Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 3,985
- 2,770
Nawasalimu wote hasa wale wenye moyo wa huruma na upendo kwa wenzetu wahitaji. Nimekwenda Muhimbili Jana kwenye Wodi ya Mwaisela namba 1. Lengo langu lilikuwa kumjulia hali Msanii wa Komedi VENGU baada ya kutokumuona kwenye kipindi muda mrefu na kusikia amelazwa Muhimbili.
Niliwakuta Ndugu zake ambao walinikaribisha kwa upendo katika kumjulia hali Ndugu yao. Jamani kusema ukweli Yule kijana anaumwa na anahitaji Sala na Maombi yetu. Hatambui mtu wala hawezi kuongea. Waliniambia kwa sasa wanashukuru mungu ana nafuu baada ya kukaa ICU muda mrefu tangu Masanja alivyokuwa anasema Jembe lake linaumwa bila kufafanua.
Nawaombeni mwenye nafasi , hali na mali akamjulie hali Kijana huyu. Alituburudisha wengi kwa USANII wake wa KOMEDI tulicheka alipokuwa Mzima. Na sasa tukamuone hospitali kwani ni jambo la dhawabu kumuona mgonjwa. Wengi labda walikuwa hawajui kalazwa wapi ni MUHIMBILI, Mwaisela WARD 1.
Labda tunaweza kuomba serikali iingilie kati Ugonjwa wake naye wampeleke INDIA ili arudi Chuoni na Kazini kwake. Mungu amnyoshee mkono wake wa uponyaji Josef Shamba.
Amen.