Vengu anaumwa nini?

Mla Mbivu

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
224
48
naona kila wiki kwenye origino komedi masanja lazima amalize kwa kusema jamaa anaumwa.
 
anaumwa ugonjwa wa mrema..upupu wa milele yaani kujikuna mwanzo mwisho
 
watanzania tuna roho mbaya ile mbaya....unafanyaje maskhara na maradh ya mwenzio,hujui anataabika jamani!
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza anaumwa nini, lakini kwa jinsi watu walivyojibu sijapata jibu la maana mpaka sasa.
 
hata mie naona watu wanaleta masihara tu hapa.................. Mwenye taarifa za ugonjwa wa kijana mwenzetu atujuze ili tumuweke kwenye maombi na duaaa........apone.................
 
Naona mpaka mtu afe ndiyo waanze kusikitika, jamaa alikuwa nyingi........!
 
anaumwa ugonjwa wa mrema..upupu wa milele yaani kujikuna mwanzo mwisho
Wakati mwingine tujifunze kuweka utani pembeni kwenye mambo ambayo yako serious. Vengu anaumwa kweli, tena sana, anakaribia kumaliza mwezi yupo kitandani wala hajitambui, wiki iliyopita madaktari muhimbili walimuhamishia ICU baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya..anahitaji maombi yetu kwakweli, acha utani ndugu yangu, mwombee mwenzio sababu hajapenda kulala kitandani, nna hakika hakuna anayejiombea ugonjwa, kila mtu angependa kuwa na afya njema siku zote.. Ila kumbuka pia kuna mipango ya Mungu!
 
Kweli jamaa anaumwa sana, sidhani kama ni ajali. Tulisikia kuwa anasumbuliwa na kisukari. Hakujua historia ya ugonjwa inavyosemekana mpaka hali ikafikia ilipo. Mungu atampa nguvu na atarejea katika maisha yake ya kawaida.
 
Ni kweli sio ajali...alizima ghafla wakafikiri ni malaria, akatibiwa hakupata nafuu kabisa baada ya hapo akafanyiwa vipimo zaidi, nafikiri ndipo sukari ilipogundulika...tunamwombea kwa mungu apone upesi..
 
[h=2]Pole sana Vengu! Tunakuombea Upone haraka na tunamuombea na mrema naye apone![/h]Tujifunze kuwa na huruma na maumivi ya wengine pia kutokana na hili!!!

Kweli jamaa anaumwa sana, sidhani kama ni ajali. Tulisikia kuwa anasumbuliwa na kisukari. Hakujua historia ya ugonjwa inavyosemekana mpaka hali ikafikia ilipo. Mungu atampa nguvu na atarejea katika maisha yake ya kawaida

quote_icon.png
By Chezo

Back
Top Bottom