Uzuri/urembo/utanashati. Vs Jamii

AshaDii nimekumiss
Ok ok kwenye mada utanashati na muonekano wako una mengi sana. Unaweza kukupa kazi ambayo hukuitarajia na ukakutana na bahati ambazo hukuzitarajia na muonekano wako na watu wanavyokuchukulia inakuwa tofauti kidogo. Kuna kazi ambazo bila usmart watu wanakuona hamnazo hata kukuamini na kukupa kazi inakuwa ni issue. Mfano ni wazi kuwa kazi niliyo nayo moja ya kigezo kilikuw ani namna unavyoonekana na vaa yako

Mr R AshaDii Missed you too...

Nimependa maelezo yako... ila tu yameishia njiani, ndio yameeleweka
But would like to know in connection na kazi unayo fanya... ni jinisi gani
ulitakiwa uvae, na je did you have an advantage of knowing before the interview??
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa anaenda kwenye "intavyuu"njiani akiwahi gari lilimwagia maji akachafuka lakini hakurudi kubadili nguo,akafika muda muafaka alipoitwa akaingia,wakamuuliza kulikoni akasema nimemwagiwa as long as nguo na uvaaji wangu has nothing to do with hiki ninachofanya hapa bali ufahamu wangu sikuona haja ya kurudi kubadili nguo,huyu jamaa alipata kazi na ni mchapakazi mzuri sana!
 
Halafu tusisahau jamani
kuna watu wamezaliwa na personality,wako presentable hivi
hata akivaa kawaida anatisha....

Wengine duh.....acha tu.....
Kuna ofisi ukivaa sana,bosi anaku mind..lo
l
Boss usitake nikuletee visa kibao kutokana na hapo kwenye bluu
 
Mentor I Love your share of experience... i can't comprehend nini kilifuata hapo...
yaani wewe uloepukiwa kiti... hio confidence ina rise to the maximum, alokuepukia
inashuka to the minimum.... And i like the fact kua wewe umejiwekea kupendeza kua
Personal ID yako... Mimi ninachoo amini ni kua - kupendeza kweli kunaenda pia na hali ya
fedha ya mtu.... pamaba atazopiga, hali aloacha home (kumfanya awe na amani...)
na the like....

Vipi naomba unijibu.... Is it right sasa quality ya kuhudumia basing on looks??

Hiyo hali ya kifedha unayoongelea ni ipi!?? Nijuavyo, as long as unao uwezo wa kununua nguo, hata kama ya mtumba, basi uamuzi wa kupendeza au kutokupendeza uko mikononi mwako. Hujaona mtu ana shati moja lakini kila ukimwona unatabasamu kwa jinsi alivyopendeza na msafi? Mama yangu mpaka kesho anatuambiaga baba alikuwa na shati moja tu (Sekondari pale Azania mama akiwa Jangwani), lakini he was always smart and clean kuliko wale wenye minguo lukuki na mizuri.

Looks: Hii kitu ni internally triggered and most times involuntary! Yaani kama mimi hapa ofisini akija dada wa HR ama accounts (wale wanakuaga wazuri n smart..sijui kwa nini!) ana shida..basi huduma yake inakuwa fast sana! aje mkaka wa ..., wai! hata speed inapungua...sijui kweli ni kwanini!
Maybe siyo sahihi lakini pia sidhani kama inaepukika!

Moja kati ya tabia za kijinga kabisa za mwanadamu ni hii,kuweka makundi,mzuri,mbaya,jambo hili linamfanya mwanadamu safari yake ya kujitambua iwe ndefu sana,chanzo chake ni kujitafuta na kibaya zaidi anajitafuta nje yake,thamani ya mwanadamu ipo ndani wala sio nje,haya mambo ya kuwagroup watu ni matatizo ya kimalezi na roho mbaya ya mwanadamu,tunashindwa kujipenda wenyewe tunatafuta jambo hilo kwa wengine,bahati mbaya nao wanahitaji upendo kwetu kwani nao hawana!!

Eiyer my brother... ni wazi na ni suala lisilopingika kua kweli morality katika jamii inashuka na kwamba watu wametoa kabisa utu katika kumuangalia mtu au kumdefine.... Ndio maana (kama alivyogusia CPU katika post # 6) watu wazuri barabarani... Perfect personality but kwake utachoka... Aibu... Hata hivyo kujua hilo bado hali epushi watu/wahudumu kutoa favoritism basing on Uzuri, Urembo na Utanashati...

Dada umezungumza matatizo haya lakini hujaonesha kupinga kama ulivyoonesha kukubali kuwa kuna wazuri na wabaya!Sikulaumu kwani hayo ni matatizo makubwa ya kijamiiKiuhalisia hakuna wazuri wala wabaya ndicho ninachoamini!

Eiyer what i was trying to do ni kuonesha hali halisi ilivyo na jinsi nilivyo observe vile ilivyo.... Sio kwamba na support... Ndiio maana swali langu kubwa ni kua yule ambae yupo katika disadvantage akijikuta katika hio hali afanyeje??
 
Halafu tusisahau jamani
kuna watu wamezaliwa na personality,wako presentable hivi
hata akivaa kawaida anatisha....

Wengine duh.....acha tu.....
Kuna ofisi ukivaa sana,bosi anaku mind..lol

100% Reciprocated.... That is a definition of my Mother...
 
Thanx kwa thread nzuri, yenye mvuto katika Akili yangu mkuu Ashadii. Nakubaliana nawe kuwa Uzuri,Urembo na Utanashati unahusika sana ktk shughuri, mambo na michakato yetu ya kila siku kuhusu maisha. Utanashati mara nyingi huwa na faida kwa mlengwa. Sote twatambua kuwa mtu asiye mtanashati (asiyejipenda/wa hovyo) hutiliwa hofu na mashaka, swala la kuaminika huwa ni dogo kwao. Mfano: Mwizi, kichaa, mwehu, mchafu, mzembe, asiyejipenda huwa hawakubaliki machoni mwa watu. Mwizi ajiwekapo nadhifu/msafi uwezekano wa yeye kufanikiwa ktk wizi wake ni mkubwa! Utanashati unahusika!
 
Mr R AshaDii Missed you too...

Nimependa maelezo yako... ila tu yameishia njiani, ndio yameeleweka
But would like to know in connection na kazi unayo fanya... ni jinisi gani
ulitakiwa uvae, na je did you have an advantage of knowing before the interview??

AshaDii senkyou sana sana for missing me
Kiukweli we had a chance to know before kuwa tunatakiwa tuwe smart sana wakati tunaenda kwenye interview na haikuwa official interview ila tuliambiwa kabla kuwa moja ya kigezo cha kupata kazi ni kuwa smart kuanzia mavazi na muonekano wako

So kiukweli usmart una mambo mengi ya faida na hasara kwani kuwa smart jamii inakucchukulia kivingine na inakuheshimu kutokana na usmart wako hata kwenye matukio yoyote yanayotokea muonekano wako una maana kubwa sana.
Jamii inakuchukulia kuwa unajiheshimu kwa namna utakavyoonekana na kuvaa

So ni bora kuwa na muonekano wa kuwa smart katika yote unayofanya
 
Hiyo hali ya kifedha unayoongelea ni ipi!?? Nijuavyo, as long as unao uwezo wa kununua nguo, hata kama ya mtumba, basi uamuzi wa kupendeza au kutokupendeza uko mikononi mwako. Hujaona mtu ana shati moja lakini kila ukimwona unatabasamu kwa jinsi alivyopendeza na msafi? Mama yangu mpaka kesho anatuambiaga baba alikuwa na shati moja tu (Sekondari pale Azania mama akiwa Jangwani), lakini he was always smart and clean kuliko wale wenye minguo lukuki na mizuri.

Hapo nilo bold... it is not always that simple.... kama ilivyo wazi kuna watu wana pesa ndefu hawewezi kuvaa.... can you imagine that type of person hana pesa?? IMO uvaaji unakua disaster....

Looks: Hii kitu ni internally triggered and most times involuntary! Yaani kama mimi hapa ofisini akija dada wa HR ama accounts (wale wanakuaga wazuri n smart..sijui kwa nini!) ana shida..basi huduma yake inakuwa fast sana! aje mkaka wa ..., wai! hata speed inapungua...sijui kweli ni kwanini!
Maybe siyo sahihi lakini pia sidhani kama inaepukika!

I do agree with a great part of this post.... But not neccessarily so abouit LOOKS for sometimes that can be bought and a person can be completely transformed from the original self.... Huyu dada in the same situation anaweza kua treated tofauti....

Attachments

  • beforeAfter_3.jpg
    beforeAfter_3.jpg
    33.2 KB · Views: 78
Okay dada but ulitakiwa uoneshe namna unavyolipinga suala hilo,tatizo ni kuwa matatizo tuliyonayo leo ni kutokana na kujitafuta kwa mwanadamu hata baadhi ya imani zilizopo leo ni matokeo hayo,kama kweli tunataka dunia iwe mahali pazuri pa kuishi ni lazima turudi kwenye uhalisia wa maisha yetu!
 
Habari zenu JF Ladies and Gentlemen.....

From my perspective and experiences mbali mbali katika maeneo mbali mbali nime observe saana hili suala la Uzuri/Urembo/Utanashati unavyochukua nafasi kubwa saana katika kupata huduma mbali mbali katika jamii – yaani ni kwamba tunapotembelea/tembelewa katika office, organizations, groups, institutions mbali mbali the way wewe personally unaonekana ndio itayo pelekea aina ya huduma na mapokezi utayopata…

Uzuri/Urembo ama utanashati ni kitu cha kwanza kabisa kua considered… then inafuata hali yako ya kifedha.. kama mbaya ama nzuri…. (hii haraka haraka – inakua skimmed kwa jicho ikipimwa na posture kama ipo confident, simu uloshika, hair style, viatu… n.k) Hii tabia hasa mijini inakua kwa kasi mno, mkionana na mtu mara ya kwanza anazingatia kwanza how you look, then nguo ulizovaa (assumed thamani) sometimes hata kama umekuja na usafiri… Then maybe ongea yako… Local?? Sophiscated?? Ordinary?? Accent?? – it is not fair BUT the truth…

Kwa Mfano…

Kunaweza kukawa watu wanahudumiwa hapo … na mhudumu awe wa kike au wa kiume akawa na attitude kama vile anavo toa huduma kwa wahusika ni kama anawafanyia favour (hali ni wazi ndio kazi inayomuweka mjini…) – Hapo hapo akaja (acha mtu anaemfahamu…. ) mdada mrembo/mzuri OR mkaka mtanashati/mzuri – Sura yoote na attitude ikabadilika ghafla kwa tabasamu ulovamia sura yake ghafla!!!...Na amini usiamini huja yenyewe inevitably…

Hata hivyo sio katika huduma peke yake…

Hili suala ni chronic hata katika maeneo ya kazi.. huchangia mtu kupata kazi.. ama kupanda cheo… ama kubebwa bebwa na maboss kisa tu uzuri wake unawa changanya n.k.. Mfano Mzuri nina wabunge wawili wadada nafahamu kwa karibu kwa first names basis… (alafu woote ni singles..) hawa wadada, ni mfano mzuri saaana wa walochaguliwa sababu ya Urembo/Uzuri – but infact hakuna kitu wanaweza kufanya… Sad… Mmoja alishinda uchaguzi wa ubunge jimbo Fulani – wakati wa kampeni hajawahi hata enda eneo husika kujinadi…

Hii issue ni kitu ambacho watu wengi hatupendi kufanyiwa… huku cha ajabu ukute na sie hufanya hivo hivo katika maeneo yetu ya kujidaia…. Sina maana kua ni sehemu zoote ama watu woote… Lah! Ila ni most of the maeneo/wahudumiaji….

Ombi Kwenu wana JF…
  1. Naomba tujaribu jadili nini hasa chaweza changia kumpandisha alie Mzuri/Mrembo/Mtanashati.. kuhudumiwa haraka, kupendelewa/kubebwa ama kuthaminiwa hali hicho ambacho anakua favoured hata Yule ambae sio Mzuri/Mrembo/Mtanashati anaweza provide…
  2. Ikiwezekana tushee experience mbali mbali katika maeneo/insitituions mbali mbali ili kupata picha kamili ya sula zima liko kwa kiasi gani….
  3. Mtu unapojikuta katika hio hali ya kunyanyapaliwa…. Ufanye nini??

Natanguliza Shukrani…

Pamoja Saaana…

AshaDii (ADI)

Uko sahihi ADI, mimi huwa ninapotembelea ofc za watu lazima nijiweke extra presentabo, Hii ipo sehemu nyingi sana kama sio zote. Hata getiti walinzi watakupitisha haraka na mawsali ya maana zaidi kulingana na uvaaji wako...nk nk
 
Thanx kwa thread nzuri, yenye mvuto katika Akili yangu mkuu Ashadii. Nakubaliana nawe kuwa Uzuri,Urembo na Utanashati unahusika sana ktk shughuri, mambo na michakato yetu ya kila siku kuhusu maisha. Utanashati mara nyingi huwa na faida kwa mlengwa. Sote twatambua kuwa mtu asiye mtanashati (asiyejipenda/wa hovyo) hutiliwa hofu na mashaka, swala la kuaminika huwa ni dogo kwao. Mfano: Mwizi, kichaa, mwehu, mchafu, mzembe, asiyejipenda huwa hawakubaliki machoni mwa watu. Mwizi ajiwekapo nadhifu/msafi uwezekano wa yeye kufanikiwa ktk wizi wake ni mkubwa! Utanashati unahusika!

Asante Gagurito for the acknowledgement.... Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na maneno yako... lakini hata hiyo hio mifano mitatu kidogo iko extreme... hao sijalenga kabisa maana ni evident... ila hio ya Mzembe na mchafu hapo tuko pamoja... waweza kuta mwingine kavaa nguo nzuri lakini haijapasiwa...(na huu umeme ndio issue kabisa!)... mwingine kavaa kiatu vizuri but kina tope lililoganda toka mvua zinyeshe last time and the like, au mwingine kweli vimenyooshwa na ni visafi but... kucha chafu! au nywele rough... yaani ilimradi tu!
 
AshaDii senkyou sana sana for missing me
Kiukweli we had a chance to know before kuwa tunatakiwa tuwe smart sana wakati tunaenda kwenye interview na haikuwa official interview ila tuliambiwa kabla kuwa moja ya kigezo cha kupata kazi ni kuwa smart kuanzia mavazi na muonekano wako

So kiukweli usmart una mambo mengi ya faida na hasara kwani kuwa smart jamii inakucchukulia kivingine na inakuheshimu kutokana na usmart wako hata kwenye matukio yoyote yanayotokea muonekano wako una maana kubwa sana.
Jamii inakuchukulia kuwa unajiheshimu kwa namna utakavyoonekana na kuvaa

So ni bora kuwa na muonekano wa kuwa smart katika yote unayofanya

Mr R... your experience umetoa i believe itakua very helpful kwa woote wataobahatika kupitia...

Thank you for sharing.... and alll is NOTED.... With appreciation....
 
Asante Gagurito for the acknowledgement.... Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na maneno yako... lakini hata hiyo hio mifano mitatu kidogo iko extreme... hao sijalenga kabisa maana ni evident... ila hio ya Mzembe na mchafu hapo tuko pamoja... waweza kuta mwingine kavaa nguo nzuri lakini haijapasiwa...(na huu umeme ndio issue kabisa!)... mwingine kavaa kiatu vizuri but kina tope lililoganda toka mvua zinyeshe last time and the like, au mwingine kweli vimenyooshwa na ni visafi but... kucha chafu! au nywele rough... yaani ilimradi tu!
Ooh! Nimekupata vizuri sasa Ashadi! hebu ngoja nipange hoja ntarudi ikudadavua hoja vizuri best. ntataka kujikita zaidi na Uzuri na Urembo zaidi.
 
Okay dada but ulitakiwa uoneshe namna unavyolipinga suala hilo,tatizo ni kuwa matatizo tuliyonayo leo ni kutokana na kujitafuta kwa mwanadamu hata baadhi ya imani zilizopo leo ni matokeo hayo,kama kweli tunataka dunia iwe mahali pazuri pa kuishi ni lazima turudi kwenye uhalisia wa maisha yetu!

Nakubaliana nawe kaka.... But genuinely kuna mahala nimeonesha na support???
 
Uko sahihi ADI, mimi huwa ninapotembelea ofc za watu lazima nijiweke extra presentabo, Hii ipo sehemu nyingi sana kama sio zote. Hata getiti walinzi watakupitisha haraka na mawsali ya maana zaidi kulingana na uvaaji wako...nk nk

ha ha ha..... Hapo juu umenifurahisha kweli.... umenikumbusha ile hali unatoka ofisini,
then ulie nae anakuuliza ume park wapi? hali umekuja kwa miguu wala hata sio tax....lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom