VIDEO: CCM wananitishia maisha - Rev. Munishi

Status
Not open for further replies.
munishi ni raia wa tz hvyo anahaki ya kukosoa nchi na serikal yake...tatzo tz ukikosoa serikal lazma upewe kes.ccm muda wenu wa kukaa madarak umeisha 2mechoka jaman...God blec TZ.
 
Hiyo ndio bongo kaka... Ukiongea kwa uhuru utaishia matatizoni.. Jamaa anavyoongea unaweza kudhani kachanganyikiwa...

Lakini Kama unafahamu issue za kina Marehemu Prof Kighoma Ali Malima, Imran Kombe wengine wengi tu basi utaelewa kwanini huyu mtu anapiga kelele. Mnakumbuka yaliyompata Dr Masumbuko lamwai?.. Tanzania uhuru wa kuzungumza ni mdogo..

Munisi uwa yuko free kuongea kila kitu, lkn TZ mambo hayako hivyo. Tusiwe biased na kulichukulia kama suala hili la kidini. Mimi ni muislam lkn hapa sioni sababu ya kupinga kwa kuwa munisi ni christian. Tanzania kila kitu kinawezekana freedom of speech hakuna.

Regards

:twitch::A S 20:MKUU NINI KILIMPATA DR.LAMWAI?NIMEKUWA NAJIULIZA MIAKA MINGI SIPATI JIBU.NASHANGAA NA UKIMYA WAKE.ALIKUWA MZALENDO WA UKWELI NA WATANZANIA WALIMKUBALI.NILIWAHI KUMSIKIA AKISEMA USALAMA WA TAIFA NDIO UNAUA UPINZANI.TUJUZE,NINI KILIMPATA.??????:A S 20: :twitch:
 
maoni ya mhariri mkapa unatuaibishakwamba polisi nchini tanzania wameanzisha zoezi la kukamata kanda za dini, hizo ni habari mbaya tena za kusikitisha. Inasikitisha zaidi kuona kuwa zoezi hilo linafanywa wakati huu wa uchaguzi mkuu. Hakuna sababu wanayoweza kuitoa kuhalalisha zoezi hilo ambalo vyombo vya habari vimeubandika jina la 'operesheni waogopeshe waache kusema. Sisi katika gazeti la injili tunalaani kitendo hicho kwa nguvu zote. Pamoja kuwa walioadhiriwa ni wasanii wa nyimbo za injili na hasa msanii maarufu faustin munishi, sisi tunaliona hilo kama pigo kubwa kwa vyombo vyote vya habari. Nani ajuae kesho itakuwa zamu ya nani? Lakini jambo moja ambalo waliohusika ilitakiwa walijue ni kwamba, siku hizi ni vigumu kuzuia information isiwafikie watu. Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknologia, na njia za mawasiliano zimekuwa nyingi ukilinganisha na wakati wa nyerere. Watu walilazimishwa kuisikliza redio tanzania, na kusoma magazeti ya uhuru na mzalendo. Yalitumiwa na chama tawala kuelezea sera zao za ujamaa na kujitegemea, ambazo zilishindwa kabisa na kuiacha tanzania ikiwa moja ya nchi masikini duniani. Lakini pamoja na kuwa tanzania sasa ina utitiri wa vyombo vya habari, huwezi kueleza tofauti, waandishi karibu wote ni wale wale waliotoka redio tanzania na magazeti yaliyokuwa yakijulikana kama magazeti ya chama na serikali, na ukiritimba wa chama kimoja bado haujawatoka. Tuna wingi wa vyombo, lakini ujumbe ni mmoja. Ni mpaka tuwe na waandishi wa kizazi kipya ambacho hakijapitishwa jeshini kupigwa msasa wa siasa ya ujamaa, ndipo tunapoweza kusema kuwa tuna uhuru wa vyombo vya habari. Ndiyo maana mageuzi ya kweli tanzania yatachukua muda kwani wengi wa wasomi tulio nao ni wale wliokuwa hawafikiri. Nyerere akifikiri kwa ajili yao. Na hata kama walifikiri mzee 'haambiliki' asingewaruhusu kutoa mawazo yao hadharani. Yale tunayotaka kusema hapa ni kwamba, kama kweli tunataka mageuzi ya kweli, lazima tuache kabisa kuwategemea wale waliokuwa viongozi wakati wa nyerere, kwani wanasema 'mbwa mzee hawezi kujifunza mbinu mpya.' wanatumia mbinu zilizopitwa na wakati, badala kuinyamazisha hiyo kanda inayodaiwa kuwa ya uchochezi kwa kusema sera za nyerere za ujamaa zilishindwa kabisa, sasa wameifanya kanda hiyo kuwa maarufu kuliko ilivyokuwa mwanzo. Sasa kila mtu anatamani kuinunua na kuisikiliza. Ccm inaendesha shughuli zake kwa mtindo wa zamani wa kikomunisti ambao umepitwa na wakati. Ni mtindo huo ndio unaowafanya watanzania waonekane kuwa walikuwa wakimpenda nyerere, na kumbe ukweli wa mambo walikuwa wanamuogopa. Wangempendaje mtu aliyewafanyia majaribio ya siasa ya ujamaa ikashindwa na kuwaacha wakiteseka? Ni ukweli usiopingika kwamba, hata viongozi ndani ya chama tawala walikuwa hawampendi julius, bali walimwogopa. Nyerere aliwafanya watu wote kuwa wapelelezi. Baba anampeleleza mtoto, na mke anampeleleza mumewe. Na kwenye nchi ambayo kila mtu alikuwa na kazi kumpeleleza mwenzake, hofu ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini ndiyo iliyokuwa inatawala na siyo heshima wala upendo. Tunasikitika kusema kwamba mwaka mmoja baada ya yule waliyemwogopa kufa, bado mkapa anataka watanzania wamwogope. Lakini watamwogopea nini wakati dola haimwogopi? Injili
siasa za ujamaa na kujitegemea zilikuwa siasa za majaribio.watanzania wanajua hili?ziliua uchumi na wasomi wa tanzania wakaacha kufikiri na kuwa na woga uliopitiliza.wasomi fungukeni sasa.acheni woga!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!magamba bana?????.we acha tu.
 
kauli yake sikuipenda,ni mchochezi tu.kwani anayemuita shetani ni nani hapo: anaweza pata kesi labda kama anatafuta umaarufu
 
unaongelea mambo ya mwaka gani? Munishi ni mlokole wa miaka mingi, nakumbuka mwaka 1982 alikuja mwanza akiwa na moses kulola kuchapa injili. Alikuwa akitumia accordian ndogo sana na iliyochakaa. Mzee mmoja anaitwa gombanila akaahidi kumnunulia accordian kubwa ambayo akaitumia kwa muda mrefu.

alikuwa jambazi lini??????miaka ya 70 nilimwona luninga ya kenya nairobi na accordian yake akiimba solo nyimbo za injili.alikuwa anaimba usiku kila siku wakati wa kufunga vipindi.alikuwa kijana mdogo sana na sauti nzuri ya kuvuia.ujambazi alifanya lini???
 
CCM acheni kuchokoza kile ambacho kitawathiri hata maisha yenu pia, kama hamtaki kutenda haki wananchi tutakapo amua mtashangaa.
 
Naomba unikome! Huo ulikuwa ni mtazamo wangu na sio mtazamo wa 'watanzania', ukome!

You Deserve What you have been Told! Hata yeye huo ulikuwa ntazamo wake. Wanaofatwa fatwa na kuhukumiwa na sisiemu behind the scene tene injustic wapo wengi, but huyu ni mfano wa kuigwa kwa ujasiri wa hali ya juu anao uonesha. You Asked for A Ban? Dont mind
 
Nimefwatilia video hii, nimegundua ilipostiwa youtube in early 2010, so tusiichukulie kama ni kitu kipya hapa jamvini.....!!! na huyu jamaa hayupo nchini tena
 
MKIAMBIWA WANAO NGOA KUCHA NI CCM NA VYOMBO VYA USALAMA MNA BISHA HAYA SASA USHAIDI UKO WAZI,JK MR fastjet unamiaka michache sana uludi uraiani wewe fanya mambo kwa kadiri kichwa chako kinavyo kutuma ipo ICC
 
Haya ni maneno ya Mchungaji
Munishi kama yanavyosikika katika
Video yake.

Kwa wale ambao mmekuwa
mkitembelea internet, mmeniona
katika Facebook nikilalamika kuhusu
yale ambayo CCM wananitendea
ninaona si haki Wananitishia Maisha
yangu kwanini!?

Just to say that CCM
imepitwa na wakati mnataka
kuninyang'anya uhai kwasababu hiyo
tu kusema CCM imezeeka, itoke
Madarakani, mnataka kuninyang'anya
uhai mnataka kuiharibu jamii yangu
kwasababu hiyo tu, kwanini?!

Ni haki
yangu kusema haya, ya Kikatiba
Mungu amenipa Pumzi nizungumze
na nchi ya Tanzania ni nchi ya vyama
vingi na kama ni nchi ya vyama vingi
lazima kuruhusu mawazo tofauti na
mimi nina mawazo tofauti na CCM,
CCM ni chama cha Majambazi,
Kimezeeka kitoke madarakani, mimi
nina mawazo tofauti, ruhusu mawazo
tofauti, watu wazungumze vitu
tofauti, kwanini mnalazimishia
mawazo?!

Kwamba mtu akiikataa CCM
mnamfuata, mnamtumia Majasusi,
mnamtumia kikosi cha Usalama wa
Taifa wamfuate kila anakokwenda
kwani amefanya kosa gani?! mimi
nimefanya kosa gani?!

Kusema CCM
imezeeka nimefanya kosa gani?! Na
kama kuna kosa mbona msinipeleke
mahakamani nihukumiwe kama ni
kosa la kustahili kufa niuwawe
kwasababu hiyo, mbona mnanitishia
maisha, kutuma watangamize jamii
yangu, kuwashawishi na pesa,
kuwasafirisha, kutumia mashemeji
zangu huko Arusha kuharibu jamii
yangu kwanini?!

CCM kwanini nasema
kwanini?! Kikwete unanisikiliza mahali
ulipo kwanini, mbona utume watu
waharibu jamii za watu kwanini
Kikwete we Kikwete?!

CCM ni yako
katika jina la yesu nakumbia Kikwete
uondoe wale wote wanaonitafuta, na
mimi sina kitu cha mtu nilichomuibia
hakuna nasema CCM ni mbaya peke
yake hilo, kwahiyo wacha kutuma
maaskari vikosi vya kunifuata mimi
sitaki, wacha kutuma katika jina la
Yesu mtumishi wa Mungu
ninakuambia hayo Mungu huyu
ninayemtumikia katika jina la Yesu
nakuamuru ondoa vikosi vyako
vinavyonifuata, ondoa watu wako
wanaotaka kuharibu jamii katika jina
la Yesu umeshindwa Shetani, Pepo la
CCM limeshindwa katika jina la Yesu.
Amen

Mchungaji Munishi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom