Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vibaka kuzunguka Ikulu, Usalama upo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lebabu11, Apr 13, 2010.

  1. l

    lebabu11 JF-Expert Member

    #1
    Apr 13, 2010
    Joined: Mar 27, 2010
    Messages: 1,192
    Likes Received: 239
    Trophy Points: 160
    Hello wana JF,

    Nimeshuhudia matukio ya vibaka kuvamia wapita njia (Ocean Road) kwenye mpaka wa IKULU mara mbili.

    Tukio la kwanza lilitokea majira ya jioni baada ya wanawake wawili kuegesha gari yao pembeni kwa dharura, walivamiwa na vibaka wakanyang'anywa simu na mikoba yao na niliposimama kutoa msaada, vibaka hao walikimbia wakiwa na mali walizopora.

    Pili imetokea juma lililopita saa sita mchana baada ya kijana mmoja mtembea kwa miguu kusimamishwa na vibaka, kumpiga makonde mazito baada ya kupinga amri yao huku wengine wakimpekua mifukoni wakachukua simu pesa na viatu kisha kutimkia ufukweni.

    Tukio hilo lilitolewa taarifa kituo cha polisi Kivukoni na polisi walikiri ni matukio ya kawaida pale hivyo watafuatilia!

    Wadau, Nini kifanyike?

    [​IMG]


    [​IMG]

    Kwa tahadhari zaidi soma;

    Jihadhari unapokuwa maeneo haya Dar es Salaam


    Daktari Mgiriki auwawa Tanzania..

     

    Attached Files:

  2. bht

    bht JF-Expert Member

    #2
    Apr 14, 2010
    Joined: May 14, 2009
    Messages: 10,171
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135
    Waheshimiwa,

    Jana usiku wa saa mbili na nusu katika eneo la daraja la Selander, nilishuhudia mwanaume mwenye asili ya kizungu akiwa kang'ang'aniwa na vijana wa kibongo kama sita hivi kwa nia ya 'kumsachi' na kumpora

    Matukio kama haya yalivuma sana miezi kadhaa ya nyuma kisha kukawa shwari, na wengi wetu labda tulidhani sasa hakuna hatari tena (mimi nikiwemo)

    kwa nililoshuhudia jana ni wazi kwamba bado tunapaswa kuwa makini sana tupitapo maeneo yale.

    Cha kushangaza hili lilitokea almost right infront of the police station, mwanzo kabisa wa daraja ukiwa unatokea mjini.

    Usalama hakuna kwa eneo la kituo cha polisi , je huko vichochoroni kwetu??

    Anyways it was just a word to alert you all, msijiachie mkipita pale kwenye gari na simu zenu na 'pochi' zitadakwa kama mwanzo.

    TEKEA PEOPLE
     
  3. Teamo

    Teamo JF-Expert Member

    #3
    Apr 14, 2010
    Joined: Jan 9, 2009
    Messages: 12,278
    Likes Received: 25
    Trophy Points: 145
    POA MPWA!
    tatizo wazungu wanajiachia sana wakati vijana wetu wana njaa
     
  4. Msanii

    Msanii JF-Expert Member

    #4
    Apr 14, 2010
    Joined: Jul 4, 2007
    Messages: 6,223
    Likes Received: 62
    Trophy Points: 145
    dah mzungu aliweza kuvumilia roba ya mbao kweli? naamini akirudi kwao ataenda kuandika kitabu kinachohusu kabari za kiafrika,

    Sina shaka kwamba hao vibaka wakishamaliza kukusanya hesabu za siku lazima wapitie hapo polisi salenda kulipia bili yao maana inaonesha hao polisi wanawalinda vibaka wasiibiwe wala hawawalindi raia wema.
     
  5. Bujibuji

    Bujibuji JF-Expert Member

    #5
    Apr 14, 2010
    Joined: Feb 4, 2009
    Messages: 27,159
    Likes Received: 5,385
    Trophy Points: 280
    Tatizo sio wazungu.
    Tatizo ni polisi walioshindwa kudhibiti uhalifu.
    Je kutoka kituoni hadi darajani panahitaji petroli ya kuweka kwenye gari?
     
  6. bht

    bht JF-Expert Member

    #6
    Apr 14, 2010
    Joined: May 14, 2009
    Messages: 10,171
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135
    yeah wajifanyaga kupita pale waki jogi mzee wanakutana na vijana kazini

    ila Selander panataka kuwa kama jangwani, ukiharibikiwa na gari jnagwani uikimbie mwenyewe uwaachie......
     
  7. bht

    bht JF-Expert Member

    #7
    Apr 14, 2010
    Joined: May 14, 2009
    Messages: 10,171
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135
    jamaaa was tall enough kwa hiyo vibaka walimdandia kama wanarukia mapera vile
    polisi wa pale wanajua 'wat goes on'.....sasa sijui kwa nini hawachukui hatua madhubuti!!!

    hiyo kweli inaweza kutufanya tuhisi kuwa kuna baraka zao kwenye huu uhalifu pale
     
  8. BornTown

    BornTown JF-Expert Member

    #8
    Apr 14, 2010
    Joined: May 7, 2008
    Messages: 1,702
    Likes Received: 89
    Trophy Points: 145
    hii inatisha kwa kweli.. kuna kipindi cha nyuma ndugu yangu alikuwa napita ilikuwa saa 1830 jioni askari wakamsimamisha wakamwambia arudi pambeach akkapande basi maana pale sio salama pana vibaka wengi sasa akawauliza ikiwa mnajua kuna vibaka kwanini msiwashuhulikie kama askari wenyewe mnawaopgopa vibaka sie raia tufanyaje yule askari akamwambia mie ndio nakuambia sasa kama unalete ubishi yakikupa yakukupata usije kutulilia. nIlijiuliza maswali mengi sikupata jibu

    wiki iliopita kuna doria ya maaskari walikuwa wanazunguka mitaa ile kuanzia mwazo wa daraja hadi pale ubalozi wa urusi kumbe hii yote ni nguvu ya soda.

    Kuna swali huwa najiuiza hivi ule ulinzi ulikuwapo kipindi kile cha awamu ya 2 uko wapi pale darajani?? ama tumrudishe mzee ruksa madarakani atusaidie kuimarisha ulinzi??
     
  9. Msanii

    Msanii JF-Expert Member

    #9
    Apr 14, 2010
    Joined: Jul 4, 2007
    Messages: 6,223
    Likes Received: 62
    Trophy Points: 145
    wewe hujiulizi hawa majambazi wanapata wapi silaha za kushambulia mawindo yao? jibu unalo.

    Polisi wana maslahi madogo hivyo ni rahisi kushawishika kufanya faulo mbaya ktk kazi zake ilhali apate chochote cha kukeep familia yake inayoishi ktk jokofu (jumba la mabati kota)
     
  10. Zogwale

    Zogwale JF-Expert Member

    #10
    Apr 14, 2010
    Joined: Jul 10, 2008
    Messages: 11,470
    Likes Received: 591
    Trophy Points: 280
    Ipo wazi kuwa Polisi pale Selender Bridge wanapata gawio la nguvu toka kwa wale vibaka.
     
  11. bht

    bht JF-Expert Member

    #11
    Apr 14, 2010
    Joined: May 14, 2009
    Messages: 10,171
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135

    Obvious tatizo liko kwa polisi, maana hata wakisimama tu pale nje they could see the whole scenario!!
     
  12. bht

    bht JF-Expert Member

    #12
    Apr 14, 2010
    Joined: May 14, 2009
    Messages: 10,171
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135
    kumbe wameridhia hii hali eeh
    vibaka wamejipatia baraka kwa polisi....

    hapo ndipo huwasukuma raia kujichukulia hatua mkononi
     
  13. Msanii

    Msanii JF-Expert Member

    #13
    Apr 14, 2010
    Joined: Jul 4, 2007
    Messages: 6,223
    Likes Received: 62
    Trophy Points: 145
    POLISI jamii ndivyo ilivyo
    maana hata vibaka ni sehemu jamii na polisi wanadumisha udugu na jamii yote bila madhara.

    Unategemea nini kwa askari ambaye alijiunga na jeshi baada ya kuona hana pass marks nzuri za kuendelea mbele kimasomo?
    Tatizo ni namna recruitment za kujiunga na polisi zinavyoendeshwa na siyo namna wanavyofanya kazi. Wanaajiri ndugu zao et all na utakuta hawana lolote zaidi ya utendaji wa KIMAPOKEO na si wa kwenda na mabadiliko ya tabia-watu.

    Tuwape motisha askari wetu kwa kuwaandalia semina mbalimbali za kukuza uelewa wao ktk masuala ya kiteknolojia na kujitambua..... Najua CCM watapinga hili kwa manufaa yao
     
  14. T

    Tall JF-Expert Member

    #14
    Apr 14, 2010
    Joined: Feb 27, 2010
    Messages: 1,433
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 0
    eeeeeh,ndio inavyokuwa,kumtia roba TALL iko kazi.
     
  15. M

    Mdondoaji JF-Expert Member

    #15
    Apr 14, 2010
    Joined: Mar 17, 2009
    Messages: 5,102
    Likes Received: 38
    Trophy Points: 145
    inasikitisha sana kwakweli
     
  16. Bigirita

    Bigirita JF-Expert Member

    #16
    Apr 14, 2010
    Joined: Feb 12, 2007
    Messages: 13,582
    Likes Received: 332
    Trophy Points: 180
     
  17. h

    housta Senior Member

    #17
    Apr 14, 2010
    Joined: May 25, 2009
    Messages: 160
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 33
    Silaha zina sehemu nyingi sana ya kupatikana. Somalia hapako salama na border zetu na Kenya haziko 100% secured. Sasa hizo silaha, tena latest ambazo hata majeshi yetu hayana unadhani zitaacha kupita na kuwafikia walengwa(majambazi). We just need to secure our borders na kuimarisha majeshi yetu. Kuimarisha namaanisha kuwapa kipaumbele kwenye maslahi pamoja na kuwa na jeshi lenye heshima na utii. Jeshi lenye kujali maisha ya raia na mali zao. Na sio jeshi lenye njaa.

    Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu. Ni maoni tu!
     
  18. I

    Isae Member

    #18
    Apr 14, 2010
    Joined: Aug 14, 2009
    Messages: 79
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 15
    Inaelekea kweli si salama kwani wakati wa jioni ukipita utakuta polisi wanalinda na wakati mwingine kuna kampuni ya ulinzi kwa hiyo naamini polisi wanafahamuhilo
     
  19. Tusker Bariiiidi

    Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

    #19
    Apr 14, 2010
    Joined: Jul 3, 2007
    Messages: 4,588
    Likes Received: 37
    Trophy Points: 145
    Siku za kituo polisi cha Selander zinahesabika pamoja na zile ghorofa mbili za NHC haswa katika mpango wa kupunguza foleni Jijini lazima kipitiwe!!! Hii ni baada ya Barabara mpya na daraja jipya kuongezwa kutokea Kenyatta Road (Oysterbay) mpaka Ocean Road (Seaview)...
     
  20. bht

    bht JF-Expert Member

    #20
    Apr 14, 2010
    Joined: May 14, 2009
    Messages: 10,171
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135
    mpwazz kwa hiyo hili litasaidaje kupunguza na vibaka kama hali hii na kuna kituo cha apolisi pale pale

    au kwa vile zile swamps zitatolewa pale maficho yatakosekana?
     
Loading...