Vibwagizo vilivyotia fora kwenye mahojiano ya Mwigulu na Zitto leo asubuhi

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Ni TBC1, refa alikuwa Marine Hassan... Sikuconcentrate kwenye points maana najua hakukuwa na jipya. Ila kwenye chorus baadhi ya mambo yalikuwa hivi

Mwigulu: Hawa wapinzani wanapotosha umma maana wanajua hata bajeti ikiamuliwa iendikwe upya kwao ni ushindi

Zitto: Mwigulu kwa maksudi kabisa anapotosha umma. Mimi naongea hoja na kwa bahati mbaya siwezi kuongea kwa jazba kama anavyofanya yeye

Mwigulu: Hata fedha za elimu kwa mfano kuendeleza shule maalumu kama Ilboru nilikosoma mimi ni za maendeleo

Zitto: Mimi chuo kikuu nilikuwa mbele yako Mwigulu, na nilipata A kwenye somo la public finance na mwalimu aliyenifundisha ni mshauri wa raisi kwenye mambo ya uchumi

Mwigulu: Kweli chuo kikuu ulikuwa mbele yangu na ulipata A, lakini wewe ulipomaliza ukakimbilia kwenye siasa, mimi niliendelea na Masters na nikapata A nyingine kwenye public finance na masomo mengine yote

Zitto: Pato la ndani kwenye maendeleo ni asilimia 0. Na hata hizo za kukopa ni asilimia 30 badala ya minimum ya 35.

Mwigulu: Hata ukimpa mtoto wa darasa la pili calculator akakokotoa bilioni 700 zilizoko kwenye elimu ni asilimia 7.2, ukijumlisha na ile 30 unapata 37.2

Zitto: Acha kupotosha umma Mwigulu. Sio suala la kukokotoa na calculator, ni suala la mantiki. Hizo bilioni 700 sio zote za maendeleo kwenye elimu bali nyingi ni mshahara na marupurupu

Mwigulu: Walioandaa bajeti ni wataalamu wa wizara ya fedha, na wanajua ni nini wanafanya. Kumbuka mimi ni waziri kamili wa fedha wa CCM, na niko jikoni.

Zitto: Hata kama ni wataalamu, nao ni binadamu. Kuna wataalamu wanafikiria familia zao tu, na kuna wanaofikiria taifa. Na pia bungeni pia wataalamu tupo na haya mambo tunayafuatilia sana

Zitto: Mwigulu kumbuka wewe ni mbunge tu uliyechaguliwa kutoka kule Iramba ambako wananchi hawana maji, wanafunzi wanakaa chini. Mbona unatetea ubovu wa bajeti?

Mwigulu: Mimi sikai tu kusubiri bajeti au kuzungazunguka kama nivyi. Juzi tu nimepeleka madawati hamsini jimboni mwangu...

My take.... Nothing to take here. chakula cha kuku (pumba) tupu...
 
Hivi hiyo fist class ya Mwigulu ni ya ukweli au mnampakazia!!! Kama ni ya kweli basi jamaa ni mkali wa kuegesha.......... Inaeleka kisha sahau kabisa uchumi wote mara tu baada ya mtihani wa mwisho!!!

Halafu mambo mengine yanahitaji kutumia logic.......... mfano huwezi kutoa jibu kama hili kwenye swali hili!!

unaambiwa ana first class ya adultery.
 
madawati hamsini kwa jimbo zima
Ina maana hayo ndio aliyotumwa kuwapigania wananchi wake
je hayo madawati hamsini ni kwa shule ngapi za jimbo lake
na toka amechaguliwa ndo amepeleka hayo madawati hamsini
na hayo ndio maenedeleo ya watu wa jimbo lake aliyotumwa kupigania
je madawa, miundo mbinu, mfumuko wa bei nayo nani anaongelea
 
Mwigulu: Mimi sikai tu kusubiri bajeti au kuzungazunguka kama nivyi. Juzi tu nimepeleka madawati hamsini jimboni mwangu...

My take.... Nothing to take here. chakula cha kuku (pumba) tupu...

Aisee hili ni janga yaani jimbo zima kuna wanafunzi HAMSINI tu
 
madawati hamsini kwa jimbo zima
Ina maana hayo ndio aliyotumwa kuwapigania wananchi wake
je hayo madawati hamsini ni kwa shule ngapi za jimbo lake
na toka amechaguliwa ndo amepeleka hayo madawati hamsini
na hayo ndio maenedeleo ya watu wa jimbo lake aliyotumwa kupigania
je madawa, miundo mbinu, mfumuko wa bei nayo nani anaongelea
Hawajui hata majukumu yao wanaishia kugawa rushwa hizo za madawati badala ya kuisimamia serikali itimize wajibu wake kuhakikisha kuwa hakuna mtoto wa shule anayekaa chini. Huyu alisoma ili apate cheti, si kuelimika.
 
Alafu ninapochoka CCM wanamtegemea huyu kujibu almost kila kitu uku akina mama Simba utamsikia waambie hao!
Utategemeaje hela za wahisani kwenye dvt expenditure wasipokupa?

Fedha za maendeleo ilibidi zitoke kwenye mapato ya ndani ili miradi yetu isikwame. Hivi hamjui iyo miradi ina chain impact kwenye uchumi wetu ie reli,barabara,bandari etc.

Hivi posho zina impact gani kwenye uchumi wetu kama sio kuneemesha wachache na kukuza anasa!
 
Huyu jamaa anaonekana anabifu sana na LISSU na dada yake...............jana sikupenda dharau yake kabisa alipomkatiza yule dada
 
This is the kind of rubbish that tanzanians must reject and reject absolutely. Hakuna anayehitaji madawati hamsini eti tumesaidiwa. Tunataka kodi zetu zifanye kazi iliyokusudiwa siyo makombo toka mezani kwenu baada ya kutuibia.
 
Watu wengi sana wamesoma Ilboru,Mzumbe na kadhalika,Mbona hawajitapi.Kusoma Ilboru sio ishu,mimi nimesoma pale form one hadi Six,nina Bachelor first class ya Mlimani na Masters ya Southampton,nimefaulu vizuri tu kwenye uchumi mbona sijitapi kujiona kwamba najua na watu wengine hawajui.Siwezi kuzima hoja ya mtu eti kwa kumwambia " wewe hujui uchumi,mimi najua uchumi".I think the guy is missing something somewhere,most certainly upstairs
 
madawati hamsini kwa jimbo zima
Ina maana hayo ndio aliyotumwa kuwapigania wananchi wake
je hayo madawati hamsini ni kwa shule ngapi za jimbo lake
na toka amechaguliwa ndo amepeleka hayo madawati hamsini
na hayo ndio maenedeleo ya watu wa jimbo lake aliyotumwa kupigania
je madawa, miundo mbinu, mfumuko wa bei nayo nani anaongelea

Madawati hamsini ni madarasa mawili tu,
na hayo ndio maendeleo ya mtu wa fst class economy, kaazi kweli kweli.
 
Mwigulu: Mimi sikai tu kusubiri bajeti au kuzungazunguka kama nivyi. Juzi tu nimepeleka madawati hamsini jimboni mwangu...

Hizo fedha za kupeleka madawat anatoa wap?je ndio tuseme wabunge siku hz ndio wafanye kazi za kuendeleza majimbo
kwa fedha zao na hivyo hakuna haja ya kuhangaika na budget ya serikali?
 
Back
Top Bottom