V.Nyerere akataa kuchangia Mafuta ya Mwenge

Mzalendo80

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
2,508
1,338
Nyerere: wafungwa wafundishe Sekondari za kata Send to a friend
Monday, 27 June 2011 08:53
0diggsdigg

Hussein Issa

KUTOKANA na uhaba wa walimu nchini, serikali imeshauriwa kuwatumia walimu waliopo magerezani kufundisha shule mbalimbali hususan za kata, ikiwa ni sehemu mojawapo ya adhabu yao.

Akizungumza Bungeni wiki iliyopita, Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vincent Nyerere, alisema walimu hao wanatakiwa kutumika kufundisha shule zilizopo karibu na magereza kwa sababu hazina walimu wa kutosha.
Nyerere alisema magerezani kuna walimu wengi wamefungwa, lakini serikali haiwatumii vyema badala yake inawapa adhabu ya kukata miti ovyo, ambayo ingetumika kutengenezea hata madawati.

Alisema walimu hao walioko magerezani wanatakiwa kupelekwa shuleni kufundisha shule za kata na wakimaliza muda wao, wanarudi gerezani kama kawaida kutumikia kifungo chao kama wengine.
Alisema shule za kata siyo za watoto wa wakubwa, bali wazazi maskini ndiyo maana haziendelei na hazitaendelea hata siku moja.
“Hapa Bungeni nina imani hakuna hata mzazi mmoja ambaye mwanaye anasoma shule za kata, hii inatokana na nini hasa zina wenyewe ambao ni walalahoi,” alisema Nyerere.

Pia, alisema haoni sababu za kuchangia mafuta ya mwenge wa Uhuru kutokana na faida yake kutoonekana.
Alisema fedha ambazo zinachangishwa kwa ajili ya mwenge ni nyingi, zinatoka kwa wananchi ambazo zingetumika vizuri maendeleo ya nchi yangekua.

“Waliwahi kuja kwangu kunichangisha fedha za mafuta ya mwenge, nikawaambia twendeni nikawawekee mafuta kituo cha mafuta, wakasema wanataka fedha siyo mafuta nikawafukuza,” alisema Nyerere.

Alisema kuchangia mwenge ni sehemu ya ufisadi, kwani hakuna mantiki yoyote ya kuzungusha mwenge nchi nzima kwa sababu tayari umepoteza mwelekeo badala ya kupiga vita mafisadi unachochea.

Alisema Mwenge unatakiwa kutumika vizuri kuibua maovu ya viongozi, siyo kuwamulikia taa mafisadi ili waendelee kutafuna nchi vizuri. “Huu ni muda wa kuwafichua mafisadi siyo kuwamulika ili waone mbele kuna nini na kuendelea kuitafuna nchi vizuri,” alisema

Source: Mwananchi

naomba mwongozo....je,kwa ground ipi mimi kama mwananchi wa kwawaida ninaweza kukataa kuchangia mafuta ya Mwenge? sioni essence yake lakini sijapata bado sababu madhubuti za kukataa nitakapoombwa kufanya huvyo.
 
Mpaka leo na dakika hii na utu uzima wangu sijui umuhimu na sababu za kuzungusha na kukimbiza mwenge .Naona ni ufisdi na unasambaza ukimwi zaidi na umsikini kuliko lengo lililowekwa mzee nyerere,wapeleke tu nyumba ya makumbusho
 
nakubaliana na wazo la daffi, uwekwe makumbusho na siku za sherehe za uhuru uwe unapelekwa uwanjani kama kumbukumbu tu kama wanaupenda sana.
 
Wazo lake kuhusu walimu wafungwa limenifurahisha. Ni ubunifu wa aina yake.

Mbopo umeona vichwa hivyo huko Chadema? Yes wafungwa kama wapo na uwezo huo waacheni wafundishe wakitumia adhabu yao kuna kosa gani ?Mweng mie siutaki hata kuusikia kabisa .
 
Mbopo umeona vichwa hivyo huko Chadema? Yes wafungwa kama wapo na uwezo huo waacheni wafundishe wakitumia adhabu yao kuna kosa gani ?Mweng mie siutaki hata kuusikia kabisa .

Sasa mbona unanisuta mimi as if mie nimepinga. Tunachosema ni kwamba kuna wabunge wazuri sana ndani ya Chadema na mawazo yao ni chanya na yenye muelekeo wa maendeleo. Hivyo hivyo kuna wabunge ndani ya CCM ambao hawana sifa za kuwa wabunge kwa ufahamu na misimamo yao. Lakini staki stereotype za kudhani kwamba kila mtu Chadema ni safi na kwamba kila mtu CCM ni mbaya. Kote kuna vichwa na makapi kutegemeana na suala lililopo. But I have really appreciated Nyerere's proposal. I wonder kama Lema naye anawaza hivi au yuko bize kuandaa maandamano.
 
Mhhh ili la wafungwa kufundisha watoto napata shida kidogo, kwa wanafunzi walimu ni role model
 
Mhhh ili la wafungwa kufundisha watoto napata shida kidogo, kwa wanafunzi walimu ni role model
Mkuu kumbuka kuna baadhi ya wafungwa wana ujuzi fulani,nachofikiri alikuwa anaongelea wafungwa ambao walikuwa walimu kabla ya vifungo vyao!!
 
Huu mwenge naona hauzungushwi kwa lia ya kuhamasisha maendeleo bali ni sehemu ya chama tawala kuendelea kujitafutia umaarufu kwa watu ili wawatafutie ajira zisizo rasmi. Jiulize ni mamilioni mangapi yanaenda kwenye posho na mafuta ya watembeza mwenge kama hiyo pesa ingechangishwa na kubaki ndani ya kata au kijiji ni shule ngapi na zahanati zingejengwa?
 
naomba mwongozo....je,kwa ground ipi mimi kama mwananchi wa kwawaida ninaweza kukataa kuchangia mafuta ya Mwenge? sioni essence yake lakini sijapata bado sababu madhubuti za kukataa nitakapoombwa kufanya huvyo.

Kwani
kuchangia mafuta ya mwenge ni lazima, huo mwenge unamanufaa gani, huo ni ushenzi wa ccm. tukipata chama kimpya ukazikwe baharini kama nani yule?
 
.. ndani yake kuna tambiko la kimila. Ni la kuwafanya watanganyika makondoo. Ndiyooooo! siyooooooo! Ipiteeeeee! Na
 
Wazo la mbunge hilo,yaani inashangaza kuwa mbunge anaweza kulihutubia taifa bila kujiandaa sababu anaonyesha kuwa hata hafahamu kuwa takwimu za mwisho wa mwaka jana zinaonyesha kuwa zaidi ya 80% ya walimu wanaofungwa huukumiwa kwa makosa yaliyo kinyume kabisa na taaluma ya ualimu.Je mheshimiwa huyu anataka kusema kuwa hata walio na taaluma mbovu ya ualimu wakafundishee????
 
Mhhh ili la wafungwa kufundisha watoto napata shida kidogo, kwa wanafunzi walimu ni role model

Sioni tatizo kwa sababu kuna wafungwa ambao makosa waliyotiwa nayo hatiani hayahusiani na maadili. Kikubwa hapo ni kamba watakuwa wanafundisha wanafunzi masuala ya kitaaluma na hilo mimi sioni kama ni tatizo.
 
Wazo la mbunge hilo,yaani inashangaza kuwa mbunge anaweza kulihutubia taifa bila kujiandaa sababu anaonyesha kuwa hata hafahamu kuwa takwimu za mwisho wa mwaka jana zinaonyesha kuwa zaidi ya 80% ya walimu wanaofungwa huukumiwa kwa makosa yaliyo kinyume kabisa na taaluma ya ualimu.Je mheshimiwa huyu anataka kusema kuwa hata walio na taaluma mbovu ya ualimu wakafundishee????

mbona ISMAIL ADEN RAGE NI MFUNGWA lakini yuko bungeni?
 
Back
Top Bottom