Varangati manispaa ilala. Walimu wasema uovu wa serikali ya ccm sasa basi

Mpatanishi

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,810
623
Habari zenu wakuu!
Nipo maeneo ya Manispaa Ilala varangati kubwa linaendelea walimu wapya wanadai mishahara yao.

Kama inavyozoeleka serikali hii ovu ya CCM mwaka huu imeamua kuwadhulumu kabisa walimu hawa mishahara yao ya mwezi wa pili.

Tayari walimu wameshaonana na afisa utumishi na majibu aliyotoa ni ubabaishaji mtupu.
Afisa huyo amedai mishahara haitakuwepo kwa mwezi huu kwakua imeshindikana ku scan majina ya walimu kwenye computer na kuyatuma hazina kwa kuwa network ipo slow.

Walimu wamechachamaa wanahoji iweje wenzao wa Mwanza, Mara, Singida wapate halafu wao wa Dar wakose?
Mpaka sasa walimu wapo hapa na wamesema uovu wa serikali ya ccm sasa basi, hawaondoki mpaka kieleweke wameshavamaia ofisi ya mkurugenzi wanamsubiri afike.

Je mishahara ya walimu hawa ndio imetengwa kwa kampeni Arumeru??

Kitakachoendelea nitawajuza.
 
Kwan kuchelewesha mishahara kuna uhusiano gani na CCM hapo? Nafikiri sio vizuri kuitupia lawama CCM hata kwa mambo madogo wasiyoyasababisha wao kwa sababu inawezekana huyo afisa Utumishi mwenyewe ni upinzani
 
Wewe vipi? si sirikali ovu la CCM, au? Serikali inatekeleza sera za CCM, sasa sijui wewe kwa nini huoni uhusiano!
 
Hawataki kugoma wanahudhuri tu darasani kula vumbi. Mpango mzima gomeni
 
Kwan kuchelewesha mishahara kuna uhusiano gani na CCM hapo? Nafikiri sio vizuri kuitupia lawama CCM hata kwa mambo madogo wasiyoyasababisha wao kwa sababu inawezekana huyo afisa Utumishi mwenyewe ni upinzani

Barabara zikijengwa, "tuipongeze serikali ya CCM", watu wakinyimwa haki zao, "tusiilaumu serikali ya CCM"
 
Wapi hii serikari bana, Mwza wengine hawajaperwa mpaka sasaa sijui kuna nini hazna.......

Tulitaka wenyewe kuipa ccm nafasi basi tusilaumu....but every first must end somewhere else....

Hii thread noma!
 
Kwan kuchelewesha mishahara kuna uhusiano gani na CCM hapo? Nafikiri sio vizuri kuitupia lawama CCM hata kwa mambo madogo wasiyoyasababisha wao kwa sababu inawezekana huyo afisa Utumishi mwenyewe ni upinzani

Serikali iliyopo madarakani ni ya chama gani ndugu yangu?
 
Wadau hii ni fedheha kwa kada hii. Serikali walipeni walimu wawe na moyo wa kufundisha vijana wetu.
 
Nasikia ni makusanyo ya kampeni hayo...unadhani skafu,kanga,t-shirt,misosi inaokotwa? Nawashukuru sana hawa walimu,lakini hii ni kazi nzuri ya CDM kutoa elimu ya urai,zamani hizo ungekuta wanakaa kimya mpaka unakuta wanakufa kwa njaa.
 
eti kuscan,network slow,mara computer haioni jina lako si apeleke hardcopy wizarani!namna hii tutajenga kweli flyovers?
 
Nasikia ni makusanyo ya kampeni hayo...unadhani skafu,kanga,t-shirt,misosi inaokotwa? Nawashukuru sana hawa walimu,lakini hii ni kazi nzuri ya CDM kutoa elimu ya urai,zamani hizo ungekuta wanakaa kimya mpaka unakuta wanakufa kwa njaa.

walimu wa mwaka huu ni wanaojitambua mkuu! Mwaka huu serikali ikae chonjo.
 
Kwan kuchelewesha mishahara kuna uhusiano gani na CCM hapo? Nafikiri sio vizuri kuitupia lawama CCM hata kwa mambo madogo wasiyoyasababisha wao kwa sababu inawezekana huyo afisa Utumishi mwenyewe ni upinzani

kama huwezi kuconnect hili tatizo na chama tawala basi unahitaji msaada maalum, utafutiwe hata tuition nadhan utakuwa msaada mzuri wa kukunusuru na hali uliyonayo!
 
Kuna tatizo gani serikalini? Kila wilaya walimu wanalalamika kutopata mishahara!
 
Back
Top Bottom