Vat kwenye nyumba za kuishi

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Katika badjeti ya mwaka huu kuna ingizo jipya la VAT kwenye nyumba za kuishi ambapo siku za nyuma ikuwa hamna. Walipaji ni wapangaji .Mnalionje hili wakuu?
 
Ebu fafanua vizuri hiyo kodi analipa nani na kwenye transaction ipi?????
Kwa mtikisiko wa uchumi duniani hata wenye MADANGURO, maCD na maDVD tutawatoza kodi,
 
I think mlipaji ni yule anayepokea toka kwa mpangaji,hebu fikiria yale majengo yote ya masaki yakilipa vat si itakuwa safi.ila sasa kwa kuwa yote ya wakubwa hawatalipa kodi
 
Nilikua nategemea bunge lilipoketi na kamati zake za fedha litangaze sheria ya kufungwa mtu kwa muda wa miaka isiyo pungua kumi bila faini kwa yeyote anaeonekana/ kapatikana na jinai/kapoteza heasbu za kodi au kakwepa kulipa kodi huku akijua fika anafanya biashara bila kulipa kodi.

Kwa nchi Kama Australia, USA ukifanya biashara au ingizo la fedha bila kutoa taarifa zitakuja kuwa za mwizi 40,!wanasitisha huduma yoyote ile iwe ya kibenki au ya kawaida. Kwa maana nyingine ni afadhali upatikane na makosa ya mauaji kwani waweza ukafungwa miaka mitano au saba na kutoka na ukasaidiwa tena na serikali kulikoni ukwepaji wa kodi hilo kila mtu ni adui yako.

Kwa wanaomjua taikuni MADDOF WA USA KAFUNGWA MIAKA 150 KWA KUFANYA MONEY LAUNDERING. HAWA NI AKINA CHENGE MNAOWANEA AIBU.

Bongo lazima tena chondechonde kule Arusha serikali imepoteza mapato yake mengi sana kwenye majengo haswa ya upangishaji. Kwa mfano, hawa UNCTR/Mahakama ya kimataifa wafanyakazi wanapnagishiwa nyumba kwa siyo chini ya dolar 500$ (Hakuna kodi hapo clean money mifukoni mwa watu) kwa mwezi na wameishi Arusha kwa zaidi ya miaka kumi.

Kwa hiyo jama tusimtafute mchawi tulipe kodi wajameni, tena kwa gadhabu.
 
I think mlipaji ni yule anayepokea toka kwa mpangaji,hebu fikiria yale majengo yote ya masaki yakilipa vat si itakuwa safi.ila sasa kwa kuwa yote ya wakubwa hawatalipa kodi

Siku zote mlipa kodi ni MLAJI, wao watakachofanya ni kuweka bei yao na VAT juu, so wewe mlaji ndio utaelemewa na mzigo wakati wao wanaendelea kupaaa
 
Hii ukusanyaji wake utakuwa mgumu kidogo, kuna watu wanakaa kwenye nyumba za kupanga hata huwa hawaonani na mwenye nyumba, huwa wana-deposit kwenye acconut tu. Sasa TRA wataipataje hiyo kodi?
 
Bongo lazima tena chondechonde kule Arusha serikali imepoteza mapato yake mengi sana kwenye majengo haswa ya upangishaji. Kwa mfano, hawa UNCTR/Mahakama ya kimataifa wafanyakazi wanapnagishiwa nyumba kwa siyo chini ya dolar 500$ (Hakuna kodi hapo clean money mifukoni mwa watu) kwa mwezi na wameishi Arusha kwa zaidi ya miaka kumi.

Kwa hiyo jama tusimtafute mchawi tulipe kodi wajameni, tena kwa gadhabu.

Hili la serikali kutotoza kodi ni swala la kisera - kwa sisi wenye mwelekeo wa ki'republican'/conservative/mlengo wa kulia - haya ndiyo mambo tunayopigania. Money laundering ni kitu kingine .. tusichanganye
 
Hili la serikali kutotoza kodi ni swala la kisera - kwa sisi wenye mwelekeo wa ki'republican'/conservative/mlengo wa kulia - haya ndiyo mambo tunayopigania. Money laundering ni kitu kingine .. tusichanganye

Ebu fafanua vizuri hiyo kodi analipa nani na kwenye transaction ipi?????
Kwa mtikisiko wa uchumi duniani hata wenye MADANGURO, maCD na maDVD tutawatoza kodi,

Ina maana ukilipa kodi ya nyumba unaongezwa 18% amabayo ni VAT. Hii haiapply kwa NHC, bali kwa wengine wote. Effect yake ni kwamba kama wewe unafanya kazi na unakaa nyumba ya say BIMA aka NIC utalipa rent ya juu zaidi maana VAT inakuhusu. KWa nyumba za wenyeji sijui lakini habari si ndio hiyo?
 
Last edited:
Kutoza kodi ni mihimu. Lakini jiulize hasa mfanyakazi wa serikali unayepangisha nyumba kwenye estate fulani. Unalipa PAYE kila mwezi, then kila unachonunua unalipa VAT, na mwisho nyumba unalipia tena VAT. HII sio too much taxation kwa mtu mmoja ? Rent ya 200, 000.00 kuanzia Julai 1st inkuwa 236,000 .Hiyo 36,000 ni Vat haimhusu mwenye nyumba. Sasa mwenye nyumba nae akipandisha kodi kutokana na sababu zake tutatishia wapi wajemeni sisi walalahoi wapangaji? Na NHC ambao ndio inawahifadhi wahindi wengi wenye fedha wakiwemo mafisadi mbona wao wasilipe?
 
Hakika hakuna jambo geni katika bajeti ya Tz kuhusiana na kodi za nyumba.
Toka zamani kuna kodi nyingi ambazo mwenye nyumba anapaswa kulipa mara baada ya kupokea kodi yake.
Kuna WITH HOLD TAX ambayo ni 2%ya total amount ya kodi yako pamoja na VAT ambayo ni 20%.

bajeti ya 2009/2010 imeshusha hilo na kufanya VAT kuwa only 18%.

Ila kwa sababu serikali ilikuwa haifuatilii ndio maana engi hawaijui lakin hakuna jipya
 
I beg to differ. Nyumba za biashara tu ndio zilikuwa subjected to VAt. Residential hakuna .Angalia kijitabu cha structure za kodi TRA.
 
Back
Top Bottom