VIDEO: Waziri Muhongo atajwa kuvujisha ziara ya Waziri Mkuu kwa meseji

Kosa nikutoa maelekezo.....Kutoa maelekezo ya hovyo? Au kuifichua siri? sijaelewa mnisaidie wadau
Hajafanya vibaya huyo mama maana yeye alikuwa anajitetea upande wake,kuna mtu ameleta uzi hapa anakanusha kuwa muhongo hakutajwa
 
Kazi muhimu ya kukarabati iyo mitambo na kuitumia ilitakiwa maelekezo rasmi sio sms.
inaonesha mtumaji alipanic na kutaka kumwahi waziri mkuu. Yawezekana waziri aliulizwa kuhusu ilojambo ili waziri mkuu anapoenda asijegonganisha kauli na iliyowahi tolewa na waziri (kamaipo).
Hataivyo muhongo si malaika,amekosea but sio kosa la kuharibu so naona si busara eti ajiuzulu kwa hili but aonywe
 
Kuwachishwa uwaziri mkuu hatua ndogo hiyo?

Amma kwa hakika wewe shule ulienda kusomea ujinga.
Punguza Munkari sisi sio watu wa Matusi kama ungekuwa umesoma ata kuandika Kiswahili kinakushinda inaonyesha ni jinsi gani upeo wako ulipoishia ,mjinga anapenda kujifunza lakini mpumbavu yeye utoka mbele na kujikweza kama wewe.
 
Watu wanafiki nyie, sasa hiyo thread upya wake ni nini? video ndio hiyo hiyo iliyoonyeshwa ITV siku ya tukio, sasa kuna kilichoongezeka au ni wewe ndio hukusikiliza vizuri siku iliporushwa kwenye TV?

Hivi kama waziri ali respond taarifa iliyotolewa na Gazeti la Jamuhuri, na kuamua kuamrisha mita ziwashwe within 24hrs nayo kwenu ni hujuma?

Hata Raisi na Waziri mkuu wali respond kwa taarifa ya Gazeti, ambayo ilikuwa ya wazi....sasa ni siri gani iliyotolewa hapo, siri ya Gazet la Jamuhuri au ya Waziri kwenda kuangalia hizo mita?

Acheni kupika majungu Watanzania, ingawa ndio vipaji vyenu lakini sometimes mjishughulishe.
 
Sioni tatizo lolote kuhusu Mhongo kutoa amri kuwa within 24 Hours hizo meter zifanye kazi.

Mlitaka asitowe hayo maelekezo?
harafu hata mi sijaona uhusiano wa hii kauli na kuvujisha siri za waziri mkuu. nadhani katika utendaji wake tuu aliamua zianze kufanya kazi
 
Yaweza kuwa sawa kuwa sms sio utaratibu sahihi wa kuelekezana kazi serikalini lakini hili lisituzuie kutumia COMMON SENSE.

Hivi ingetokea Wairi mkuu au Raisi angemuhoji Muhongo kama alichukuliaje taarifa ya Gazeti la Jamuhuri kuhusu Mita...ni jibu lipi lingemfanya Waziri Mkuu au Raisi aone Prof aliwajibika?...Je Muhongo angesema nilisubiri nitakapopata muda ndio niende Bandarini kukagua na kutoa agizo kwa utaratibu rasmi au....nilituma ujumbe immediately kuamrisha mita zifanye kazi ili baadae nikipata nafasi nikalifanyie kazi?

Alafu mbona kama tunajitoa ufahamu, kana kwamba hao Wataalamu wa TRA, Bandarini, including Mama Mushi, sorry Mama Masawe,sorry Mama Chuwa, kuwa wao wana haki ya kuiba/kuhujumu na Waziri tu ndio anayepaswa kukamata/kuzuia.....nini wajibu wa Watanzania wengine?

Wataalamu wakificha taarifa Waziri atagundua vipi?

Najua mtakuja na hili swala kila kukicha coz kuna wanaosukuma na kufadhili ili wafarijike.
 
Punguza Munkari sisi sio watu wa Matusi kama ungekuwa umesoma ata kuandika Kiswahili kinakushinda inaonyesha ni jinsi gani upeo wako ulipoishia ,mjinga anapenda kujifunza lakini mpumbavu yeye utoka mbele na kujikweza kama wewe.

= hutoka

Unazidi kujihakikishia kuwa shule ulienda kusomea ujinga.
 
Ukifuatilia comment za watu hupati shida kuona ni kwa vipi hata yule Babu wa Loliondo aliwafungisha tela watu wazima na akili zao wakahamia Loliondo.

Na maoni yaliyokuwa yanaendelea wakati ule ndio kama hayahaya.....ile dawa inatibu....ile dawa lazima akupe yeye mwenyewe la sivyo huponi...Ile dawa inatibu magonjwa yote blah blah blah.

Alafu mzazi mjinga hivyo unatarajia kesho umuhimize mwanao asome ili akatafiti dawa za kutibu Malaria...aache kuua Albino na Vikongwe.
 
Back
Top Bottom