FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,792
- 5,374
Upendo ni tabia halisi ya Mungu inyodhihirishwa kwetu sisi siku zote, na haikuanza leo ilianza toka kuwekwa misingi ya ulimwengu. Imeandikwa, mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote pia mpende jirani yako kama nafsi yako, juu ya hayo hakuna hukumu. Pia imeandikwa ITAKUFAA NINI KAMA TUKIWAPENDA WALE WATUPENDAO TU? WAPENDENI ADUI ZENU NA KUWAOMBEA, KUWABARIKI TENA MSILAANI, kwani mfanyapo hayo mwawapalia makaa ya moto kichwani pao, ADUI YAKO AKIWA NA NJAA WEWE MNYWESHE, AKIWA NA NJAA WEWE MLISHE.
>>>Sisi tumepata kujua upendo ni nini, kwani Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Nasi vilevile tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu.
>>>>>Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo.
Upendo
Happy Valentine day to you all
FL

- Haujivuni
- Hauhesabu makosa
- Huvumilia yote
- Hauna nyakati
- Ni kwa wote
- Hudumu nk
Happy Valentine day to you all
FL