Vichwa Vya Nguruwe Vatundikwa Msikitini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
6553274.jpg

Damu ya nguruwe kwenye sakafu ya eneo la msikiti
Thursday, August 02, 2012 5:50 AM
Wakati waislamu wakiendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani, waislamu nchini Ufaransa wameelezea kusikitishwa na vichwa viwili vya nguruwe vilivyotundikwa kwenye geti la kuingia msikitini huku damu ya nguruwe ikitawanywa kwenye sakafu.
Umoja wa wanafunzi wa Kiyahudi nchini Ufaransa wameungana na jumuiya ya kiislamu nchini Ufaransa kulaani kitendo cha vichwa viwili vya nguruwe kutundikwa kwenye geti la kuingilia msikitini.

Tukio hilo limetokea kwenye mji wa Montauban ambako mwezi machi mwaka huu mwanaume aliyejitangaza kuwa yeye ni gaidi wa Al-Qaeda, Mohamed Merah aliwaua wanajeshi wawili wa Ufaransa.

Vichwa viwili vya nguruwe vilining'inizwa kwenye geti la kuingilia msikitini huku kiasi kikubwa cha damu ya nguruwe kilimwagwa kwenye sakafu ya kuingia msikitini.

Waislamu walioenda msikitini kusali sala ya alfajiri jana jumatano walikumbana na vichwa hivyo vya nguruwe vikiwa tayari vimeishatundikwa kwenye geti la kuingia msikitini.

Rais wa msikiti huo uliopo kwenye kitongoji cha Tarn-et-Garonne, Hajii Mohamed alilaani tukio hilo akisema haamini kama mtu mwenye akili zake anaweza akafanya kitendo cha kuishambulia dini ya kiislamu tena katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

"Tukio kama hili kutokea ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kusema kweli halielezeki, ni tukio la kueneza chuki", aliongeza.

Umoja wa wanafunzi wa Kiyahudi nchini Ufaransa nao umeungana na waislamu kulaani tukio hilo.

Ufaransa ndio nchi yenye waislamu wengi kuliko zote barani Ulaya ikiwa na jumla ya waislamu zaidi ya milioni 4.

<tbody>
</tbody>

6553274.jpg




Vichwa Vya Nguruwe Vatundikwa Msikitini
 
Duh, its too bad! matendo mengine bwana, si bora angeenda kumtafuta huyo aliyejiita al-qaed kuliiko kuwaharibia wenzke swaumu. Anyway, labda kuna kitu nyuma ya pazia.
 
Nina laani kitendo hicho walichofanyiwa waislaam wa Ufaransa, pia nina laani kitendo cha SMZ kuzuia waumini wa ndini zingine kutokuonekana wanakula katika mitaa ya Zanzibar na Pemba katika kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani
 
Bora kutundika vichwa kuliko kujilipua na kuua watu kule Nigeria. Kichwa kimetundikwa tu kwenye geti hakijamgusa mtu ila wao wanajilipua wanaua watu wasiohusika. Madhara pekee yanayoonekana hapo ni kulazimishwa kuona nguruwe tena msikitini wakati wako kwenye mfungo na kusababisha wale walafi watamani kula ilihali muda bado
 
wanajaribu kupinga dini ya haki ila daima watashindwa na dini inaendelea kukua tena hukohuko Ulaya.
 
Back
Top Bottom