Vigezo vitakavyotupa Rais bora 2015 (Dini, Muungano, kipato, elimu, Katiba Mpya, wafadhili)

Issue ya kuandika kitabu mi siiungi mkono kwa kuwa anaewza kuwakodisha wataalamu wazuri wakamwamndikia kila kitu kilicho bora kwa kiwango kikubwa sana. Yapo maandishi mengi sana na mazurimfano research works ambazo ni reliable and valid,lakini hakuna anayezifanyia kazi. Hapa ni wagombea kuwekwa kitimoto, maswali ya papo kwa papo kwenye mikutano na vipindi vya luninga kama ilivyokuwa kwa mkoa wa Arusha uchaguzi uliopita
 
Kura yangu ya urais 2015 nampgia zitto au membe kama hawatogombea ntapga kura ya udiwani na ubunge tu wachadema ya urais nitaiacha kwani sioni mgombea bora zaidi ya hao.
 
yupo aliyetayari kumlipa mtu amuandikie kitabu, halafu yeye anaki-kariri. Sema kwenye kujibu maswali ya wakufunzi na wana-vyuo itabidi atafute mbinu.
.
Mkuu hapo nakupa 100%, hoja ya kuandika kitabu ni dhaifu sana,kama vile tulivyoshupalia uadilifu tukazani kuwamwadilifu pekee inatosha. Pamoja na kuandika kitabu, katika mfumo huu uliooza tunahitaji mtu jasiri, mwenye maamuzi, anayeweza kukemea na sio tatizo limetokea anasimulia tena tatizo, katika hatua mbalimba iwe za chama au serikali amefanya nini. Hivi fisadi aliyethibitika awe rais 2015 kwa sababu tu ameandika kitabu?; Maoni yangu asitoke chama tawala kwasababu " He/she can't swim against the current".
 
Hatuhitaji mgombea urasi ambae jk akibadili miwani au sauti naye anabadili ili wafanane, akipunguza nywele nae kaiga, hatuhitaji mgombea ambaye maneno anayoongea hayatoki rohoni, mgombea ambae ana jukumu la mahusianoya kimataifa, badala ya kuyaboresha anaomba talaka na kutaka uadui na majirani, je angekuwa rais jumuiya ya afrika mashariki ingekuwepo leo? Hizo gharama zilizopotea angezitoleaje maelezo, hapo tu ameshindwa kuhimili, akipewa pakubwa si ataomba talaka kila mahali

Umeona eeee! Jamaa anaiga mpaka style ya kutembea,Smile ya jk, anatamani kujichubua ili afanane na jk, Joka la Mdimu,Chui wa Karatasi,. Pale Foreign Affairs siku hizi ameanza kujichanganya na staff wa kawaida kama alivokuwa jk, All in All Rais wetu wa Tano Mungu akipenda ni Mh.Ndugu Mpendwa,Mzalendo,Mchapakazi,Jasiri,Mweledi,Mvumilivu,Mtu wa Watu Comrade Edward Ngoyai Lowassa.
 
All in All Rais wetu wa Tano Mungu akipenda ni Mh.Ndugu Mpendwa,Mzalendo,Mchapakazi,Jasiri,Mweledi,Mvumilivu,Mtu wa Watu Comrade Edward Ngoyai Lowassa.

Umesahau sifa zake muhimu sana.

Mwizi wa Mali za Umma na Kiongozi wa Magenge na Mitandao ya Kiharifu hapa nchini Fisadi Edward Ngoyai Lowassa.
 
Khe!sasa mie ambaye siwezi kusimama mbele za watu na kudefend hata maswali matatu si ntaomba misikiti na makanisa yanipigie tu kampeni alafu mie ningoje kuapishwa? ama mnasemaje watanzania,si tulifadhaika wote jamani?
 
Maccm yanavyojua kudesa yakiongozwa na mchumi kilaza mwigulu wataenda kutafuta mtaalamu awaandikie kitabu. Nyambafuuuuuuu. Kelebu.
 
Membe ni mzuri kuliko Lowassa kwa mbali sana kama tunabisha tuifanye debate pale chuo kikuu kujadili mambo yote ya nchi uwekezaji wa madini, mafuta, ufisadi, uwezo wa kuongea na wawekezaji na ulinzi.
 
Rais ajaye wa Tanzania (na hasa yule wa Tanganyika) ni sharti awe na majibu ni kwanini nchi yetu ni maskini huku tuna rasilimali za kumezewa mate na mataifa mengine! Ni sharti awe na uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa! Utaratibu wa kubebana natamani nione ukikoma 2015 tukiwa na Tanzania na Tanganyika mpya!
 
mkiikuuza hii picha mtakubaliana nami kuwa wakati ukifika wananchi hatutaki kuhutubiwa, tunahitaji kuwauliza maswali wanaotaka tuwaajiri top post.

ili wasituhonge mikutano tutaiandaa sisi wenyewe tuwaweke kikaangoni. maswali hayapatikani vyuoni pekee, hata vijijini maswali yapo.

hapo umeonyesha uwezo mkubwa wa kufikiri.
 
Kama Membe anaweza kuwa rais, basi Tanzania itabidi kuomba sana maana miaka 5 itakuwa kama miaka 50.
We don't have leadership vaccum! Katika kipindi chake kama waziri wa Mambo ya Nje tumeshuhudia kwa mara ya kwanza mkuu wa diplomasia kutangaza vita na majirani wa Malawi badala ya kuwa mwanadiplomasia. Hili linaonyesha jinsi anavyokurupuka hata kwa yasiyo mhusu.
Kama mtu aliyefanya kazi ya ushushushu (intelligence) kukurupuka ni kati ya vigezo muhimu vya kumuondoa kwenye wadhifa alionao hata nyingine.
Mabalozi wa nchi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao wote kasoro mmoja tu wanamuona mbabaishaji, mtaka sifa na asiyejibu anachoulizwa.
Katika hili, namwomba Mola atuepushe naye vinginevyo atatusababishia matatizo mengi kuliko kutatua yaaliyopo.
kwa hiyo wewe unataka nani awe rais?
 
Membe ni mzuri kuliko Lowassa kwa mbali sana kama tunabisha tuifanye debate pale chuo kikuu kujadili mambo yote ya nchi uwekezaji wa madini, mafuta, ufisadi, uwezo wa kuongea na wawekezaji na ulinzi.

Hiyo itarudia historia ya debate ya Mrema(IQ sawa na Lowasa) na Mkapa(Membe).

Ikitokea,tegemea kusikia maneno ya kukariri kama yule mwingine alivyokariri Chavda...Chavda. Huyu yeye atakariri maneno ya elimu...elimu..elimu...ajira...ajira...ajira...bomu...bomu...

Lowasa alichowashinda wengine ni connection tu za magenge na mitandao ya wizi na uhalifu ambayo ipo nyuma yake,na imewekeza sana pesa ili ayalinde makundi haya ambayo yanajua kwa jinsi naye asivyo msafi atawapa deal za kuila hii nchi vizuri.

Otherwise kumlinganisha kiuwezo wa fikra na uzalendo Lowasa na Membe ni kumkosea heshima bure Membe.
 
Hatuhitaji mgombea urasi ambae jk akibadili miwani au sauti naye anabadili ili wafanane, akipunguza nywele nae kaiga, hatuhitaji mgombea ambaye maneno anayoongea hayatoki rohoni, mgombea ambae ana jukumu la mahusianoya kimataifa, badala ya kuyaboresha anaomba talaka na kutaka uadui na majirani, je angekuwa rais jumuiya ya afrika mashariki ingekuwepo leo? Hizo gharama zilizopotea angezitoleaje maelezo, hapo tu ameshindwa kuhimili, akipewa pakubwa si ataomba talaka kila mahali
Majungu hayo mkuu
 
Back
Top Bottom