Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,269
- 675
- Thread starter
- #21
Kikwete anaimudu kazi yake pamoja na changamoto zilizopo.Kila awamu inakutana na changamoto tofauti kulingana na hali halisi ya wakati wake.
Nyerere aliipigisha Tanzania mark time kwa miaka takriban 25 akiiacha nchi ikiwa haina mwelekeo mzuri kiuchumi.Bwana huyu ambaye kwa jina jingine aliitwa Haambiliki alikuwa akiongoza nchi kama akili yake ilivyokuwa ikimtuma.Kam unabisha muulize Edwin Mtei kwa nini alimwaga manyanga.Uzao wa sasa hauwezi kujua adha iliyokuwepo enzi za Nyerere na kwa ufupi Mungu apishe mbali enzi hizo zisirudi tena.Waliokufa kwenye kampeni a vijiji ambao idadi yao haitambuliki Mungu awalaze mahali pema Amin.Wale walioporwa nyumba zao walizozijenga kwa jasho lao poleni.Wale waliopoteza maisha yao kwa vita kwa sababu za kimtazamo na tofauti za viongozi poleni.Wale ambao walipambana na kampeni ya kupambana na walanguzi na kutupa mali zao porini au baharini poleni maskini.Na hatimaye hata wale waliolazimika kutembea nusu uchi kwa kukosa mavazi na kuvaa makatambuga kwa sababu ya ukiritimba wa Haambiliki poleni pia.Hatimaye mambo yalipofika shingoni mwake akaleta msamiati wa kizanaki...kung'atuka.
Mzee Ruksa alikuwa katika hali ngumu sana lakini baada ya wiki moja akatangaza kuwa hakuna tena mgao wa mafuta ya petroli na baadaye hatua kwa hatua nchi ikafunguka na kwa mara ya kwanza watu wakaanza kuangalia tv!Magazeti yakaanzishwa pamwe na vituo vya TV na maisha yakawa tofauti kabisa na yale ya enzi za Mwalimu.Watanzania wakanza kuona nguo zinapatikana madukani na wakaanza kuvaa viatu na kununua kila walichokitaka bila kuuliza mtu.Hiyo lebo ya Ruksa ndipo ilipopatikana maana huko nyuma kila kitu hat betri za tochi ilibidi zipitie kamati ya ugawaji.Mwinyi alijikuta katika kipindi kigumu baada ya aliemtangulia kuona mafanikio yake na akaanza kumchora.Pamoja na hayo Mzee huyo Mstaarabu alikuwa mtulivu hadi kipindi cha Ufisadi Mkubwa kilipoingia.
Mkapa aliyofanya hakuna haja ya kuyadondoa kwa sababu kizazi hiki kinayatambua.Makubwa ni kujenga barabara, kuua Wapemba na kuiba mali za umma.Hatuoini Nyerere au Mwinyi Towers hapa.Sijui waliogopa au hawakupata fursa?
Kwa Kikwete hatujaona jambo la kushtua nchi kama mauaji ya Mazegenuka,Mwembechai na Wapemba! Vitisho dhidi ya Wananchi havipo na uhuru umezagaa kila pembe.Hali ya uchumi haijawa na unafuu lakini huwezi kuilinganisha na enzi za Mwalimu,Mwinyi na za Mkapa.Kuna matumaini ya Kikwete kupata kile ambacho waliomtangulia hawakuweza kukipata.JK amefanya kazi nzuri pamoja na changamoto zilizopo na siku hizi Watanzania wanamiliki vitu ambavyo zamani ilikuwa ndoto.Tatizo letu hatuyaoni mazuri ya JK kwa sababu hatujui mabaya ya Nyerere,Mwinyi na Mkapa.
Si Nyerere,Mwnyi au Mkapa anaweza kugusa kiatu cha Kikwete.Jama huyu ni tofauti kabisa.Ni binadamu wa kuigwa na kiongozi wa kipekee kabisa.Tumshukuru Mungu!
Mwinyi naye
Underlined, kumiriki vitu kwa watanzania sio Tatizo, juulize kidogo anayemiliki ni nani?? Mtanzania au?? historia yake ikoje?? ukipata hayo majibu yake basi utaelewa kwamba bado kuna tatizo
Red:Najua mambo yanabadilika sana kutokana na utandawazi but jiulize huu mfumko wa bei unatoka wapi???