Velentine day

Utamu

Member
Feb 2, 2012
26
2
valentine day ndo imekaribia,
ikiwa ni siku ya wapendanao,ndugu jamaa na marafiki kukaa pamoja,
natoa nafasi kwa atakayejisikia kuwa pamoja nami siku hiyo,
kukaa,kula,kunywa kuongea na ku dance
 
valentine day ndo imekaribia,
ikiwa ni siku ya wapendanao,ndugu jamaa na marafiki kukaa pamoja,
natoa nafasi kwa atakayejisikia kuwa pamoja nami siku hiyo,
kukaa,kula,kunywa kuongea na ku dance

Siku ya uzinzi na kufumaniana hii siipendi kama nini
 
FEBRUARI ni mwezi wa mahaba kama inavyojulikana kwa wengi. Ni kipindi cha kuonyesha upendo hasa kwa adui zetu, pia ni wakati wa suluhu na amani kuanzia kwenye familia hadi jamii.

Zipo simulizi mbalimbali kuhusu siku ya Valentine inayosherehekewa kote duniani kwa watu kueneza upendo wa kiroho, licha ya maana halisi ya siku hii kugeuzwa kutokana na sababu za ‘usasa'.

Imo kwenye akili za watu wengi hasa wanaotoka nchi za Magharibi. Hii ni moja ya simulizi inayoaminika zaidi kwamba tangu karne ya tatu, enzi za utawala wa Kirumi chini ya Mfalme Claudius II, aliyeamini kuwa askari mkakamavu lazima awe kapera (asiyeoa) hasa wakati huo ambapo kulikuwa na vita katika taifa hilo.

Kwa mawazo yake, jambo hilo lilimlazimu kuwaamuru askari wote wa Kirumi kutokuwa na wenza, jambo lililomkera Valentine, kijana aliyejitoa kwa ajili ya kueneza upendo na amani, aliyekuwa mfungisha ndoa kwa Warumi.

Baada ya tangazo la Mfalme Claudius II, mabinti na askari wa nchi hiyo ambao hawakuwa na wenza walihuzunika lakini wengi wao walipata faraja baada ya Valentine kupinga agizo la mfalme na kuamua kufungisha ndoa kwa siri.

Hata hivyo, taarifa za Valentine kukaidi agizo la mfalme zilimfikia Claudius II, aliyeamuru kukamatwa kwa kijana huyo ili auawe. Kweli, Valentine alitiwa gerezani.

Wakati anatumikia kifungo hicho, palikuwa na binti wa mkuu wa gereza hilo aliyekuwa akipenda jinsi Valentine alivyoishi, hivyo alikuwa akienda kwa siri gerezani humo kumtembelea.

Binti huyo alionyesha upendo na hata siku aliyouawa Valentine, aliandika barua kwa msichana huyo na mwisho aliweka anuani iliyosomeka: ‘From your Valentine' (kutoka kwa Valentine wako). Siku hii ilikuwa Februari 14 mwaka 270 na baadaye alitangazwa kuwa mtakatifu.

Tangu wakati huo, jamii ilianza kuadhimisha siku ya upendo kwa watu wote. Hata ulipoingia Ukristo, Warumi waliendelea kusherehekea Sikukuu ya Wapendanao (Valentine's Day), lakini wakabadilisha kutoka fikra ya upagani ya ‘mapenzi ya kiroho' (spiritual love) na kuleta fikra ya ‘mapenzi ya mashujaa' (candle love), yaliyowakilishwa na Mtakatifu Valentine, aliyeuawa kwa ajili ya kutetea mapenzi na amani.

Kwa nchi zinazoendelea, mapokeo ya siku hiyo yalishamiri mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa namna tofauti ya usherehekeaji, ambapo wengi wao walipotosha kabisa maana ya Siku ya Wapendanao na kuifanya siku ya mapenzi ya wawili zaidi. Wapo walioadhimisha siku hii baharini kwenye meli kubwa ya kifahari.

Ingawa mwanzo wa siku hii ni muungano wa vijana wawili wa jinsia tofauti, walio tayari kuungana katika maisha yao yote kuunganishwa katika ndoa, kwetu imekuwa ni kubakana, huku tamaa na kutaka kuonekana wa kisasa zaidi vikitawala.

Washerehekeaji wakuu wa siku hii katika nchi za kimaskini ni vijana hasa walio kwenye balehe. Siku chache kabla ya Februari 14, tembelea maduka ya kadi, maua na zawadi utajionea pilikapilika za vijana wa kike na kiume wakitafuta kadi na zawadi kwa ajili ya wapenzi wao.

Wanasahau kwamba siku hii ni maalumu kwa ajili ya upendo wa kiroho, kuungana na adui zetu, kuombana misamaha, kubadilishana zawadi na kupeana ujumbe na kadi za upendo huku mkisahau mabaya na chuki zilizopita.

Tumeigeuza siku hii na kuifanya kuwa maalumu kwa mavazi na mapambo ya rangi nyekundu. Tumeifanya kuwa siku ya ngono. Wengi huanzisha uhusiano mpya wa kimapenzi na kwa wenye ndoa ndiyo siku ya kutokomea kwenye nyumba ndogo na kwenda kwenye starehe na vimada.

Kwa wazazi makini, hii ni siku ya kufahamu iwapo kijana wako ameanza uhusiano wa kimapenzi ama la, kwa sababu muonekano wa furaha na uchangamfu katika mwili na sura yake utaongezeka.

Aidha, Februari 14 isiwatie ari vijana ya kuingia katika maisha ya ndoa kwa kukulupuka. Si busara kuchochea mapenzi ya Siku ya Valentine kuwa mwanzo wa majuto baada ya kuambukizwa virusi vya ukimwi kwenye ngono zembe.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya mapenzi wameeleza kuwa Siku ya Valentine kwa kiwango kikubwa inaongeza kasi ya maambukizi ya ukimwi mijini na vijijini, hasa kwa vijana wa shule za sekondari.

Ni vema kurudi kwenye mstari. Tujihadhari na tafsiri ovu tuliyoipandikiza vichwani mwetu kuhusu namna ya kuadhimisha siku hii ya muhimu ya kukumbuka matendo mema ya Mtakatifu Valentine.

Tueneze upendo wa kiroho na amani kwa wengine wenye kuhitaji, hasa walemavu, yatima na wazee. Ni siku ya kuwakumbuka waliotengwa, kwa sababu mbalimbali, tuwatembelee wafungwa na kuwapa zawadi.

Ni wakati wa kufanya mabadiliko ya Fikra na sisi wote kuwa mfano wa Mt. Valentine.
 
valentine day ndo imekaribia,
ikiwa ni siku ya wapendanao,ndugu jamaa na marafiki kukaa pamoja,
natoa nafasi kwa atakayejisikia kuwa pamoja nami siku hiyo,
kukaa,kula,kunywa kuongea na ku dance
we ni F AU M?
 
valentine day ndo imekaribia,
ikiwa ni siku ya wapendanao,ndugu jamaa na marafiki kukaa pamoja,
natoa nafasi kwa atakayejisikia kuwa pamoja nami siku hiyo,
kukaa,kula,kunywa kuongea na ku dance
we ni mtamu kweli?
 
Back
Top Bottom