Nahitaji Vifaa vya Ujenzi

Samahani kuna mtu ambaye anaweza kujua nondo za size 12 zitakuwa ngapi ktk tone moja? ili kuweza kukukisia labda nahitaji nondo 100 size 12 ninunue tone ngapi?

Mama Joe, kwa data nilizonazo zinaonyesha kuwa kwa nondo za kutoka nje (naambiwa kuwa ni za Pakistani) hizo za mm 12 zenye urefu wa futi 40 zimo 92 kwenye tani moja .
 
Asante dada Belinda. Hizo nondo ulishawahi kuzitumia na ukajua ubora wake? Maana naambiwa kuna nondo zingine zinazotengenezwa TZ zinavunjika kama kuni. Hivi kuna watu wanao-import nondo kutoka nje zenye ubora zaidi?

Mazingira, nilitumia hizo nondo tu kwenye ujenzi wa nyumba ambayo sasa wanaishi watu na ni ya ghorofa moja..nilikuwa na contractor na kwa utaalam wa kazi yake akasema zipo imara..huu ni mwaka wa nne sasa sijapatwa na sijaona dalili ya tatizo lolote...pia kuna sehemu nyingine inauza nondo unaingia ndani ndani ile njia ya ITV na Institute of Tax Administration..jina la hiyo kampuni imenitoka.
Swala la ujenzi ni zoezi zito..kuanzia mahitaji/vitu vya ujenzi na fundi/contractor pia uvumilivu unahitajika mana bajeti huwa haiendagi kama inavyopangwa..
 
Asante dada Belinda kwa taarifa hii. Hapo nilipoweka red. Kuna kiwanda kule cha kutengeneza nondo ila fundi mmoja kanionya kuwa hicho kiwanda cha Mikocheni nondo zake hazina ubora na ndo hizo zinazovunjika kama kuni. Akasema za Sita Steel na viwanda vingine zinafaa kwa kujengea nyumba gorofa moja na ikizidi hapo inabidi utumie za nje.
 
Wakati naanza ujenzi, hiyo ni sehemu mojawapo ya nondo nilipitia kuangalia na sikununua hapo..unajua tatizo lingine, uhalali wa taarifa tunazopewa ni ngumu sana kufanya maamuzi. Laa kwa vile ni fundi kakuambia na nia ni kukufanyia kazi yako vizuri uwe na nyumba imara hivyo mwambie akushauri vitu bora vya ujenzi..Kila la kheri kushinda site na kusimamia ujenzi!!
 
Asante dadangu. Yaani weee acha tu, ujenzi ni shughuli nzito, si mchezo ati. Na hii inachangiwa na kukosekana kwa uaminifu kwa mafundi wetu. Wizi uko nje nje, ukizubaa kidogo tu wanakuliza. Mama mmoja anasema yeye kwake walikuwa wanaiba hata zege lilichonganywa baada ya kuwabana sana na kushindwa kuiba simenti na vitu vingine. Lol!
 
Wakuu nahitaji supplier wa mchanga mzuri usio na vumbi kwa ajili ya ujenzi na mwenye bei nzuri. Kama wamfahamu mtu au wewe unafanya biashara hiyo ni PM.
 
Mama Joe, kwa data nilizonazo zinaonyesha kuwa kwa nondo za kutoka nje (naambiwa kuwa ni za Pakistani) hizo za mm 12 zenye urefu wa futi 40 zimo 92 kwenye tani moja .

Asante sana wote kwa michango yenu, nimeweza kuulizia kokoto nyeusi zinapatikana Kerai Construction hapa Mbezi Jogoo pia ingawa sijajua bei. Sasa swali langu ni kuhusu maji, nimekuta ukuta wa mdogoangu una ufa na ananiambia fundi kasema ni labda "malori ya maji yalikuwa yanaleta maji ya kisima ambayo huwa hayaendani na aina ya cement waliyotumia..."
Je maji ya kisima hayafai kujengea kabisa? na kama yanafaa kwa aina gani ya cement? Mie kwangu kuna slope kali kwa maana nipo mlimani hasa hivyo ninahitaji kuwa na basement au vyumba vya chini upande mmoja. Na sababu ya slope maji ya mchina hayapandi huku juu hivyo nilitaka nichimbe kisima changu (bore hole) kuanzia sasa kinisaidie na ujenzi pia kama yatafaa. naomba ushauri wenu.
 
Mama Joe ngoja tusubiri wataalamu wa mambo ya ujenzi waje watuambie kuhusu hilo la maji maana hata mimi natarajia kuanza ujenzi si muda mrefu. Hebu ulizia hizo kokoto nyeusi nami nijue bei yake. Ila inasemekana kuwa hata hizi nyeupe zipo ngumu zinazozofaa kujengea nyumba hadi yenye gorofa moja bila tatizo lolote.
 
Mazingira and co,
bei za Kerai walau ulinganishe na kwingine

Kerai Industries.jpg
 
Mazingira and co,
bei za Kerai walau ulinganishe na kwingine

View attachment 29832

Mama Joe mbona nasikia kuwa bei ya kokoto za Lugoba ni bei mbaya kuliko hizi za kwingineko lakini naona hawa Kerai wanauza za Dar sijuwi ni za Kunduchi au wapi kwa bei kubwa zaidi. Umefika wakakupa maelezo zaidi kuhusu hilo? Halafu bei zao za matofali naona ni kubwa sana.
 
Ndugu yangu nami nimeiweka hapa ili nijue kwingine kwenye nafuu, mwishoni mwaka jana matofali 6" ilikuwa 900tshs sasa nimeshangaa hii bei sijaielewa, nilimkuta dada sales office ambaye aliniambia eti ni pamoja na transport, kupandisha na kushusha ila umbali ukizidi unalipia kidogo. Alisema kujua bei kamili uwe unanunua na unataja umbali unakoenda kisha bei mnaelewana Ila leo naisoma vizuri karatasi nakutana na "Factory price without transport". bosi hakuwepo. Na mie nasubiria mvua matope yapungue kidogo nikaona kwanza nijue bei za kwingine, pili naweza uliza leo siku naenda dola imepanda bei ikawa nyingine. Naomba mwenye kujua wapi tofali nzuri bei nafuu zaidi atujuze, kokoto mradi uende na fundi zipo nzuri nyeupe kwa nafuu, ila tofali nzuri sijajua wapi.
 
Mama Joe nimeambiwa kuwa huko mitaani kuna watu pia wanaofyatua matofali kwa mashine na bei ina range kwenye tshs 1100 - 1400 transport inclusive within Dar. Kama una fundi tayari na ni mzoefu atakuwa anafahamu pa kuyapata ila kuwa makini maana mafundi hutangulia kwa wauzaji kwenda kuweka cha juu kabla hajakupeleka huko kununua. Kufanya window shopping mwenyewe ni mihumu pia.
 
Hapo kwenye nyekundu, nami niko kwenye harakati hizo za kufanya window shopping ya matofali mazuri na bei reasonable na kokoto pia. Nikipata taarifa zaidi nitawapa. Stay tuned. Kwa upande wa nondo tayari nimeshaamua nitanunua KAMAKA Hardware pale Tabata relinii kwa Warusi, ni waaminifu na bei zao ni nafuu mno. .
 
Back
Top Bottom