Video: Laptop kwa kila mwanafunzi inawezekana!!! or ...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995

Serikali ina mpango wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi wa sekondari ana laptop na wana mpango wa kujenga barabara ya kwenda juu kwa juu. Cha kushangaza vitu vya msingi kama matanki ya kupigana na moto kwenye shule zetu hayapo na katika taifa linalotaka kuishi katika ulimwengu wa kisasa bado wanapigana na moto mkubwa kwa ndoo za maji! Hata mbinu za msingi za kupambana na moto hakuna anayejua huko kwenye mashule yetu na badala yake watu wanapiga "mayowe"!!!

My Take:
Tunataka vya mbinguni, vya duniani vimetushinda! Give me a f@#$ng Break! On othe hand, si Ikulu ilipokoswa koswa ilibidi private fire company ije kusaidia kuzima moto siyo..
 
Last edited by a moderator:
waanze kwanza na kuhakikisha kuwa wanafunzi wa primary hawana utapiamulo (data zinasema 34%), halafu waje kitabu kimoja kwa kila mwanafunzi wafuate dawati ndiyo wawaige Rwanda!
 
mwanafunzi anaekwenda shule na njaa, nguo zimechanika chanika, analazimishwa ende na godoro na ndoo yake hostel, ada ya shule hana uhakika nayo......................tunasema tutampa laptop yake YA KAZI GANI?

kweli msema pweke hakosi! manake viongozi wanasema tu watakacho japo hakina hata chembe ya mantiki
 
bweni la wasichana sekondari limeungua, na shule haikuwa na vifaa vya kuzimia moto zaidi ya watu kupiga mayowe.. na wanakijiji kutumia maji (ya kawaida) kuzima moto bila kujali chanzo cha moto huo ni nini! Hakuna Fire Code Tanzania?
 
Serikali ina mpango wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi wa sekondari ana laptop na wana mpango wa kujenga barabara ya kwenda juu kwa juu. Cha kushangaza vitu vya msingi kama matanki ya kupigana na moto kwenye shule zetu hayapo na katika taifa linalotaka kuishi katika ulimwengu wa kisasa bado wanapigana na moto mkubwa kwa ndoo za maji! Hata mbinu za msingi za kupambana na moto hakuna anayejua huko kwenye mashule yetu na badala yake watu wanapiga "mayowe"!!!

My Take:
Tunataka vya mbinguni, vya duniani vimetushinda! Give me a f@#$ng Break! On othe hand, si Ikulu ilipokoswa koswa ilibidi private fire company ije kusaidia kuzima moto siyo..

Mkuu nikurekebishe kwenye red hapo.
Serikali iliahidi kuwa kila Mwalimu awe na lap top na si kila mwanafunzi.
Nakumbuka Jk mwenyewe ndo alisema maneno hayo.
By the way naweza nisiwe sahihi kwani inawezekana walisema tena kuhusu wanafunzi ila sikusikia.
 
uko sawa; la kuwaidhi wanafunzi lilitangulia hilo la walimu.. so in short ni walimu na wanafunzi wote.. lakini sijasikia mpango wowote wa kuhakikisha kuna fire code inayozingatiwa na shule zote..
 
Back
Top Bottom