Vasectomy imeniponza: Mke wangu ana mimba ya wajanja, nifanyeje!

ntaanza kufanya DNA test very soon ili niweze kujua 'gravity' ya hii kitu, nahisi nimedhalilishwa sana mbele ya jamii. afadhali ingekuwa sijafanya hiyo operation ingekuwa rahisi kupotezea lakini ni ngumu ktk hali yangu ya sasa.
ukute na hao wengine wote sio wako sijui itakuwaje na ushafyeka production zone una hatari wewe heri usipime
 
Inawezekana pia kukawa na makosa katika hiyo vasectomy waliyokufanyia yaliyosababisha mimba ikatungwa.

kuondoa mashaka nilienda kuhakikisha hilo na nikaambiwa operation iko sawa bin sawia.......so nimemegewa mkuu!
 
Kinachoniuma ni kwamba nilipochukua uamuzi wa kufanya vasectomy, alifurahi sana na kuwaeleza watu jinsi alivyoona kuwa mimi ni responsible husaband. manesi pia walinisifia sana. sasa ghafla wife ana mimba, ntauweka wapi mimi uso wangu jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiii! si afadhali angetumia kinga, walau angenisitiri utu wangu?
Pole sana mkuu.mambo mengine yanataka hekima ya kimungu kutoa ushauri. Isipokuwa usichinje wala kupiga wala kuua. Haitatoa suluhisho lolote kwako na kwa familia yako maana mna watoto wengine tayari. Kama inakuwa ngumu achana naye in such a way that nobody would notice. Hii ni kuwasaidia watoto wakue nao wakayaone ya kwao mbele ya safari.
Mwisho wa yote kabisa, kwanini ulienda kutoa kizazi? That is the last thing I would do!!!
 
kwa hiyo unanishauri na shule nimpeleke na gharama nyingine nitoe as if ni mwanangu huku nikijua sio wangu? Hata kama limbwata hii sasa itakuwa imezidi, loooooooh!

Kuna namna ya kisheria ya kumlea mtoto wa namna hiyo. Inawezekana pia wapo wasio wako katika hao wengine, kawapime DNA kama huna presha ya kupanda.

La msingi hapa ni kuwa wewe una familia, na watoto hawana makosa. Jadiliana na mkeo, mkishindwa kuelewana kuna baraza la usuluhishi la ndoa kanisani/msikitini, ikishindikana ndio mwaweza kumwona mwanasheria kuona nini kifanyike.

Tafadhali, usipaniki, na pia ukumbuke ni JINAI kuchinja mtu. Option zipo nyingi tu mbona? Mkeo si binadamu wa kwanza kuzini, kumbuka pia hilo.
 
ndo maana sasa naona hata kupima DNA inaweza ikaja kuwa yaleyale ya kujimaliza kabla ya wakati..............sijui itakuwaje ntapojua kuwa hata hawa wengine kati yao sio wangu. presha inaweza kuniondoa duniani


Mkuu DNA..! Kwa hii situation ni sawa na kwenda kupima Ngoma after knowing one of your kimeo kimesha R.I.P. Here is where you have to show your Manhood. All the best kaka (I can feel it th way u feel ryt na)
 
Kaka VASECTOMY imekusaidia kujua kuwa mkeo ni kimeo, na pengine watoto ulionao yawezekana si wako. Cheki DNA, kama ndo vile mpige chini bwana, heri ya lawama kuliko fedheha! Utaleaje watoto wa kubambikiwa bila hiari yako halafu wakikua wanamtafuta baba yao
Pole mkuu
 
huyo mwanamke hafai, anauza mechi mpaka nyavu zinatingishwa? na huyo jamaa anayempa huko mtaani atakuona wewe bwooooooooooooooooooooooooooooozooooo!!!!

anyway, ndoa ni yenu wawili, mwite mkeo zungumza nae (hala hala muite ukiwa umetulia na ushashusha jazba), uamuzi wa kusuka au kunyoa upo mikononi mwako
 
kaka yamekukuta ya kufungia mwaka! pole sana,fanya uamuzi baada ya kuhakikisha kua huyo mtoto/mimba sio yako!
 
Mimi Ushauri wangu ni kama ifutavyo:-
1:Jikubali kwamba hilo ndilo tatizo lililokupata..ukiishajikubali utaweza kuyapokea magumu yaliyo mbele yako.
2.Pima hao watoto wotw DNA ili ujue ukweli..kwani usipojua ukweli itakua inazidi kukutesa pale utakapokua unahisi na wengine sio wako.Lakini pia itakusaidia wakati utakapokua una resolve na mke wako, hata kama utajua kuwa wote si wako,lakini ndio ukweli wenyewe na itabaki kuwa hivyo.Penye ukweli uongo hujitenga.Ila wakati wa kupima ukubaliane na lolote litakalo kutokea kwani najua utaumia sana,hasa pale utakapokuta mtoto unaempenda sana ndio sio wako.
3.kaa na mke wako pale utakapoona kichwa chako kimetulia,jua kwanini aliamua kukusaliti maana wakati mwingine haya mambo unapomkera mwenzio anaenda kutafuta tulizo upande mwingine.Lakini pia kuwa tayari kusamehe pale utakapoona uko tayari kuanza nae maisha mapya.
4.Kuwa tayari kukubaliana na matokeo ya maamuzi yako dhidi ya jamii.mf.Unaweza kutaka endelea kuishi nae wakati huohuo unaangalia jamii inayokuzunguka itakuchukuliaje, kumbuka msimamo wako ndio utakaoamua hatma ya maisha yako.Ukifikiria watu wengine watakuonaje unaweza acha kufanya maamuzi sahihi.
5.Fikiria maisha juu ya watoto itakuaje pale utakapoamua kuachana nae.Usije kutengeneza watoto wa mitaani,au majambazi au wasio na maaili wakati ungeweza kuliweka sawa mapema.
6.Kumbuka pia utakapoamua kuanzisha uhusiano mpya unachangamoto ya kuja kukutana na mtu atakayehitaji mtoto,hapo utafanyaje?Itakua ni balaa pengine kuliko hata huyu uliye naye Kwani wahenga walisema"zimwi likujualo..........."
Mtangulze Mungu katika matatizo yako.
Namalizia kwa mfano huu:Kuna mkoa niliwahi kuishi na kukutana na mzee mmoja fundi magari ambaye ni darasa la saba tu:Yule mzee mke wake alijifungua mtoto wa kiarabu na kumuka yule mzee na mke wake wote ni wabantu.Alimuuliza mara kadhaa mke wake huyu mtoto ni wanani?mke akang'ang'ania ni wa huyo jamaa.Basi jamaa akakubali yaishe.
Sasa si unajua watu wakaanza chokochoko zao kuwa yule mtoto si wake.Yule mzee akawa anawaambia kuwa ni wake.na kama kuna bab wa huyo mtoto ajitokeze..hadi leo hii nakuambia yule mzee yuko na huyo binti wake muarabu na keshaolewa, na anajua yeye ni baba yake.
alitumia busara ndogo tu ya kuto kuharibu maisha ya watoto wote kwa sababu ya huyo mmoja.

Mwisho wa siku wewe ndio muamuzi.Pole kwa gazeti sikua na nia ya kukuchosha,ila ni katika kutoa mchango wa mawazo.;
 
Pokola: Kwa sheria ya Tanzania Ndoa ya Tanzania (1971) mojawapo ya sababu zinazoweza kupelekea ndoa kuwa 'irreparably broken down' na mahakama kutoa talaka ni uzinzi (adultely) ya mwanandoa mmoja. Na ukigundua mimba si yako huo ni ushahidi kuwa mkeo alitoka nje ya ndoa na kisheria waweza kwenda mahakamani kuomba 'separation' au 'divorce'. am out

Si kweli MKA.

Kuna hatua ZA LAZIMA za kufuata, kabla ya separation/divorce, eg. exhaustion of all other possible avenues, eg. marriage conciliatory bodies within the church/mosque. Si rahisi sana kuvunja ndoa.

Na pia swali la msingi ni: Nini kitawatokea watoto baada ya separation/divorce decree ya mahakama? Jibu ni rahisi tu: WATOTO WOTE NI SAWA, HAKUNA MTOTO HARAMU (bastard) TANZANIA, tofauti na nchi nyingine za commonwealth. Back to square 1!!

Huyu mwenzetu anahitaji ushauri, si ushabiki. Sawa Mka? Haika maee!!
 
Hapo tu ndio panapokuponza...

Kuna mwalimu mmoja alikuwa anatumia lugha kali sana inapotokea jambo kama hili. Alipenda kusema kuwa..."unalipa matunda ya uungwana au ushenzi wako"!!

Kwa hili huna ujanja kwa sababu wewe mwenyewe uliamua kuivunja armoury yako. Mwambie akuonee huruma. Hebu bembeleza wife na kumweleza kuwa hiyo idadi inatosha,......Vinginevyo KITANDA KITAENDELEA KUTOZAA HARAMU!!

Pole sana lakini!!

Du! Makubwa!!! Yaani mke aisaliti ndoa then jibaba limpigie magoti wife na kumbembeleza??? I would focus on the kids and let her enjoy her life after all magonjwa nje nje siku hizi.
 
chukua watoto woote kapime dna kama ni wa kwako fukuzia iyo mama mbali baki na watoto wako muanze maisha upya,mwanamke gani anaenda kucheza nje tena ngono zembe ? Kimbiza mwizi meeeeeeeeeeeeeen
 
Hapa mzazi akizaa tu nae zamu yake akakate mirija huna jinsi hapo we elea tu mimba ya mme mwenzio au mlazimishe atoe inauma sana.
 
Dah, ndugu yangu mwaka wa balaa ni balaa tu! Pamoja na vitimbi vyote vya 2011 vya umeme,katiba mpya,jairo,ngeleja bado shemeji kaongeza na cha kwake?...inauma sana. Hiyo ndo mitihan ya maisha mkuu. Pata utulivu utafakari kwa kina ushauri utakao pewa.hata ukijua leo kuwa watoto baadhi si wako,haitakusaidia la msingi kumbuka smile walizokuwa wakitoa kwako wakiwa wadogo huku ww ukiamin ni watoto wako.najua inachanganya sana lakini mwisho wa siku huwa ukweli na maridhiano ndo tiba ya kweli.tulia,kaa na ongea naye
 
yaani nashangaa kujua kuwa kumbe hata kwa wanaume mkikumbwa na masahibu ya mahusiano mnakua na njia panda ya maamuzi?! sasa nakubaliana na kaka yangu moskwito, there is no easy way anyhow!
kama tulivyo wanawake wengi, mawazo ya kuwa watanionaje, itakuaje etc yapo tu. lakini cha ajabu zaidi ni kua uliamua kufanya vasectomy na kuuambia umma wote? mambo yenu ya ndoa mnashare na watu wangapi? kama unawaonea aibu manesi waliokupongeza, hameni hosp. hongera kwa kutegemea mtoto wa 9.
Kinachoniuma ni kwamba nilipochukua uamuzi wa kufanya vasectomy, alifurahi sana na kuwaeleza watu jinsi alivyoona kuwa mimi ni responsible husaband. manesi pia walinisifia sana. sasa ghafla wife ana mimba, ntauweka wapi mimi uso wangu jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiii! si afadhali angetumia kinga, walau angenisitiri utu wangu?
 
Back
Top Bottom