Video:Askari abambwa live akipokea rushwa!!

Hiyo ndiyo bongo yetu hatuendi bila ya Rushwa, Rushwa imeenea kila sehemu Mahospitalini,maofisini,Mahakamani,viwanja vya ndege sijuwi hili tatizo Mheshimiwa Rais wetu JK atalimaliza lini? Wahusika wa hilo tatizo sugu au gonjwa sugu wanajuwa lakini wanalipuuza sasa tutafika safari yetu ndefu ya Maendeleo?
 
Mr Gambler umenifurahisha sana kutuwekea video nzuri, sasa hivi maaskari wetu wanaumbuka, na wao kweli wamezidi kutunyanyasa na kutubambikia kesi za uwongo
 
Mkubwa wa hili jeshi yuko wapi kuchukua hatua ?hii kali sana dah ! bongo kazi ipo mpaka kufikia maendeleo
 
na wale pale maaskari wa salender bridge wamezidi kwa rushwa, wamekaa kama mafisi, nitafurahi sana kama watanaswa katika video
 
Wakubwa wanakula rushwa nene nene wadogo wanakula rushwa ndogo ndogo
hahahahaha...akale wapi huyo koplo? mwacheni tu...nasikia hiyo ilikuwa ni hela ya mafuta ya gari (defender la polisi)
 
huyo askari si atakuwa na cheo kikubwa! hizo alama za v zinamaanisha ana cheo gani?
 
mmechemka?? hakuna anayejua hiki ni kituo cha wapi?

kila mtu hula katika madhabahu yake! mnataka watoto wenu tu wasome academy, wake je? Polisi wamechoka kusindikiza mafisadi ilihali kesi za mafisadi hazitatuliki.

Nani miongoni mwenu anaishi bila kuchomoa mtu hasa ninyi mnaomtumikia kaisari?

Hivi hiki ni kituo cha polisi au ni kile kichemba cha mahakama iliyopo kule kindondoni karibu na Tumaini university. Maana huko ndiyo centre ya dili kama hizo, hata ukipiga mtu au ukamgonga na gari mpaka akazimia au kufa, kwa elfu tano tu unaachiwa huru!!!
 
Kula ni kula mpwa,vibaya kukomba mboga. Sikukuu ziko jirani na mwanzo wa mwaka ada shuleni zinatakiwa. Mwacheni akusanye vijisenti jamani...
 
Back
Top Bottom