VIDEO - Wanaume Wenye Ukimwi Waoana Argentina

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
VIDEO - Wanaume Wenye Ukimwi Waoana Argentina
3829010.jpg

Alex na Jose wakibusiana baada ya kufunga ndoa Tuesday, December 29, 2009 6:37 PM
Wanaume wawili mashoga wa nchini Argentina ambao wote wana virusi vya ugonjwa wa hatari wa ukimwi wamefunga ndoa na kuwa mashoga wa kwanza kuoana katika nchi za Latin America. Alex Freyre mwenye umri wa miaka 39 na Jose Maria Di Bello mwenye umri wa miaka 41 wamekuwa watu wa kwanza kufunga ndoa za jinsia moja katika nchi za Latin America.

Alex alifunga ndoa na mpenzi wake Jose katika harusi iliyofanyika katika mji wa kusini mwa Argentina wa Ushuaia.

Mashoga hao ambao wote wana ugonjwa wa ukimwi awali walipanga kufunga ndoa yao desemba 1 ambayo ni siku ya ukimwi duniani lakini jaji wa mahakama moja nchini humo aliweka pingamizi la kufanyika kwa ndoa hiyo.

Jose na Alex walipata kibali cha kufunga ndoa ya jinsia moja mwezi novemba mwaka huu na kupewa ruhusa na mahakama kufunga ndoa katika mji mkuu wa nchi hiyo Buenos Aries.

Hata hivyo kutokana na sheria za Argentina ambazo zinaeleza wazi kuwa ndoa ni baina ya mwanaume na mwanamke, jaji mkuu wa jiji hilo alikitengua kibali hicho na kuipiga marufuku ndoa hiyo.

Mashoga hao ili wafanikishe azma yao ya kuoana walihamia katika mji mwingine wa Ushuaia katika jimbo la Tierra del Fuego ambako gavana wa jimbo hilo aliwapa ruhusa ya kufunga ndoa.

Alex na Jose walikula kiapo cha ndoa na kuvalishana pete za ndoa kabla ya kupeana mabusu mbele ya afisa wa serikali na waalikwa kibao waliohudhuria sherehe hiyo.

Mtetezi wa haki za mashoga na wasagaji wa Argentina, Claudio Morgado, ambaye alikuwepo kwenye harusi hiyo alielezea kufurahishwa na jitihada zilizofanywa na mashoga hao kuhakikisha wanafunga ndoa.

Alisema kuwa huo ndio mwanzo wa haki za mashoga na wasagaji kuanza kutambulika nchini humo.

Chini ni VIDEO ya harusi hiyo.


VIDEO - Wanaume Wenye Ukimwi Waoana Argentina
















http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3829010&&Cat=2
 
Back
Top Bottom