Uzoefu miaka kumi

mshamu

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
418
133
Ndugu hivi tangazo la kazi linapohitaji mtu mwenye uzoefu wa miaka kumi wanakuwa wanhitaji wazee au kuna vijana wenye uzoefu huo au ni mbinu zao watoto wa wakulima tusiombe!
 
Ndugu hivi tangazo la kazi linapohitaji mtu mwenye uzoefu wa miaka kumi wanakuwa wanhitaji wazee au kuna vijana wenye uzoefu huo au ni mbinu zao watoto wa wakulima tusiombe!
tujalie wewe umemaliza chuo ukiwa na miaka 24 ukakaa mtaani mwaka mzima
baadae ukapata kazi ukiwa na umri wa 25,ukijumlisha hiyo miaka10 jumla utakuwa
na miaka 35 hapo bado wewe ni kijana. kwa kampuni change mimi huwa siwalaumu
ila hizi kampuni kongwe kwanin wafanye hivyo!!!!!!!!
 
Ndugu hivi tangazo la kazi linapohitaji mtu mwenye uzoefu wa miaka kumi wanakuwa wanhitaji wazee au kuna vijana wenye uzoefu huo au ni mbinu zao watoto wa wakulima tusiombe!
Lawama tu. Ukweli kuna haja ya kwa baadhi ya nafasi kuweka uzoefu kwa kuwa huendi pale kujifunza kazi bali kufundisha wengine. Unapoona tangazo jaribu kuangalia wanataka applicant wa nafasi gani? Mfano wewe umehitimu leo Chuoni unataka kuomba nafasi ya Senior Human Resource Officer ambayo inahitaji uzoefu wa miaka 7. Au unaomba Principal Administrative Officer wakati nafasi husika inataka uwe na uzoefu wa miaka 12 kazini theni unalalamika. Hata hivyo sera ya ajira ni kwamba nafasi zote za kuingia (entry post/position) uzoefu sio kigezo mojawapo
 
Back
Top Bottom