Vichaa kuandamana hadi magogoni kupinga kuingiliwa kazini

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,176
305
Jumuiya ya Vichaa Tanzania (JUVITA) imetishia kuitisha maandamano ya vichaa nchi nzima kupinga kazi yao ya kuokota makopo kuingiliwa na watu wenye akili timamu. Tukio hili limejitokeza baada ya mamia ya makundi ya watu wenye akili timamu kuanza kuokota chupa za maji safi pamoja na makorokoro mengine na kwenda kuyauza ili kujipatia chochote kitu.

JUVITA wanaamini watu hao (waokota makopo) wamenukuu vibaya kauli ya mkazi wa magogoni aliposema kuwa atatoa ajira milioni moja kila mwaka, hivyo wamedhamiria kuandamana hadi magogoni ili kumuomba mkazi huyo kuitolea ufafanuzi kauli yake na hivyo kuinusuru kazi yao ya kuokota makopo kwani bila ya kuokota makopo ukichaa wao utapoteza maana.
 
Nawashauri bora wasiende tu maana wataishia kupigwa mabomu tu, hawajui kuwa hii ilikuwa moja ya ajira milioni moja alizotangaza mkulu
 
JUVITA itakuwa ni chama kinachoongozwa na wana damu ya kichadema chadema cuz CDM ndio wapenda maandamano na wapenda kususa susa!
 
akh chadema tena?!!!! ngoja nirudi zangu jukwaa la sports
 
Back
Top Bottom