Vibwagizo vilivyotia fora kwenye mahojiano ya Mwigulu na Zitto leo asubuhi

Kwa hiyo Mwigulu madawati hamsini ndio marejesho ya kodi zetu. Jamani naomba musianzishe 3d kama hizi tunaweza kuwepa ban la maisha bure humu maana mitusi inakuwa karibu kweli na keyboard. Aah
 
naomba huyu nchemba atafutiwe psychiatrists maana naona ana matatizo ya akili nahasi ni kihiyo mmojawapo wa mambo ya uchumi
 
Watu wengi sana wamesoma Ilboru,Mzumbe na kadhalika,Mbona hawajitapi.Kusoma Ilboru sio ishu,mimi nimesoma pale form one hadi Six,nina Bachelor first class ya Mlimani na Masters ya Southampton,nimefaulu vizuri tu kwenye uchumi mbona sijitapi kujiona kwamba najua na watu wengine hawajui.Siwezi kuzima hoja ya mtu eti kwa kumwambia " wewe hujui uchumi,mimi najua uchumi".I think the guy is missing something somewhere,most certainly upstairs

Hahahaaa; wajitapa kijanja eeeh!!
 
Ha ha ha ha ha haaaaaa Juzi tu nimepeleka madawati 50 kule Iramba! Yani inamaa Mwigulu anawachukulia wana Iramba cheap kiasi hicho?

Mlisema huyu jamaa ni mchumi first class??! kweli Siasa si Hasa! manina wallahi
 
This is the kind of rubbish that tanzanians must reject and reject absolutely. Hakuna anayehitaji madawati hamsini eti tumesaidiwa. Tunataka kodi zetu zifanye kazi iliyokusudiwa siyo makombo toka mezani kwenu baada ya kutuibia.

Unajua hawa jamaa walizoea kuwa kuleta/kupeleka maendeleo/huduma mahali fulani ni hisani na sio wajibu. Ndio maana kwake yeye hayo madawati 50 (subject to verification) anaona dili sana.

Ndio walikolifikisha taifa hili kwenye lindi la umaskini. CCM na serikali yao ni wapuuzi, dhaifu sana, wanafiki na SILLY kabisa!
 
Ni TBC1, refa alikuwa Marine Hassan... Sikuconcentrate kwenye points maana najua hakukuwa na jipya. Ila kwenye chorus baadhi ya mambo yalikuwa hivi

Mwigulu: Hawa wapinzani wanapotosha umma maana wanajua hata bajeti ikiamuliwa iendikwe upya kwao ni ushindi

Zitto: Mwigulu kwa maksudi kabisa anapotosha umma. Mimi naongea hoja na kwa bahati mbaya siwezi kuongea kwa jazba kama anavyofanya yeye

Mwigulu: Hata fedha za elimu kwa mfano kuendeleza shule maalumu kama Ilboru nilikosoma mimi ni za maendeleo

Zitto: Mimi chuo kikuu nilikuwa mbele yako Mwigulu, na nilipata A kwenye somo la public finance na mwalimu aliyenifundisha ni mshauri wa raisi kwenye mambo ya uchumi

Mwigulu: Kweli chuo kikuu ulikuwa mbele yangu na ulipata A, lakini wewe ulipomaliza ukakimbilia kwenye siasa, mimi niliendelea na Masters na nikapata A nyingine kwenye public finance na masomo mengine yote

Zitto: Pato la ndani kwenye maendeleo ni asilimia 0. Na hata hizo za kukopa ni asilimia 30 badala ya minimum ya 35.

Mwigulu: Hata ukimpa mtoto wa darasa la pili calculator akakokotoa bilioni 700 zilizoko kwenye elimu ni asilimia 7.2, ukijumlisha na ile 30 unapata 37.2

Zitto: Acha kupotosha umma Mwigulu. Sio suala la kukokotoa na calculator, ni suala la mantiki. Hizo bilioni 700 sio zote za maendeleo kwenye elimu bali nyingi ni mshahara na marupurupu

Mwigulu: Walioandaa bajeti ni wataalamu wa wizara ya fedha, na wanajua ni nini wanafanya. Kumbuka mimi ni waziri kamili wa fedha wa CCM, na niko jikoni.

Zitto: Hata kama ni wataalamu, nao ni binadamu. Kuna wataalamu wanafikiria familia zao tu, na kuna wanaofikiria taifa. Na pia bungeni pia wataalamu tupo na haya mambo tunayafuatilia sana

Zitto: Mwigulu kumbuka wewe ni mbunge tu uliyechaguliwa kutoka kule Iramba ambako wananchi hawana maji, wanafunzi wanakaa chini. Mbona unatetea ubovu wa bajeti?

Mwigulu: Mimi sikai tu kusubiri bajeti au kuzungazunguka kama nivyi. Juzi tu nimepeleka madawati hamsini jimboni mwangu...

My take.... Nothing to take here. chakula cha kuku (pumba) tupu...
Mwigulu hizo ni A za kukariri,lakini practical haujui kitu
 
HApa Iramba dawati moja ni Tshs.14,250/= tu

Ni kama 712,500/= so what is that token to the maendleo ya wana Iramba, or even the fiscal budget?. Aisee wana Iramba andamaneni mumkatae mbunge wenu, ni afadhali muwe hamna mbunge kuliko huyu mzinzi.

It's amazing how low he is, the first class economist is!
 
TEHE TEHE TEHE TE TE TEEEEEE MIMI NLPOSEMA JAMAA HANA LOLOTE KIMAENDELEO KATIKA JIMBO LAKE WENGINE MKASEMA THREAD YANGU INASHAMBULIA MTU, NILIPOSEMA UWEZO WAKE WA KU CONSTRUCT IDEAS NA KU INTERNALISE TO THE COMMUNITY MKASEMA MI NASEMA UWONGO, ACHA KABISA YAMEJITOKEZA SASA KWA FIRST CLASS ECONO..ANADAI KULETA MADAWATI 50 KWA SHULE NGAPI VILE? JUZI NILIPOMWONA HAPA CATHOLIC HALL SINGIDA NILIMFUATA AKANIPIGA CHENGA NILITAKA TU KUMWAMBIA UNATIA AIBU HIYO SKAFU YA NCHI YETU KWA KUTOA LAST CLASS POINTS MJENGONI KWANI MAENDELEO IRAMBA MAGHARIBI HAKUNA. MIMI NIMEZUNGUKA VIJIJI VYOTE 120 VYA IRAMBA (MAGHARIBI NA MASHARIKI) HAKUNA PENYE NAFUU. HAPO NILIPOKUWA NA MAAFISA MBALIMBALI TUKIFANYA POVERTY ANALYSIS NA IDENTIFICATION YA OVCs. SHULE ZOTE (PRIMARY AND SEC) ZIMECHOKA TENA SANA TU. YEYE ANALETA HABARI YA MADAWATI 50? HAKIKA NASEMA MWIGULU NJOO IRAMBA 2015 KUOMBA KURA KISHA UTASOMA NAMBA YAKE. M FOR C WILL MAKE YOU LEARN. LEO NIMEKUTANA NA MZEE WANGU MMOJA AKANIAMBIA ... OF WHAT BENEFIT ..... OF ONES DEGREE IF THAT DEGREE CANNOT HELP OTHERS TO ATTAIN AT LEAST A DIPLOMA IN LIFESKILLS AND SELF DEVELOPMENT WHICH LEADS TO ONE'S TRANSFORMATION? HAPO NIKASEMA ATAWAJIBU ......MBA" ANYWAY SISI NDO TUNAOUJUA UMASKINI WA JIMBO LAKO, PLEASE IRAMBA MAGHARIBI WAKE UP, ANGALIENI VIPAUMBELE VYA MHESHIMIWA MIAKA INAENDA HATA KIMOJA HAKIJATIMIA. ACHILIA MBALI HATA MKUTANO WA HADHARA TU KWA WANANCHI WAKE, AKITIA MGUU ANAOGOPA KIVULI CHAKE MWENYEWE ANATIMUA MBIO KURUDI TOWN (SGD) KWA MO. MWIGULU ATAPITA IRAMBA MAGHARIBI ITABAKI, WANANCHI AMKENI DO SOMETHING. DO NOT WAIT FOR THE LAST CLASS ECONO.
 
Ndio maana wakati fulani tulipendekeza kwamba kuna haja ya kuzisajili hizi degree na kuwapa practical license wenye kufuzu na kuweka utaratibu wa ku-renew maana hii ya mwigulu ni outright ajuwa!

His lecturers must feel very ashamed of this potato head! Nimetema mate chini!
 
Huyu jamaa anaonekana anabifu sana na LISSU na dada yake...............jana sikupenda dharau yake kabisa alipomkatiza yule dada


Mwigulu kafilisika kiakili ndo sababu badala ya kuchambua hoja anasema atawaelekeza mara ngapi Lisu na Dada yake? haya sio maneno yanayoweza toka kichwa cha mwenye akili timamu.

Hakika mwigulu amechanganyikiwa
 
Hawajui hata majukumu yao wanaishia kugawa rushwa hizo za madawati badala ya kuisimamia serikali itimize wajibu wake kuhakikisha kuwa hakuna mtoto wa shule anayekaa chini. Huyu alisoma ili apate cheti, si kuelimika.

kabisa na hiyo ni rushwa ili wananchi wamchague tena kipindi kingine maana anasema mnaona hizi ni fedha zangu nimetoa mfukoni kununu amadawati
Wakati alipaswa aisimamie serekali ihakikishe inatoa elimu bora kwa wanafunzi wa jimbo lake kwenye shule kuwe na madawati ya kutosha na vitabu na malipo ya walimu wa shule hizo yafike kwa wakati
Huyu ni yule utakuta hata walimu wa shule za jimbo lake wanasotea mshahara au wanapakia toyo kwenda kufuata mshahara mjini na shule hazina hata walimu wa kutosha au vitabu na vifaa vya maabara


Madawati hamsini ni madarasa mawili tu,
na hayo ndio maendeleo ya mtu wa fst class economy, kaazi kweli kweli.

Mkuu hilo ndo ameona amefanya la maana toka achaguliwe kuwa mbunge
Na hilo ndo analojivuni akuwa amefanya la maana kununua madawati hamsini
Je hao wanafunzi wa jimbo lake ina maana wote wana madawati ya kuwatosheleza kiasi kwamba hawahitaji mengine
Je shule za jimbo lake zina vitavu vya kutosha
je walimu wanalipwa mishahara na posho zao zote kwa wakati
Je barabara za jimbo lake zote ziko vyema zina lami na zinapitika kwa mwaka mzima
Je jimboni mwake kuna madawa kwenye hospitali ya kutosha na wananchi wake wanahudumiwa kwa wakati na huduma ni bora
je wahudumu hao wa afya wana malipo mazuri ya mishahara na marupurupu kiasi kwamba hawana shida yoyote
Je jimboni mwake mfumuko wa bei ni wa chini sana kiasi kwamba wananchi wake hawana shida
Je petrol na bidhaa za mafuta jimboni mwake ziko chini sana kiasi kwamba wananchi wake hawana shida yoyote
Je umeme na maji kwenye jimbo lake ni vitu ambavyo havina shida wananchi wake wanao mpaka wa ziada hawahitaji huduma hiyo tena
Je bidhaa mbalimbali kwenye jimmbo lake zinapatikana kwa bei nzuri na zote zipo hana shida yoyote
Mhh mbona maswali ni mengi sana kwake
 
uchukulia dawat moja la watu wawil hata liuzwe laki ni milion 5 sa unautangaziaa umma kwa kias hich cha pesa ili muiba bilion
 
unajua hawa jamaa walizoea kuwa kuleta/kupeleka maendeleo/huduma mahali fulani ni hisani na sio wajibu. Ndio maana kwake yeye hayo madawati 50 (subject to verification) anaona dili sana.

Ndio walikolifikisha taifa hili kwenye lindi la umaskini. Ccm na serikali yao ni wapuuzi, dhaifu sana, wanafiki na silly kabisa!

madawati hamsini mheshimiwa anajivunia. Ok! Bahati mbaya sikuona madawati yenyewe ni ya kiwango gani. Lakini mimi binafsi nilipita katika tarafa moja na kukutana na kilio cha madawati ilibidi tukashauriana na rafiki yangu tukakubaliana tununue madawati kwa ajili ya baadhi ya shule za eneo hilo, hatimaye katika kujadili na mjasiriamali mwenzangu tukanunua madawati 85 (yana mbao kwa juu na stand zake za chuma) dawati moja shilingi 75000 (75000x 85) sasa wewe na first yako madawati 50 hapo haujaweka cha juu na uongo kiasi si utasema mengi? Point sio madawati come to the constituent and make changes. Soma alama kijana wairamba hawajalala kama unavyodhani. Kumbuka ulipewa kwa ajili ya watu ku test new flavor baada ya iliyokuwepo kuwa sour, sasa imagine test yako 2015 itakuwa kama shubiri nani ameze kitu. Mpaoo musigazi coz you cant be musheija.
 
Huyu jamaa sikujua kama alifanyakazi BOT, sasa naona anavyolipuka Bungeni ninakuwa na maswali ya kujiuliza. Uzalendo huu alionao sasa alikuwa nao toka anasoma? Alikuwa nao akiwa anafanyakazi BOT? Alikuwa nao pesa za EPA zikikwapuliwa? Alikuwa nao majengo pacha yakifanyiwa usanii? Hii urembo anao uweka shingoni ni kwaajili ya kufunika na kutupumbaza sie. Komba hata muda wake wa kuimbia TOT umeisha, ni bora akachukue mikoba kule kwenye Bendi. Muda sio mrefu watakuwa na kazi ya kuwaambia wananchi kuwa walifanya makosa kweli wawape ridhaa tena mwaka 2020.
 
iramba sehemu za ndago kuna mbao za mninga,sasa kama yeye kapeleka madawati hatumii akili!angewezesha vifaavyauseremala
 
Huyu bana ndo THINK TANK WA CCM baada ya John Malecela na Pius Msekwa kufilisika kisiasa. Akiongea unasikia kabisa mlio wa debe tupu.
 
madawati hamsini kwa jimbo zima
Ina maana hayo ndio aliyotumwa kuwapigania wananchi wake
je hayo madawati hamsini ni kwa shule ngapi za jimbo lake
na toka amechaguliwa ndo amepeleka hayo madawati hamsini
na hayo ndio maenedeleo ya watu wa jimbo lake aliyotumwa kupigania
je madawa, miundo mbinu, mfumuko wa bei nayo nani anaongelea

mwenyekiti wa kijiji anapaswa kujivunia madawadi hamsini na siyo mbunge....
 
Mwigulu ameiuza nafsi na utu wake kwa CCM. Sasa anapigania na kusimamia yale asiyoyaamini.
Wale wenye uwezo wa kuongea na mwenyezi Mungu, naomba watume maombi maalum ili kijana mwenzetu akombolewe.
Kumlaumu wala hakusaidii, zaidi tutampoteza moja kwa moja. mjue hiyo elimu kaipata kwa kodi zetu wenyewe.
Tumsaidie ili arudishe utu wake, anaweza kutufaa mbele ya safari.
Mbona bakhresa ananunua chupa tupu za maji na anazisafisha na kutuuzia zikiwa na maji tena?
 
Hawajui hata majukumu yao wanaishia kugawa rushwa hizo za madawati badala ya kuisimamia serikali itimize wajibu wake kuhakikisha kuwa hakuna mtoto wa shule anayekaa chini. Huyu alisoma ili apate cheti, si kuelimika.

Madawati hamsini ni madarasa mawili tu,
na hayo ndio maendeleo ya mtu wa fst class economy, kaazi kweli kweli.

mwenyekiti wa kijiji anapaswa kujivunia madawadi hamsini na siyo mbunge....

Kabisa mkuu
Hata mimi naweza jivunia nimetoa madawati hamsini na mchango wa kujenga darasa kijijini kwetu bana
 
Back
Top Bottom