Video: Kova azungumzia sakata la Jerry Muro

Hivi jamani......kweli inakujia akilini mtu amakutwa na bastola iko full hana risiti alafu akaachiwa kweli kwa dhamana ya kujizamini mwenyewe???? labda hizo stori wapelekwe watoto wa chekechea hata mtua asie enda darasani hatawaelewa?????

a million dollar question... Yaani haingii akilini mtu ana pingu na bastola anaachiwa halafu mtu ana mkanda au gwanda anawekwa ndani wiki!!!

...UPELELEZI UNAENDELEA
 
Jerry alonga na watu....

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=eUB9B2XfxVw&feature=player_embedded[/ame]
 
a million dollar question... Yaani haingii akilini mtu ana pingu na bastola anaachiwa halafu mtu ana mkanda au gwanda anawekwa ndani wiki!!!

...UPELELEZI UNAENDELEA

Kesi hazifanani Janjaweed, every case has its merits depending on circumstances!
 
anaweza kuwa na umri mdogo, lakini akatenda kuliko mizee yenye umri wa baba yake, nani kakwambia uzee ndio utenda kazi, mbona tunamjadili huyu kijana, ujue ni ICON, kumbuka Biko alikufa akiwa na miaka 35 nakumbuka, lakini anaheshimika kule kwa madiba sambamba na kina Walter Sisulu, Oliver Tambo....

Babukijana nani alikwambia polisi wanakuacha bila upelelezi ukikamatwa na silaha isiyo na maelezo wala uhalali ikiwa imejaa risasi, hapohapo ukiwa na pingu.
hapo hujanielewa sizungumzii umri bali uwajibikaji wao kiutendaji na namna kesi zao zilivyo tofauti,hata hivyo nakuunga mkono hii kesi ni kizunguzungu

BK hivi kwa mtu kama JM anajijua fika yeye anawindwa kwa udi na uvumba kuhusu kuwalipuwa wala rushwa na madhambi mengineo kweli akurupuke tu akachukue rushwa ya 10 milioni kwa mtu alifukuzwa kazi na PM inakujia akilini kweli. JM anamlaka yapi ya kumrudisha mtu kazini alie fukuzwa kazi na PM. Huyo mhasibu alietimuliwa kazi kwani JM ndie alie sababisha ama ni uzembe wake kazini hadi ukafika kwa bosi wake PM akatimiliwa.
Hizi zote habari nakwambia ni ujanja wa kumnyamazisha JM asiendelee na mapambano yake ya kupinga rushwa.
JM kama upo jamvini usife moyo wala usikate tamaa mapambano bado yanaendelea wembe ni uleule
hapo ndipo namimi nazidi kushangaa zaidi,sasa nnachojiuliza hivi kweli mtu kama jerry muro aliejitoa muhanga kufatilia wale matrafiki waziwazi bila kificho,leo hii akabambikiwa bastola na pingu ndani ya gari yake,na kesi ya UONGO KAMA KAMDAI yule afisa bagamoyo hongo nayeye wala hamjui na hana taarifa yoyote????halafu jamaa akamsingizia kama aliacha hata miwani ndani ya gari ya muro,na muro mwenyewe akajua ni uongo then akanyamaza tu?jamani hata mtu uwe mwoga vipi kuna kikomo,ina maana muro kapakaziwa mambo yooote hayo na akakaa kimya tu?tuwe na mapenzi na watu lakini tusipitilize wakikosea tuwakosoe sio tuwatetee tu.
 
Nimeangalia video ya JM, maelezo yake yanaacha mianya mingi ya kumbana kisheria. Kama alivyoshauriwa na wengi JM atulie, aache kutoa maelezo maana baadae yanaweza kutumika against him... Anahitaji mwanasheria kuzungumza na vyombo vya habari (kama ni lazima) na kufuatilia suala zima.


Annina
 
Nimeangalia video ya JM, maelezo yake yanaacha mianya mingi ya kumbana kisheria. Kama alivyoshauriwa na wengi JM atulie, aache kutoa maelezo maana baadae yanaweza kutumika against him... Anahitaji mwanasheria kuzungumza na vyombo vya habari (kama ni lazima) na kufuatilia suala zima.


Annina

kwa kweli Jerry needs some guidance on this!!!
 
wajameni... Bastola anamiliki kihalali kabisa. Mimi hilo nalijua. Lakini pingu ndio litu ambacho sielewi.

Mkuu unajuaje hiyo wanayodai kumkuta nayo ndiyo hiyo unayojua anamiliki kihalali?

Mh! watakuwa wamembambikiza tuuuu!
Lol!
 
kwa kweli Jerry needs some guidance on this!!!

Jerry anajua anachokifanya refer to his statement. "Aulize nimevitoa wapi, Kova is a very minor person, siyo jeshi la polisi yule na vitu siyo vya leo nina mwaka nao wa nne"

Statement hii ina ujumbe mkubwa sana kuhusu umiliki wa Jerry wa hivi vitu. Sema tu kwamba akibwabwaja sana atajikuta anavunja miiko ya kazi yake
 
Jerry anajua anachokifanya refer to his statement. "Aulize nimevitoa wapi, Kova is a very minor person, siyo jeshi la polisi yule na vitu siyo vya leo nina mwaka nao wa nne"

Statement hii ina ujumbe mkubwa sana kuhusu umiliki wa Jerry wa hivi vitu. Sema tu kwamba akibwabwaja sana atajikuta anavunja miiko ya kazi yake


Nimeliona hili, ndio maana nikasema atulie kama alivyoshauriwa na wengi...unless ni maelekezo toka kwa AC...



Annina
 
Jerry Muro amezungumza live kwenye kipindi cha Usiku wa Habari live on TBC, usiku huu. Nimemsikiliza Jerry kwa makini na kumsoma in between the line, anasema ukweli kwa asilimia 100% kuwa hajapokea rushwa yoyote!. That is a fact!.

Pamoja na ukweli huu, bado Jerry anaacha maswali mengi bila majibu, haswa inconsistance kwenye kila anapoongea, hayo yatakuja mtundika msalabani ajikute akisulubiwa bure bila hatia, haswa anaposema hamjui kabisa huyo jamaa ndio na yeye alishangaa kumuona pale, jamaa alisharipoti kwenye gari ya Jerry kuna bastola na pingu, na yeye alisahau miwani yake nyeusi, hivyo vyote vimekutwa ndani ya gari, it ncan be just a coincidence, in fact its amaizing coincidence!.

Kwa vile Jerry ni mpiganaji na lengo ni kumsaidia, ushauri wangu muhimu kwa Jerry, "Don't talk too much, utalikoroga"!. Kamanda Kova na vijana wake, tayari wameshalikoroga, cha muhimu ni Jerry kunyamaza na kuwaachia hiyo kamba, wajinyonge wenyewe.
 
Najua kuhusu hilo lakini sikiliza maelezo kova aliyotoa hivyo vitu kakutwa navyo na kakiri ni vyake,sio kilakitu unangangania polisi kubambikia sikiliza tena kova anasema nini sio unakurupuka tu.na maelezo ya jamaa alieombwa rushwa nikwamba Jerry alimtisha na bastola na pingu.

Jerry mwandishi wa habari pingu na bastola vyanini, pingu haziuzwi popote bongo bastola sawa waweza sema ulinzi wake haya risiti hana na imekutwa loaded.

Jamani kwani uhalali wa mtu kumiliki bastola ni kuwa na risiti? Naomba nieleweshwe hapa!!!

Tiba
 
Jerry atawageuka,hawana njia,wamelikoroga na sasa itabidi walinywe.
 
Ukiwa unamiliki bastola huwa unatakiwa kutembea na copy za vibali kuthibitisha kuwa huyo sila ni yako kihalali mtu yeyeote anayetembea na bastola muda wote hivyo vitu huwa anakuwa navyo kwenye gari lake na hata wakati wa kununua hiyo bastola wanakwmbia kabisa toa copy halafu wanaithibitisha maana huwezi tembea na document orignal muda wote kuna kupoteza ama zikachaa

Mkuu una uhakika na ulichokisema kwamba ukiwa unamiliki bastola lazima pia utembee na copy za document? Kuna sababu gani za msingi kutembea na docs? Unafikiri askari makini akikukamata na bastola atakubali umuonyeshe copy za kibali kuimiliki hiyo silaha halafu akuachie? Hebu fikiria mara mbili!!!!!

Tiba
 
Swali langu ni kuwa pingu alikuwa anazitumia kwa ajili gani?

Ingawa hata kamba ni pingu..hizo ni pingu za chuma tu na sidhani kama kuna kosa kumiliki pingu. Ila alikuwa nazo za nini?

say kwa ajili ya mambo ya mapenzi na mwandani wake akirudi nyumbani; kwani ni kosa hilo? Hata miye ninazo za rangirangi..
 
Mimi nina mashaka sana na Muro. Lazima kuna issue. Tusubiri na tutaongea hapa hapa JF

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema lilimshikilia na kumhoji mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro, baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwananchi aliyelalamika kwamba kuna matapeli wamekuwa wakimtisha wakimdai rushwa.

Aidha, limesema halina tatizo lolote na mwandishi huyo kama taarifa zilivyovuma na badala yake linafanya kazi kulingana na sheria na taratibu zake.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari na kumtaja mwananchi huyo kuwa ni Michael Wage, ambaye alikuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kabla ya kuvuliwa wadhifa huo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na ubadhirifu wa fedha.

Alisema Wage alifika katika kituo Kikuu cha Polisi juzi saa 5 asubuhi na kulitaarifu Jeshi hilo, kwamba kuna watu watatu ambao wanajifanya maofisa wa Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waandishi wa habari na wanajeshi huku wakitoa vitisho wakitaka wapewe Sh milioni kumi.

Alisema mwananchi huyo alilalamika kwamba watu hao wamekuwa wakimwandama na kumsumbua tangu Januari 28 mwaka huu, wakidai kwamba yeye ni fisadi na ana majumba mengi ya kifahari Morogoro, hivyo walitaka wapewe hongo hiyo ili wasimkamate.

Aidha, Kova alisema mwananchi huyo alidai kwamba watu hao ambao walikuwa na pingu, wamekuwa wakimwambia kwamba asipotoa fedha hizo watamchukulia hatua na kumtangaza katika jamii kwa ufisadi.

“Wage alipokuja kwetu, alisema hatoi fedha na anataka watuhumiwa hao wakamatwe na wakawekeana miadi ya kukutana saa 6 mchana katika hoteli ya City Garden katikati ya Jiji kwa makubaliano kwamba watapeana fedha hizo katika eneo hilo ... polisi walifikiri ni matapeli na tukaenda muda huo,” alisema.

Alisema baada ya kufika katika eneo hilo, lengo likiwa ni kuwakamata matapeli hao, gari namba T 545 BEH aina ya Toyota Cresta, liliingia lakini mwenyewe alikataa kushuka na kumtaka Wage alifuate gari hilo.

“Polisi wangu walipoona gari limekuja na watuhumiwa kukataa kushuka, walilifuata na walipofika walishangaa kumwona Jerry Muro na baada ya Wage kusema huyu ndiye ambaye amekuwa akimsumbua sana, polisi ilibidi wamchukue mpaka kituoni ili kupata maelezo mazuri,” alisema.

Kova alisema mlalamikaji huyo alikuwa akidai kwamba anamfahamu Jerry na amekuwa akimsumbua hata kumfuata nyumbani kwake na kukubaliana wakutane jijini Januari 29 mwaka huu na kutoa vithibitisho mbalimbali kwamba anamfahamu ikiwa ni pamoja na miwani yake aliyokuwa ameiacha ndani ya gari lake.

“Wage aliileza Polisi vithibitisho vilivyopatikana katika gari la Jerry ikiwamo miwani yake aliyoisahau, pia alieleza kwamba Jerry anatembea na bastola na pingu na vyote tulivipata katika gari lake na kumhoji ambapo alikiri kuvimiliki,” alisema.

Alisema pingu zilipatikana kwenye ‘dash board’ huku silaha ikiwa kiunoni na katika uchunguzi wa awali wa maeneo yaliyohusishwa na tukio hilo na uhusiano baina ya watu hao, polisi ilifanya upelelezi na kupata uthibitisho kupitia CCTV.

“Pia napenda mfahamu hakuna suala la Jeshi la Polisi na Muro, isipokuwa kuna mlalamikaji na Polisi na hata kama angekuwa ni askari ametenda kosa kama hilo, angechukuliwa hatua za kisheria … Jeshi la Polisi Kanda Maalum hatuna ugomvi na Muro na ni rafiki yetu sana,” alisema.

Alikiri kutambua umiliki halali wa Muro wa bastola CZ97B namba A6466 na kwa upande wa pingu, Kova alisema ni kinyume cha sheria kutokana na kwamba pingu humilikiwa na Polisi au Magereza pekee.

Pia Kamanda alisema Jeshi hilo limemtaka Muro, kuwasilisha risiti ya pingu hiyo, kutokana na kwamba hakuna sehemu yoyote inapouzwa na sheria haimruhusu mtu yeyote kumiliki labda kampuni na ni kwa kibali maalumu.

“Silaha kama hii ukimwonesha mtu ni lazima ashtuke … hivi hata kama wewe ni mwandishi wa habari za uchunguzi, pingu zinahusiana vipi na utafutaji habari? Hii pingu ukimwonesha mtu tena aliyeumwa na nyoka kama Wage lazima ashtuke,” alisema.

Hata hivyo Kova alisema kuwa kesi hiyo haitaenda mahakamani mpaka ipitie kwa wakili wa serikali na kueleza kwamba Jerry yupo nje kwa dhamana na kuwataka watuhumiwa wengine wawili wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo wajisalimishe.

Muro ameibuka kuwa mtangazaji mahiri kwa mwaka 2009 na kujinyakulia tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka kupitia vipindi vyake vya Televisheni vya Usiku wa Habari vinavyorushwa katika kituo cha TBC1 na kabla ya kuhamia kituo hicho alikuwa akiendesha kipindi kama hicho katika ITV.

Miongoni mwa mambo aliyokuwa akirusha katika vipindi hivyo ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na ukiukwaji wa sheria na polisi wamekuwa walengwa wakuu wa vipindi hivyo.

Wakati huo huo, Simon Nyalobi anaripoti kuwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) limelitaka Jeshi la Polisi nchini kufanya uchunguzi haraka na kumfikisha mahakamani Muro ili haki iweze kutendeka.

Akizungumzia suala la kukamatwa kwa Muro, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema hatua iliyochukuliwa na Polisi dhidi ya Muro yawezekana zikawa ni njama za kumtisha asiendelee na uchunguzi wake wa tuhuma kubwa kubwa.

“Muro ana kashfa zingine kubwa anazifuatilia zinazowahusu vigogo wa Serikali, yawezekana hii ni mbinu ya kutaka kumdhoofisha asiendelee na uchunguzi wake … lakini kama ni kweli aliomba rushwa, basi atakuwa ameidhalilisha taaluma ya habari,” alisema Mukajanga alipozungumza na waandishi wa habari jana.

Hata hivyo, alisema Muro asitumiwe kama kondoo wa kafara na kuwaasa waandishi wa habari kuwa makini katika kazi zao wakati huu hususan mwaka huu wa uchaguzi kwani lolote linaweza kuwatokea.
 
Jerry anajua anachokifanya refer to his statement. "Aulize nimevitoa wapi, Kova is a very minor person, siyo jeshi la polisi yule na vitu siyo vya leo nina mwaka nao wa nne"

Statement hii ina ujumbe mkubwa sana kuhusu umiliki wa Jerry wa hivi vitu. Sema tu kwamba akibwabwaja sana atajikuta anavunja miiko ya kazi yake

Kwa hiyo mkuu unataka kusema Jerry naye ni ..oka?
 
Back
Top Bottom