Vibaka washamiri daraja la Manzese

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
Saturday, August 01, 2009 11:01 AM
WAKAZI wa Manzese darajani wameitaka Manispaa kuimarisha ulinzi darajani hapo kwa kuwa vibaka wameweka kambi eneo hilo.
Wakazi hao waliitaka manispaa kuimarisha ulinzi katika daraja hilo kwa kuwa wezi na vibaka walikuwa wakijificha na kutishia maisha ya wakazi wa maeneo hayo.

Wamesema wezi hao hujificha katika daraja hilo na hupora mali za watu pindi weanapopita darajani humo.

Wamesema kuwa nyakati za usiku vibaka wamekuwa wakijificha darajani humo hali inayofanya wakazi kuogopa kulitumia daraja hilo na kuvuka njia ya kawaida chini na kusababisha idadi ya ajali kuongezeka

Wakazi wa maeneo hayo wameiomba manispaa kuweka walinzi kwenye daraja hilo kwani daraja hilo litakuwa halina faida kama wakazi wa eneo hilo wataendelea kuogopa kulitumia kwa kuhofia kukabwa na wezi wanaowasubiria watu kwenye daraja hilo.
 
Hawa vibaka hawa wengi wao walikimbia shule kwa hiyo kwa vile wanajua kabisa wamefulia wanakaba watu huku wakisingizia mafisadi......
 
lile eneo ni hatari sana na hakuna mtu asiyejua ila hakuja juhudi zozote zinazofanywa na wakazi wa eneo lile katika kukabiliana na tatizo hili, nakumbuka mwaka 1999 nikiwa kwenye daladala nilikaa siti ya dirishani vibaka walifanikiwa kunipora gazeti.
 
nakumbuka mwaka 1999 nikiwa kwenye daladala nilikaa siti ya dirishani vibaka walifanikiwa kunipora gazeti.
Duh !!! Mkuu sasa hii kali ina maana walijua umefunga hela kwenye hilo gazeti nini? au huyo kibaka alikuwa kwenye training........ahahhahahha
 
Duh !!! Mkuu sasa hii kali ina maana walijua umefunga hela kwenye hilo gazeti nini? au huyo kibaka alikuwa kwenye training........ahahhahahha

Hahahahaha nafikiri jamaa alikuwa mafunzoni ama labda lilikuwa gazeti KIU/ IJUMAA jamaa kaiba akamalizie hadithi, siunajua zile hadithi za Shigongo zinazokwenda mpaka sehemu ya 53,..,..,.. nakuendelea manake jamaa maeneo hayo wanazifagilia sana hizo.
 
Back
Top Bottom