Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,139
Tuhuma za wafanyakazi ATCL zifanyiwe kazi haraka
Najivunia kuwa Mtanzania, naipenda nchi yangu, wakati wowote nipo tayari kuitetea sifa ya nchi hii na kamwe sitamuonea haya ye yote aliye kikwazo cha maendeleo ya Tanzania aidha kwa kufahamu au kutofahamu, kwa kutumiwa au kwa maslahi yake binafsi.
Ni kutokana na mtazamo huo, nadiriki kusema kwamba yanayotokea sasa katika Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) yanasikitisha na ni aibu, hivyo serikali inapaswa kuchukua hatua haraka ikiwa ni pamoja na kuzifanyia kazi tuhuma za wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Kauli za wafanyakazi hao zimenifurahisha, si kwamba nimethibitisha kuwa ni za kweli, ni kwa sababu wamesema wanachoamini, wameeleza hisia zao na kutoa msimamo, nashawishika kuamini kuwa waliyasema hayo kwa kuongozwa na uzalendo na si chuki binafsi, aidha kwa Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, David Mattaka au viongozi wengine.
Naamini kuwa serikali imeelewa, tatizo ATCL si upungufu wa ndege au ukosefu wa fedha tu, wafanyakazi hawana imani na utawala ulio chini ya Mattaka na Bodi ya Wakurugenzi inayoongozwa na Balozi Mustafa Nyanganyi.
Kuna mambo ya msingi yanayostahili kufanyiwa kazi haraka, hayahitaji uchunguzi au utafiti, hayahitaji mwongozo wa sera au fedha za kigeni, mfano, kurudisha uhusiano mzuri kati ya menejimenti na wafanyakazi.
Hata kama ATCL itakidhi masharti ya usalama, hata kama ndege zake zote zitakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa asilimia 100, ni ndoto kwa kampuni hiyo kupata mafanikio kama hakuna uhusiano mzuri kati ya utawala na wafanyakazi.
Sina mamlaka ya kusema tuhuma za wafanyakazi wa ATCL ni za kweli au la, lakini nina wajibu wa kuiomba serikali isizipuuze, ufanywe uchunguzi ili kufahamu tatizo ni nini na nani kasababisha. Busara itumike ufumbuzi upatikane haraka iwezekanavyo, Watanzania wana haki ya kujivunia alama hiyo ya Tanzania na si kusononeka.
Upendeleo, kujuana, huyu ni mwenzetu, na rushwa visiwe na nafasi katika mchakato wa kurudisha hadhi ya ATCL, ye yote anayeonekana kuwa ni kikwazo cha mafanikio katika kampuni hiyo awekwe kando kwani ni chombo cha Watanzania, fahari ya Watanzania, mali ya Watanzania na ipo kwa ajili yao, hivyo maslahi ya taifa yazingatiwe.
Ni kwa kuzingatia hilo, ikithibitika kuwa kuna udhaifu wa kiutendaji katika menejimenti, wahusika waondolewe haraka, jukumu hilo wakabidhiwe wenye uwezo wa kuiongoza ATCL kwa ufanisi, watakaoiwezesha kampuni kumudu ushindani kwa kibiashara katika usafiri wa anga ndani na nje ya Tanzania.
Sioni tatizo kumuondoa Mattaka katika uongozi wa kampuni hiyo kama ikithibitika kuwa yeye ni tatizo ATCL, na pia sitashangaa endapo Bodi ya Wakurugenzi itavunjwa kwa manufaa ya umma kama imeshindwa kusimamia menejimenti.
Ninaamini kuwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa; wapo makini kutafuta ufumbuzi wa matatizo ATCL, na sina shaka kuwa uamuzi wa serikali utakuwa wa haki na utazingatia maslahi ya taifa.
Kwa kuwa wafanyakazi wa ATCL wameonyesha nia ya kuandamana kwenda Ikulu, Waziri Kawambwa akazungumze nao, wapewe nafasi ya kusema waliyonayo, na awaeleze serikali inafanya nini ili kurudisha hadhi ya kampuni hiyo.