Uzito wa Zitto, Wepesi wa Hoja kwa Suala zito

Kama kweli kuna watu wanampiga Zitto kwa sababu ya dini yake...basi ni jambo la kusikitisha.

Labda tu kama kuna watu wameishiwa hoja wanaanza kukimbilia hizo nguzo kuu za kishetani zilizosukwa na kusimikwa na CCM yenyewe (Makundi/mitandao, ufisadi na udini/ukabila/ukanda). Mtu yeyote anayejikta katika nguzo hizo, hafai kabisa hata kugombea ujumbe wa nyumba kumi.

Wanaomuunnga mkono kwa dini yake ni wengi zaidi,,, we fikiria hadi Mohamed Shossi anaunga mkono CDM linapokuja suala la Zitto agombee urais. Eti ndio alisababisha CDM ikapata wabunge wengi...
 
IKHOIKHOI ,

Tusisahau pia kwamba - Chini ya Katiba ya Muda ya JMT iliyodumu kwa miaka kumi na mbili 1965 hadi 1977, kigezo cha umri mgombea Urais kilitamka: AWE AMEFIKISHA MIAKA 30; Miaka 40 ni kigezo kilichoingizwa kwenye Katiba ya JMT 1977, ambayo tunayo hadi sasa; Swali linalofuata ni je:


  • Kwanini wakati ule kigezo kilikuwa ni miaka 30 wakati population ya vijana (18-35) ilikuwa ni ndogo sana ikilinganishwa na leo?
 
Nimesoma Gazeti la Raia Mwema la Jumatano wiki hii, habari zilizoshika kasi ni za Zitto pekee. Zitto anaandikwa kama vile ni Rais tayari, kwa tathmini yangu Raia Mwema la Jumatano limeandika jina 'Zitto' mara nyingi zaidi ya ambavyo toleo moja la Raia Mwema limewahi kumwandika mtu yeyote akiwemo hata Rais.

Ni mteja wa JF (active member), ninaingia JF walau mara moja kwa siku na kila nikiingia lazima kuwe na maada inayojadiliwa kumhusu Zitto, hasa baada ya yeye kutangaza kugombea urais. Kwa tathmini yangu kuna wastani wa Thread mbili mpya zinaanzishwa kila siku kumhusu Zitto na zinapata wachangiaji wa kutosha. Kama nimechemka takwimu nisaidiwe tafadhari.

Ni msomaji wa gazeti la Mwananchi japo sio kila siku, lakini kila toleo ninalobahatika kulisoma lina habari kumhusu Zitto.

Sina hakika kwa vyombo vingine vya habari vya siasa ila kwa hivyo nilivyovitaja hapo juu msimamo ni kama nilivyoeleza.

Kwa msimamo huo wa Zitto kutajwa tajwa mara nyingi sana inatoa picha gani? Zitto kaongeza popularity baada ya kuwin media, na akiendelea vizuri itamsaidia.

1. Katangulia kujitangaza mapema, wananchi tutamfanyia assessment ya mabaya na mazuri yake na tutatoa mrejesho nyuma (feedback) mapema ya Zitto tusiyempenda na akiweza atajirekebisha mapema (japo mbele ya wananchi, moyoni ni juu yake). Kufikia mwaka 2015 muda wa kampeni yeye tayari alishachambuliwa na tulishamwelewa.
Faida inakuja kwamba kama ataweza kujionyesha vile watu wanataka kumwona atafanikiwa, watu hatutkuwa na muda wa kuanza kumchambua mtu mwingine tena kwa kipindi kile kifupi cha kampeni, bora huyu ambaye tulishamjua na mapungufu yake tunaona kwamba tunaweza kuyaishi.
2. Hasara ya kutangulia ni kwamba maovu yake tutayajua mapema kwa sababu muda unatosha wa kuibua vitu vibaya vinavyomhusu na muda mwingi atautumia kujisafisha.
3. Kwa sababu kawahi kujitangaza watu watamtafuta waweze hata kumpandikizia kashfa (muda unatosha) kama point ya 2 juu, atahitaji kujisafisha.

Yote kwa yote kuna faida kubwa zaidi kujitangaza mapema kuliko kujitangaza umechelewa, kama tuna kumbukumbu nzuri baadhi yetu tulilalamika kwamba kama Dk Slaa angetambulishwa mapema hari ingeweza kuwa nzuri zaidi ya ilivyokuwa. Kwa hiyo kama Chadema wana nia ya kweli ya kugombea urais strategy ya Zitto inahusika sana.
 
Mkuu Suala la ZItto kutaka kugombea URAIS wala sio Zito kama unavyotaka kutuaminisha hapa.
Ni Suala Jepesi Mnoo, Kutokana na Katiba ya Sasa, Zitto kuna sifa ana lack za Kugombea.
So kitu atakachokifanya ni Kuhakikisha kuwa suala la Umri linarekebishwa kwenye mchakato wa katiba Mpya chini ya Tume ya Judge Warioba ili apate sifa za Kuwa Mgombea which is BASICALLY NI UBINAFSI NA UROHO WA MADARAK ambao kimsingi unampotezea sifa zoote za kuwa hata katibu wa Tawi la Chama.......Over.

Hoja yako imejadiliwa, na ndio uzito wenyewe wa hoja, vinginevyo bado kuna maeneo hayo yenye hoja nyepesi nyepesi, za kumuunga mkono, na za kumpinga, na nadhani kama unafuatilia mjadala huu utagundua hilo; karibu;
 
Mkuu the fact kuwa hakuna chama kinachofanya hivyo au kina mpango wa kuyafanya hivyo, haina maana kuwa viendelee kufanya wanayofanya sasa. Otherwise, tutakuwa tunalalamika tuu halafu wakti huo huo tunajustify wanayofanya sasa. Kwa mfano utaratibu wa CCM, nafasi ya mwenyekiti na makamu wake hazigombewi, bali hutokana na uteuzi wa Kamati Kuu na majina kuthibitishwa na Halmashauri Kuu (Nec), ambapo chini ya utaratibu wa sasa, Rais ndiye anayekuwa mwenyekiti wa chama taifa. Kimsingi huu si utaratibu mzuri. Lakini pia haiwezekani uachwe kwa sababu tuu mazingira hayaruhusu. Kuwepo kwa mabadiliko ya kuchagua mtu makini mwenye viwango vya kuwa Rais kutalazimisha kuwepo mabadiliko kwenye vyama pia.

Mkuu EMT,

Hapa tunaongelea siasa za uchanguzi katika nchi yetu ya Tanzania. Hatuwezi kujenga hoja yoyote tukaeleweka bila kuangalia hali halisi na mazingira yetu. Kujaribu kuanzisha mfumo wa selection of candidates kwa sasa ni kutaka baadhi ya watu waangamizwe kabla ya uchaguzi wenyewe.

Nimesema huko nyuma kuwa, mfumo wetu wa uchaguzi ni wa kisanii na wala hauna uhalisia wowote. Hauna uwezo wa wowote wa kutoa uhakika wa ulinzi wa mali na maisha ya watu wanaongombea uongozi katika nchi yetu. Ndiyo maana kwa sasa, wagombea wengi ni wale wenye uwezo mkubwa na mafukara wachache sana ambao ni risk takers!

Baada ya uchaguzi wa 1995, utakumbuka kilichowapata walioiunga mkono NCCR Mageuzi na Mrema. Wafanyabiashara walifilisiwa na baadhi ya wafanyakazi walipata shida makazini kwa maelekezo ya dola. Mwaka 2000, serikali ilitoa waraka wa utumishi unaomtaka mtu anayegombea na kupitishwa na tume kuachia nafasi yake katika utumishi wa umma. Hata hivyo, wale waliogombea kupitia CCM walirejeshwa kazini na wale wa upinzani kupoteza ajira. Wengine walirudishwa ila baada ya kusota sana. Pia watu ambao wameonekana kuunga mkono upinzani iwe ni wafanyabiashara au wafanyakazi, wamepata usumbufu sana kwenye biashara zao na makazini...na wengine kupoteza mali, vyeo au ajira zao.

Sasa unamtaka nani atangaze leo kugombea ili ashughulikiwe? Ndiyo maana tunamshangaa Zitto kwamba nani kamhakikishia ulinzi wake binafsi na mali zake kutoka kwa dola ile ile ambayo imewanyanyasa watu ambao wameonekana kutishia nafasi ya CCM kuendelea kubaki madarakani.......Kama hili watu hawalioni basi...ila ipo siku litaonekana!!

Mfumo wetu bado haujafika hapo. Ushauri wangu ni kwamba vyama vya upinzani vijiimarishe na kujenga ari ya ushindi (kama ilivyokuwa wakati wa kudai uhuru) huku vikiweka mikakati yao ya kufumua mfumo wa sasa wa utawala na uchaguzi pia.
 
Last edited by a moderator:
Unapoongelea suala la kanuni na katiba, inashawishi sana. Inasikika vizuri masikioni. Lakini ukweli ni kwamba hakuna taasisi duniani inayoendeshwa kwa kanuni na katiba peke yake. Kuna mila na desturi pia, tena taasisi zingine hazina kanuni wala katiba-zina mila na desturi tu ambazo hazijaandikwa popote. Kwahiyo, kwa kuzungumzia kanuni na katiba tu, unakuwa haujaeleza ukweli wote.

Nakubaliana na wewe kimsingi, ila hoja yako nilishaijadili kwenye bandiko lingine na kuuliza swali, lakini sijajibiwa; ukipata muda itafute, au nikirudia mabandiko yangu ya awali nitaku 'cc';
 
Msiwe mnatishika na kila scrutiny kwa chama chenu, sio kila hoja ina nia mbaya, vinginevyo kama nilivyosema, mimi ni raia mpiga kura, CCM inafuata baada ya hao, lakini kama nilivyokuambia, sio ajabu mimi kupigia kura mgombea wa chama kingine Chadema ikiwepo, na haitakuwa mara ya kwanza kufanya hivyo; Vinginevyo, majibu yangu unayosema hayajitoshelezi bado nayasimamia kama counter argument kwa hoja yako;

Kwa usemi huo, wewe utakuwa CCM masalia...Kwa wana CCM original, chama kwanza na kitu kingine ikiwemo nchi kinakuja baada ya hapo.

Tafadhali jaribu kutuweka sawa kama mtazamo huo ndani ya chama umeshabadilishwa.

I hope, unakumbuka wimbo wa John Kombo ambao amekuwa akiuimba mbele ya viongozi wote wa CCM bila kukemewa.
"...Wapizani, tuwachane chane tuwatupe
...CCM tuwakumbatie tuwabusu...."

Hao wapinzani sio watanzania??
 
Tumemchoka huyu jamaa, kila wakati habari zake,,, mbona ni mtu wa kawaida sana,, hoja zake ni za kawaida,, elimu yake ni ya kawaida,, hakusoma shule za vipaji maalum... Jamani ana nini huyu Zittoooo, anatukuzwa utafikiri yuko daraja moja na akina Albert Einstein, Isaac Newton,,, Give us break folks...

Hivi Dar es Salaam Stock Exchange iliclose vipi ijumaa, ilipanda au ilishuka???
 
nitaongezea kidogo.

Tumefundwa kuwa kuna aina mbili ya KATIBA. 1. KATIBA ILIYOANDIKWA 2. KATIBA ISIYO ANDIKWA. Ni ukweli kuwa, katiba ya chadema imeandikwa na hivyo kila kitu kiko wazi mtu kukijua kupitia katiba hiyo.

LAKINI.
Morals( mila na desturi) za CHADEMA ktika mambo ya uongozi hazijaandikwa, bali zipo mioyoni mwa watu. Nasema hazijaandikwa kwa kuwa hadi tunafika 2010 januari, wengi walijua mbowe ndiye angegombea URAIS. Hadi bunge linavunjwa wengi waliamini hivyo. Lakini kilchokuja kutokea ilikuwa ni tofauti kabisa.

1. Nani alijua Dr. Slaa angegombea?
2. Nani alijua Dr. slaa angeachia jimbo lake alilolihodhi na bila shaka angeshinda ushindi wa kishindo.

Bila shaka suala la urais ni zito sana, linataka mtu kuwa mvumilivu na mwenye subra.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya kuwa, Mmwogope mtu anayeutafuta urais, huyo akipata urais atatuangamiza. Ni hofu ya namna hii inayosababisha watu na mimi nikiwa mmoja wao kutokuamini dhamira ya Zitto

Upo sahihi, lakini kutegemea sana KANUNI zisizoandikwa ni tatizo, hasa iwapo hoja za namna hiyo zinajengwa kwenye mijadala nyeti namna hii kama ya Urais wa nchi, Rais ambae anapatika kupitia mfumo wa siasa wa demokrasia ya kiliberali, mfumo ambao upo imported, mfumo ambao suala la uongozi ni suala la mtu binafsi, sio suala la chama...; Kanuni zisizoandikwa zina maana zaidi kama suala hili lingekuwa ni la kutafuta viongozi kimila; Vinginevyo katika demokrasia ya uliberali, anachohitaji mgombea ni Name Recognition na Uwezo wa Fedha, basi; Suala la timing linakuwa halina nguvu, hasa iwapo mgombea ni wa upinzani, sio wa chama kilichopo madarakani, huku lengo lake kuu likiwa ni kukiondoa chama kilichopo madarakani;
 
Wanaomuunnga mkono kwa dini yake ni wengi zaidi,,, we fikiria hadi Mohamed Shossi anaunga mkono CDM linapokuja suala la Zitto agombee urais. Eti ndio alisababisha CDM ikapata wabunge wengi...

Masikini...hao wanaweza kudhani kuwa wanamsaidia kumbe wanamwangamiza.

Waangalie kilichotokea kwa CUF halafu ndo waanzishe jaribio jingine ama kwa Zitto au mtu mwingine.

Kwa kuwa hapa umeingiza suala la dini...naomba hiii iwe kauli yangu ya mwisho kuhusu hoja hii na mambo ya dini!!
 
Mchambuzi hoja ya watu kumpinga Zitto zipo hivi;

Ielelweke kuwa Zitto hajavunja kanuni yoyote ya chama au katiba ya CDM kutangaza kugombea urais 2015. Tatizo linakuja, hajafanya "proper timing" ya yeye kutangaza suala hilo. Leo ni 2012, mpaka 2015 bado safari ni ndefu sana upepo wa kisiasa unaweza kuvuma vyovyote.

In connection to that, CCM inateswa na mzimu wa urahisi 2015. Sasa kitendo cha yeye kutangaza hilo maana yake hajajifunza makosa ya CCM kukesha kulumbana, kuhujumiana n.k kwa sababu ya urais tu!!!!! Sasa kwa nini yeye asijifunze kutoka kwa wapinzani CCM?????

Mimi ningeomba Zitto aelewe mpaka sasa CDM haijasema itamsimamisha nani kwa sababu inajua kazi kubwa iliyopo mbele yake ya kuchanga karata yake vizuri katika kipindi kilichobaki ili 2015 mambo yaende kama ndoto zao zilivyo yaani kushika dola.

Nijuavyo Zitto ni mjuvi sana na si kwamba haya tusemayo hayajui ila sielewi ni kwa nini anafanya hivi. Namtahadharisha asidhani CCM tayari imeshindwa 2015 kiasi cha kung'ang'ania au kugombea urais kiasi hicho.

Namuombea kwa Mungu ampe uhai na hekima ili KUDRA ya Mwenyezi Mungu ifanye kazi.
brother zitto ni mjuvi sana kama ulivyosema anajua tunayosema na anelewa anachokifanya hiyo ndio kazi aliyotumwa kupunguza nguvu zetu ndio anachokifanya mkuu yupo kazini huyo bahati tumeshamjua dawa kama kuchinja kobe
 
Ndugu Mchambuzi, binafsi nimependa sana title ya thread yako pamoja na maswali makubwa mawili uliyoliza kwa pande zote mbili; unajua sana kutumia maneno. Jibu langu ni kwa maswalli yote mawili fupi sana na wala haliangalii kambi kati ya hizo mbili.

Zitto ana haki ya kusema lolote katika jamii hii kama ambavyo wewe na mimi tunavyoandika hapa, ila kama ambavyo kila power ina responsibilities zake, yeye kama mtu mwenye power fulani katika jamii inabidi ajue responsibilities zinazokuja na power aliyonayo. Kutangaza kuwa anataka kugombea uraisi mwaka 2015, miaka mitatu ijayo kunafanya kila jambo atakalosema au kufanya wakati huu chini ya power aliyonayo kuwa ni kampeini ya kuwania uraisi mwaka 2015, na hivyo kuwa amekiuka responsibilities zake. Wakati mwingine kukaa kimya kunatuma message yenye nguvu kuliko kusema lolote. Na sisi tulifuyndishwa wakati fulani kuwa debe tupu haliachi kutika tunaanza kudhani kuwa huenda Zitto ni debe tupu sana ndiyo maana liaanza kutika mapema!

Asante kwa mchango wako kichuguuu,

Mimi naona tunakabikiwa na changamoto nyingi sana katika zama hizi za demokrasia ya uliberali; Tunataka mageuzi ya kisiasa kwenda kwenye mfumo huu, lakini tunaweka 'brakes' kwenye nguzo muhimu zinazojenga demokrasia hiyo, kama vile suala la mgombea ambalo chini ya mfumo huu, ni suala la mtu binafsi, sio suala la chama; Hii ni tofauti na mifumo mingine kama tuliyokuwa nayo enzi za TANU na CCM - kabla ya ujio wa vyama vingi vya siasa, ambapo suala la kugombea ni suala la chama, sio mtu binafsi;

Nazidi kuhimiza kwamba - kitendo cha kumpinga Zitto kwa kutumia KANUNI ambazo hazijaandikwa, kinampa Zitto MORE POLITICAL MILEAGE; Kwa Zitto, this is more a political Assest, na kwa wale wanaompinga, hasa ndani ya chama chake, it is more of a Political Liability; Wapo wananchi ambao wanatafsiri kinachoendelea kama ni fitina na woga dhidi ya Zitto, kwani msukumo wa kumpinga Zitto hautoki kitaasisi hata kutoka chadema bali unatokea barabarani na vibarazani; Hili ni tatizo; Pengine kuna wachache humu wenye upeo wa kuona tofauti, lakini kwa wapiga kura wanaotaka mabadiliko, wengi wao ambao ni wajinga (kwa maana ya umaskini, maradhi na ujinga), hili ni tatizo; Ni muhimu Chadema ikatoa kauli ya kikanuni baada ya kukaa chini na Zitto, vinginevyo mtakuja kuona madhara ya malumbano haya yasioegemea hoja Kikanuni, bali hoja juu ya ustaarabu na utamaduni, kuhusu suala linalohusu demokrasia ya uliberali, huku sehemu kubwa ya utamaduni wake ni kwamba - suala la kugombea nafasi ya siasa ni suala la mtu binafsi, sio la chama;

Wengi wangetumia muda kidogo kuelewa msingi wa hoja yangu, ambao nimeujadili kidogo hapa katika majibu yangu kwako, nadhani wangeelewa nini ninacho lenga na mada hii;
 
Hakuna tatizo, hasa kama ukiondoa kuhisi na kuweka uhakika kwako binafsi, usiyumbishwe na kuamua kwa hisia, tena hizia za watu wengine, pata hisia kwa kuwa na facts zinazokuridhisha wewe na akili yako natumaini ya kiutu uzima.

Ndo nachotafuta mie hapa kwa kuuliza

Mkuu Haika, sisi ni watu wazima na tunaona kila kitu kinavyoenda. Hatuhitaji ushahidi wa kuunga unga au kuokoteza kusema kuwa Zitto anavyojaribu kupeleka mambo sivyo!

Suala la kuchukua uongozi wa nchi katika mazingira yetu ni kama vita. Kwa watazamaji, vita inaweza kuwa real au factious. Katika vita halisi, wapiganaji wanakuwa pamoja mwanzo hadi mwisho na hakuna nafasi ya kuwagawa katika vipande vipande au kuwapunguzia morali ya kuendelea na mapambano. Tumeshuhudia na kusimuliwa vita za ukombozi Msumbiji (FRELIMO), Zimbabwe (ZANU-PF), Angola (MPLA) na Namibia (SWAPO). Sehemu yoyote ambayo mapigano yaliendeshwa kwa hisia za vikundi vikundi kama Zibambwe, ukombozi ulikuwa mgumu, wa gharama kubwa kwa maisha na ulichukua muda mrefu.

Kwa sasa CHADEMA wanapambana kujenga base ya chama...na nahisi hilo ndilo liko kwenye fikra za kila mwanachama wa kweli na kipaumbele cha kila kiongozi. Je Zitto anaonekana hivyo, especially unapomtazama na mambo yake ya urais?

Ila katika vita za kwenye movies, unaweza kufanya lolote kwa sababu hakuna cost ya aina yoyote itakayokupata in terms of lives au kutofikia malengo..Hata hivyo, unaweza kuharibu movie na kuwakera watazamaji.

Je Zitto yuko kwenye mapambano halisi au ya kisanii (fictious)??

Kwa mfano huo, na maswali yangu mengine katika post zangu za huko nyuma, unaweza kuona kuwa uamuzi wa Zitto unazua maswali mengi ambayo hayana majibu na hata kama majibu yapo, kuna watu hatuwezi kuridhika nayo. Kwa maana hiyo, tuna kila sababu ya kufikia hitimisho kwamba tayari kajigeuza muumini wa nguzo za kishetani za CCM (makundi/mtandao, ufisadi na ukabila/udini/ukanda)...

Sina shaka, kila kitu kitajulikana soonl!!
 
Last edited by a moderator:
brother zitto ni mjuvi sana kama ulivyosema anajua tunayosema na anelewa anachokifanya hiyo ndio kazi aliyotumwa kupunguza nguvu zetu ndio anachokifanya mkuu yupo kazini huyo bahati tumeshamjua dawa kama kuchinja kobe


Kama kweli ni mjuvi na anakubali kutumia, anaweza kutuongoza katika challenges tunazokabiliana nazo??
 
Mods hili jukwaa sasa linachosha!kwa siku zinaingia thread mbili au zaidi juu ya suala hilohilo ambalo kwa watu makini,huwezi kupoteza muda kujadili kwasababu moja tu!ZZK hana sifa ya awali(UMRI)ambayo hata babu yangu anayo,itakayomuwezesha kuanza sarakasi na matusi(WALIOZALIWA KABLA YA UHURU HAWANA UWEZO WA KULETA MAENDELEO)kuelekea huo Urais anaoota usiku na mchana.Lazima wanajamvi mtambue kwamba katiba iliyopo sasa ni hai,halali na tunafanya kazi,maamuzi na pengine kwa kiasi fulani tunafikiri kwayo.Suala la huyu bwana lingefaa lijadiliwe baada ya hiyo katiba mpya kutungwa na kumpa sifa hiyo.Nani anajua kwamba umma utaridhia umri upunguzwe?Tunatumia nguvu kubwa kujadili(kiherehere)cha mtu mmoja anayeonekana kila akilala anauota uraisi hali kadhalika mchana kutwa.Hatimaye wote tutakuwa majuha kwa kupigwa upofu wa mawazo.

In politics, mabadiliko ni kitu cha kawaida sana, usishangae suala la umri likabadilika ghafla kama itakuwa ni ASSET kwa elite kuelekea 2015; Nani alitegemea dakika ya mwisho suala la zamu ya mwanamke ndio litatawala uchaguzi wa spika; CCM ipo katika hatua ya kusambaratika, kwahiyo lolote ambalo litaipa CCM a political mileage, believe me, CCM italichukua, hata kama ni kuweka umri wa mgombea urais uwe miaka 30; Isitoshe, katiba ya muda iliyodumu kwa miaka kumi na mbili yani 1965 - 1977, kigezo cha kugombea Urais kilikuwa ni MIAKA 30, hili la miaka 40 lilikuja na Katiba ya 1977;

Ndio maana nimeweka a second set of questions kwenye bandiko langu namba moja ambalo limezingatia uwezekano huu; Kwahiyo ni muhimiu Zitto, na hata wote wenye kutaka nafasi hii nzito ya Urais wa nchi, pia wakaulizwa maswali, hasa yale ambayo nimeyaweka kwenye bandiko langu namba moja chini ya kichwa - Tukihamia kwenye upande wa pili wa hoja.
 
Asante kwa mchango wako kichuguuu,

Mimi naona tunakabikiwa na changamoto nyingi sana katika zama hizi za demokrasia ya uliberali; Tunataka mageuzi ya kisiasa kwenda kwenye mfumo huu, lakini tunaweka 'brakes' kwenye nguzo muhimu zinazojenga demokrasia hiyo, kama vile suala la mgombea ambalo chini ya mfumo huu, ni suala la mtu binafsi, sio suala la chama; Hii ni tofauti na mifumo mingine kama tuliyokuwa nayo enzi za TANU na CCM - kabla ya ujio wa vyama vingi vya siasa, ambapo suala la kugombea ni suala la chama, sio mtu binafsi;

Nazidi kuhimiza kwamba - kitendo cha kumpinga Zitto kwa kutumia KANUNI ambazo hazijaandikwa, kinampa Zitto MORE POLITICAL MILEAGE; Kwa Zitto, this is more a political Assest, na kwa wale wanaompinga, hasa ndani ya chama chake, it is more of a Political Liability; Wapo wananchi ambao wanatafsiri kinachoendelea kama ni fitina na woga dhidi ya Zitto, kwani msukumo wa kumpinga Zitto hautoki kitaasisi hata kutoka chadema bali unatokea barabarani na vibarazani; Hili ni tatizo; Pengine kuna wachache humu wenye upeo wa kuona tofauti, lakini kwa wapiga kura wanaotaka mabadiliko, wengi wao ambao ni wajinga (kwa maana ya umaskini, maradhi na ujinga), hili ni tatizo; Ni muhimu Chadema ikatoa kauli ya kikanuni baada ya kukaa chini na Zitto, vinginevyo mtakuja kuona madhara ya malumbano haya yasioegemea hoja Kikanuni, bali hoja juu ya ustaarabu na utamaduni, kuhusu suala linalohusu demokrasia ya uliberali, huku sehemu kubwa ya utamaduni wake ni kwamba - suala la kugombea nafasi ya siasa ni suala la mtu binafsi, sio la chama;

Wengi wangetumia muda kidogo kuelewa msingi wa hoja yangu, ambao nimeujadili kidogo hapa katika majibu yangu kwako, nadhani wangeelewa nini ninacho lenga na mada hii;

Kwa wale wanaoamini kuwa Zitto katumwa na CCM hiki ndicho wanachokiongelea...Kwamba Zitto anajaribu kuleta mtafaruku ndani ili kuwagawa wapiga kura wa CHADEMA na mwishowe kuisaidia CCM.

Bahati nzuri kama kuna waliomtuma, basi wamekosea kwa kuanza hizo njama mapema kiasi kwamba by 2015, Zitto anaweza kuwa keshafutika kwenye siasa za urais. Hata hivyo, kwa sasa njama hizo zinachelewesha mipango ya kufikisha chama kwa watanzania wengi zaidi na kurahisisha kazi ya kuiondoa CCM madarakani. Which also suggests CCM's stake in the whole drama of Zitto's dreams!
 
Sina hakika wewe Mchambuzi na Bwana jmushi1 mnajadili katiba ipi hapa.

Mie nilidhani Mushi alikuwa anaongelea katiba ya nchi ambayo kwa asilimia 100 imeandaliwa na CCM. Hata hivyo, sina hakika kama katiba ya CCM kama chama ina jambo lolote la maana ambalo inaweza kuchangia au kuathiri katika hii issue!

Na huo ndio ulikuwa msingi wa hoja yangu katika majibu yangu kwa jmushi1, ambae alipendekeza niweke kundi la tatu la kumuunga zitto ambalo ni lile linalotaka kumpandikiza zitto kupitia CCM; nikamweleza kwamba mwisho wa siku, katiba na kanuni zitakazompitisha au mkataa Zitto ni zile za Chama Chake Cha Chadema, sio katiba ya NCCR, CUF, CCK< au hata ya CCM kama kuna ukweli kwamba CCM ndio inampandikiza;

Vile vile nikasema kwamba - haiingii akilini kwa jmushi1 kujadili kwamba CCM inampandikiza zitto, wakati CCM hiyo hiyo ndio inasimamia katiba yake ya nchi yenye kigezo cha mgombea urais kiwe miaka 40; Katiba ya JMT kama inavyojulikana na katiba ya CCM kwani iliundwa kukidhi matakwa ya chama kimoja; Kumefanyika amendments chache baada ya ujio wa vyama vingi lakini bado hizi hazijamaliza UHATAMU WA CCM;
 
Kwa usemi huo, wewe utakuwa CCM masalia...Kwa wana CCM original, chama kwanza na kitu kingine ikiwemo nchi kinakuja baada ya hapo.

Tafadhali jaribu kutuweka sawa kama mtazamo huo ndani ya chama umeshabadilishwa.

I hope, unakumbuka wimbo wa John Kombo ambao amekuwa akiuimba mbele ya viongozi wote wa CCM bila kukemewa.
"...Wapizani, tuwachane chane tuwatupe
...CCM tuwakumbatie tuwabusu...."

Hao wapinzani sio watanzania??

Unani address mimi kama nani lakini:

  • Mwanachama wa CCM?
  • Kada wa CCM?
  • Kiongozi wa CCM?
  • Mpambe wa kundi fulani la kutafuta Urais 2015 kupitia CCM?

Nadhani ukiwa specific kwanza juu ya hili, nitakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kujibu hoja zako na tukaelewana;
 
........Kwa mfano huo, na maswali yangu mengine katika post zangu za huko nyuma, unaweza kuona kuwa uamuzi wa Zitto unazua maswali mengi ambayo hayana majibu na hata kama majibu yapo, kuna watu hatuwezi kuridhika nayo. Kwa maana hiyo, tuna kila sababu ya kufikia hitimisho kwamba tayari kajigeuza muumini wa nguzo za kishetani za CCM (makundi/mtandao, ufisadi na ukabila/udini/ukanda)...

Sina shaka, kila kitu kitajulikana soonl!!

Nilitaka kujua kaka
japo bado hujanijulisha
 
In politics, mabadiliko ni kitu cha kawaida sana, usishangae suala la umri likabadilika ghafla kama itakuwa ni ASSET kwa elite kuelekea 2015; Nani alitegemea dakika ya mwisho suala la zamu ya mwanamke ndio litatawala uchaguzi wa spika; CCM ipo katika hatua ya kusambaratika, kwahiyo lolote ambalo litaipa CCM a political mileage, believe me, CCM italichukua, hata kama ni kuweka umri wa mgombea urais uwe miaka 30; Isitoshe, katiba ya muda iliyodumu kwa miaka kumi na mbili yani 1965 - 1977, kigezo cha kugombea Urais kilikuwa ni MIAKA 30, hili la miaka 40 lilikuja na Katiba ya 1977;

Ndio maana nimeweka a second set of questions kwenye bandiko langu namba moja ambalo limezingatia uwezekano huu; Kwahiyo ni muhimiu Zitto, na hata wote wenye kutaka nafasi hii nzito ya Urais wa nchi, pia wakaulizwa maswali, hasa yale ambayo nimeyaweka kwenye bandiko langu namba moja chini ya kichwa - Tukihamia kwenye upande wa pili wa hoja.

Ukomo wa umri au bila ukomo si tatizo endapo tutakuwa na hoja za msingi....

Kama tunataka kujipa nguvu za kusukuma hoja ya umri, basi tuchanganue sababu zilizowafanya wale waliokuwepo wakati wa uhuru waweke miaka 30 na wale wa baadaye wakaweka miaka 40. Tukijua hoja zao na kuzichambua tunaweza kuja na mapendekezo ya hoja zinazokidhi mahitaji ya nyakati na siyo mtu/watu.

Vinginevyo, tutabaki tunaelea hewani!
 
Back
Top Bottom