Uzoefu wangu kuhusu faida za Tembo Card VISA na MASTER CARD

Mtu Mzima

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
394
124
Mimi ni mteja wa benki inayotoa card za Tembo card VISA na Master Card.

Nimekuwa mteja wa benki hiyo kwa kipindi kirefu tangu enzi hizo tukiwa tunatumia tembo card ya kawaida.

Baada ya wateja wote kulazimishwa kuwa na tembo card ya VISA au MASTERCARD mimi pia nilibadilisha na kupata Tembocard Visa.

Baada ya kusoma matangazo kwenye tovuti yao kuhusu matumizi ya kadi hizo mpya nikavutiwa kutumia huduma hasa ya online shopping.
Huduma nyingine za kuvutia zilizoorodheshwa ni hizi.

TemboCardMasterCard

Features

With TemboCardMasterCard you can have access to your account 24 hours a day whenever and wherever.

Withdraw cash at more than 1 million ATM’s globally
Make purchase at more than 30 million merchants where MasterCard is accepted
Pay recurring bills
Shop world wide
You can track your expenses as your CRDB Bank account will have the list of all purchases made including date, time spent and name of a merchant.

TemboCardVisa

TemboCardVisa provides instant and safe access to your bank account from any place and at any time. TemboCardVisa is secured by the VISA Electron assurance and is globally accepted as a mode of paying electronically – through any VISA affiliated merchant outlet or VISA affiliated ATM worldwide.

Features and Benefits

Free TemboCardVisa
Pay for your purchases conveniently using TemboCardVisa
Pay for online shopping and transactions
Worldwide acceptance

Matumizi mengine lukuki yapo:
TemboCard

Baada ya kuvutiwa na huduma hizo nilkwenda benki nikajisajili ili niweze kupata huduma hizo hasa ya online shopping.

Kwa mshangao bado nikawa siwezi kutumia kadi. Baada ya kufuatilia benki nikaambiwa jibu ambalo sikutegemea kupata.

Jibu lilikuwa kwamba: Kadi yako pamoja na kuwa ina alama ya visa electron ni tembo card ya kawaida, haiwezi kutumika kwa shughuli niliyoomba.
Nikashauriwa nibadilishiwe kadi.

Pale benki nikaambiwa kadi nzuri itakayonifaa ni Tembocard master card.

Mwezi mmoja baada ya kupewa kadi yangu ya Tembocard Master card nikaenda tena kuisajili kwa ajili ya online shopping.
Siku mbili baadae nilipofuatilia nikaambiwa hizo kadi za Mastercard bado hazijaanza kutumika kwa ajili hiyo kwa hiyo siwezi kutumia kwa matumizi ninyoomba.

Kuna mambo mawili hapa.

Moja ni kwamba nimekuwa nikilipa Tsh 6,000 kwa mwaka kama ada ya kuwa na Tembo card Visa kwa takriban miaka 4 wakati kadi yangu ni (Sham au feki visa)

Pili kwa maoni yangu naona walistahili kuwambia wateja ukweli kuhusu hizi kadi zao za Master card. Ingawa nina wasiwasi pia hata hizo za visa.

Hayo ndio yaliyonikuta.

Nimeona ni vema ku-share ili msije mkashtuka mambo haya yatakapowakuta.

Yawezekana wapo wengi wanaotembea na tembo card za kawaida wakidhani ni visa au mastercard.

Naomba kuwasilisha.
 
nenda standard chartered au stanbinc

upate kadi za kweli....

nimesikia hata exim bank na diamond trust wanatoa visa card za ukweli.sina uhakika lakini

crdb ni local zaidi
 
Nimefanya crdb kwa muda mrefu sana tena department ya tembo card tatizo Crdb kuna staff pale wako sifuri kichwani pengne unabahati ya kuhudumiwa na wanafunzi wa fild, na pengne kama kachoka anaweza kukujibu simple mradi tu uondoke.
 
Wewe uliye na majibu tupatie mwenzetu!
 
Mbona mie nilishafanya online transaction kwa kutumia "TemboCard Visa"?, japokuwa haikuwa card yangu, ila niliomba kwa rafiki yangu akatumia card yake na ikakubali, ninachojua mimi ni kwamba inabidi Card iwe "activated" na unaingia mkataba wa kukubali itumike kwa matumizi hayo.
 
Kama umesoma post yangu taratibu zote unazosema nilizifuata.

Pengine wewe ulikuwa miongoni mwa wachache waliobahatika.

Nimetoa tahadhari tu kwa watumiaji wa hizo kadi usije siku moja ukawa na shida ya kuzitumia halafu ukakwama.

Kwa jumla imani yangu kwa sasa na hizo kadi imepungua sana.
 
Nimefanya crdb kwa muda mrefu sana tena department ya tembo card tatizo Crdb kuna staff pale wako sifuri kichwani pengne unabahati ya kuhudumiwa na wanafunzi wa fild, na pengne kama kachoka anaweza kukujibu simple mradi tu uondoke.
Mkuu unaweza elezea kuhusu tembo card hospital ile ya crdb kitambo icho
 
Niko na kad ya faida exim ambayo master card niliwaambia lengo ni kufanya manunuzi mtandaoni...ajab niliambiwa kadi IPO tayar naweza Fanya manunuz japo sikupewa fom ya kujaza kuomba itumike ivyo....nimejab kuosajil playstore pia na PayPal imekataliwa....Wanazingua nitawarudia tena
 
Hivi unaweza kuwafungulia mashitaka kwa udanganyifu na kukutia hasara ya makato pasipo kukidhi mahitaji yako!?
Sheria zna sema vp !??
 
Equity bank wana visa card na hazina usumbufu huo ulioelezwa na mdau hapo juu
 
sasa hivi CRDB wanafyatua card ambazo hazina hata jina lako pindi ufunguapo account

yaani kama kusajili laini vile unakuta card tayari wanacho fanya ni kuisahili tu na kukupatia
 
sasa hivi CRDB iwanafyatua card ambazo hazina hata jina lako pindi ufunguapo account

yaani kama kusajili laini vile unakuta card tayari wanacho fanya ni kuisahili tu na kukupatia

Mbona equity bank wanakupa kadi siku hiyo hiyo na jina lako wanaandika
 
Mbona mie nilishafanya online transaction kwa kutumia "TemboCard Visa"?, japokuwa haikuwa card yangu, ila niliomba kwa rafiki yangu akatumia card yake na ikakubali, ninachojua mimi ni kwamba inabidi Card iwe "activated" na unaingia mkataba wa kukubali itumike kwa matumizi hayo.
Exactly. Hizi card sio AUTOMATIC visa ama Master card. Lazima ufanye activation kwa kujaza fomu maalum inayopatikana benki hapo hapo, ndipo iwe activated
 
Back
Top Bottom