Maana katika hizo ulizozitaja hapo mi hakuna hata moja ninayoitaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom