Vasco aaga tena: Baada ya Saudia, maneno Botswana

..safu ya viongozi kwenda kuaga msafara, kisha safu ya viongozi kwenda kupokea msafara!

...hili liinchi linazalisha nini cha kutufanya tuweze kutumbua namna hii hizi pesa za kujiombeleza kila kukicha?!!

Niliongelea hii kwenye thread moja wiki iliyopita, hawa jamaa kwanza hawana kazi? Membe na hao wengine wote wanafanya nini hapo? na kila mmoja ameenda hapo na msafara wa magari, nchi hii sio masikini hata kidogo, inawezekana ni masikini wa viongozi wenye fikra sahihi, and we seem to loose the plot every time.
 
Mimi mwenyewe sizifahamu hizo protocal, lakini nauliza kwa kufikirika ulidhani safu ya kumsindikiza raisi iwaje! kwa muono wako wewe!
 
Mimi mwenyewe sizifahamu hizo protocal, lakini nauliza kwa kufikirika ulidhani safu ya kumsindikiza raisi iwaje! kwa muono wako wewe!

PH, muono wangu katika hili ni kama ifuatavyo:

--- Katika kurekebisha hiyo protocol ya kulakiana, kiongozi mmoja wa ngazi ya juu anatosha kabisa. Hii ni katika kupunguza gharama, pia kwa namna fulani kubadilika ili kwenda na wakati iwapo hizi protocol zimekuwepo miaka nenda rudi, kunafika wakati ni muhimu kuzirekebisha.
 
...Hakiyanani tena hii misafara ya Rais wetu, haswa hizi protocol zilizopitwa na wakati zinauzi mpaka basi tu... i get so angry i wish the whole gadayym thing could just blow up into ashes tujue moja.

...halafu hicho kindege wamekifanya kama AirforceONE! kinaparamia kila bara kila nchi utafikiri ni cha nchi inayozalisha mafuta!

I know, halafu angalau basi angekuwa anasafiri mwenyewe, lakini ki Air Bajaji wanaki overload utafikiri pantoni la Kigamboni. Kikipotelea vichakani siku moja tunasema oooh kimetunguliwa na makaburu. Mola pishia mbali.

Na mimi nina hasira na hii misafara ya kwenda kumpokea Rais. Hivi ni kwa nini wanadhani ni muhimu kumpokea?

Karibia theluthi moja ya bajeti yetu ni misaada, lakini kama wangekata gharama kama hizi za kwenda kuagana na kupokeana, kwani tusingeweza kujitegemea kweli?
 
Sangoma wake kamwambia asikae pale Ikulu pana wanga; ndio maana anashinda anavumbua!! IBN Batuta!! Kutawala kwa kupiga lamli kuna matatizo yake!!
 
I know, halafu angalau basi angekuwa anasafiri mwenyewe, lakini ki Air Bajaji wanaki overload utafikiri pantoni la Kigamboni. Kikipotelea vichakani siku moja tunasema oooh kimetunguliwa na makaburu. Mola pishia mbali.

Na mimi nina hasira na hii misafara ya kwenda kumpokea Rais. Hivi ni kwa nini wanadhani ni muhimu kumpokea?

Karibia theluthi moja ya bajeti yetu ni misaada, lakini kama wangekata gharama kama hizi za kwenda kuagana na kupokeana, kwani tusingeweza kujitegemea kweli?

Nakuunga mkono mia kwa mia
hivi yale mafuta na posho za kujaza wingi pale eapoti hayawezi kutumia kugharimia kununua vitabu vichache hata kwa nursery zetu? (hivi serikali inazo nursery schools kweli?).
Pia angalia suala la kupotezeana muda kusubiri misafara hii ipite ambapo WALIPA KODI wanaokamuliwa kisawasawa wanacheleweshwa kwenye shughuli zao ilhali wanaotumbua kodi hawajali wala kutafuta mbinu za kutatua matatizo yatokanayo na misafara yao.
WIZI MTUPU
nna hasira we acha tu
 
Back
Top Bottom