Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,080
Maiti ya Gaddafi | Video mpya imetolewa ikionyesha kwa ukaribu zaidi jinsi mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi ukichezewa na kuburuzwa buruzwa ndani ya gari huku watu wakiupiga picha kwa simu zao. |
Baada ya kukamatwa na kuuliwa kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi mwezi oktoba mwaka jana, video nyingi zilitolewa zikimuonyesha akiwa hai kabla ya kuuliwa huku shati lake likiwa limejaa damu. Katika video hii mpya ambayo imeingizwa kwenye internet wiki hii na kuwa gumzo duniani, maiti ya Gaddafi ikiwa kifua wazi inaonyeshwa kwa ukaribu zaidi huku wanajeshi wa kundi la waasi wakiichezea na kupiga nayo picha. Haijajulikana ni kwa nini VIDEO hiyo imetolewa sasa lakini video hiyo imekuwa gumzo duniani kufuatia mwanaharakati Sami al-Hamwi kuweka linki kwenye Twitter akisema kuwa rais wa Syria Bashar Assad aiangalie video hiyo kwa ukaribu ili ajifunze yaliyomkuta dikteta mwenzake wa Libya. Gaddafi aliitawala Libya kwa miaka 42 kabla ya utawala wake kupinduliwa mwaka jana na yeye mwenyewe kuuliwa na maiti yake kuzikwa jangwani. Angalia VIDEO ya maiti ya Gaddafi chini. |
<tbody>
</tbody>
VIDEO Mpya ya Maiti Ya Gaddafi Ilivyochezewa
Last edited by a moderator: