Video: Mtalimbo Umelala umelala doro

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=ewKsKe8XiRA[/ame]

Jamani nimeusikia wimbo wa Lady Jay Dee, wimbo huo unasema mtarimbo umelala doro.

Nimejaribu kufikiria nini maana ya wimbo huo?

Nikaangalia maudhui....dahhh nikafeli.

Naomba anayejua maana ya wimbo huo anisaidie kunielimisha.
 
Mmmm hata mimi ameniacha njia panda,ila mtalimbo c c c c na si ameolewa huyo mdada au mmmm sisemi
 
Mmmm hata mimi ameniacha njia panda,ila mtalimbo c c c c na si ameolewa huyo mdada au mmmm sisemi

Wewe ndio haueleweki! Kakuacha njia panda, afu tena kaolewa! Ina maana kuna kitu unakielewa hapo, tufafanulie basi!
 
sio wimbo wa lady jaydee, ni wa machozi band kijana aliyesimamia mzigo anaitwa mwinyi goa, kama kweli umeusikiliza lazima utakuwa umesikia maneno haya..''hukutosheka vya sahani, tumezungusha ungo''. Maudhui ni kumkanya mtu asiye rizika na vya kwake.
 
sio wimbo wa lady jaydee, ni wa machozi band kijana aliyesimamia mzigo anaitwa mwinyi goa, kama kweli umeusikiliza lazima utakuwa umesikia maneno haya..''hukutosheka vya sahani, tumezungusha ungo''. Maudhui ni kumkanya mtu asiye rizika na vya kwake.

Linapokuja suala la machozi band sina mashaka na wewe!
 
mtalimbo hamuujui? mtarimbo ukuilala doro si ndio kama vile ngoma ikinyopa?
hiyo ndiyo kazi ya fasihi........wengine waliumiza sana vichwa vyao kwenye wimbo wa mjomba.................
 
Hana lolote mjasiliamali tu yule, angekuwa anampenda kweli angempatia mwenzake kijimimba, lakini jamaa yupo kimaslahi zaidi.


MPWA KITOTO SI NDO KITAONGEZA MASLAHI AU???




Kwa nini jamani? na wewe upo deep sana.

Mpwa mi shallow kabisa!!! umeunyumbua wimbo utdhani ulishiriki kuandika!!
 
Huo wimbo ni wa zamani sana enzi za Beni Bati. Hizo zilikuwepo sana miaka ya 1960s na 1970s, nadhani wengi wa wana JF hamkuzikuta hizo. Zilikuwa ndiyo kama miduara ya sasa, zikiongozwa na beni (band) kusindikiza arusi n.k. Labda kama enzi hizi wanavyofanya matarumbeta. Arusi msururu wa magari ulikuwa ukisindikizwa na beni, au mdundiko, hasa Dar es Salaam sijui miji mingine. Nyimbo ziko nyingi lakini huo ulikuwa mmoja wapo uliokuwa maarufu sana enzi zile. Zingine kama 'Mwanionea mpenzi mwenyewe hayupo, mola akipenda mpenzi atamrudisha' pia zilikuwa maarufu sana kwa beni bati. Kahistoria karefu kidogo wana JF, Jay Dee na wana njenje na wengine wanazirudia tu hizo nyimbo.
 
aseee nimesikia hii track asubuhi klauzi efuemu, huu wimbo wapwa haujakaa sawa.
kuna kitu kimefichwa na tafsiri yake kwakweli sio nzuri
 
Mpwa mi shallow kabisa!!! umeunyumbua wimbo utdhani ulishiriki kuandika!!

Du sio siri wimbo huu unanikonga moyo, nasubiriaga ijumaa kwa hamu nikacheze mtarimbo doro na ukinikuta nyuma ya mijimama na seketula utanitaka.
 
Back
Top Bottom