Uzio wa hotel aliyozindua rais j kikwete wabomolewa

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,799
30,724
Leo nimepita maeneo ya Snow crest hotel aliyozindua Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete siku ya ijumaa nakukuta uzio[ukuta] umebomolewa.
Nimejiuliza maswali mengi bila kupata majibu,inakuwaje hotel iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais imevunjwa ukuta siku tatu baada ya kuzinduliwa.
Wakuu wa vyombo vya usalama walishindwa kumfahamisha rais kwamba hotel ilikuwa imejengwa eneo la hifadhi ya barabara ?.

Nadhani hii ni aibu nyingine ambayo ingeweza kuepukwa kama wanausalama wangezingatia maadili ya kazi yao.

Naomba kuwasilisha.
 
Ngongo,
Mazingira ya kumwita rais kuzindua ile hoteli , kwangu binafsi siyatambui kabisa!
Kuna usanii wa juu sana pale!..Hakika ni udhalilishaji sana kwa rais kuhudhuria kitu kama kile, ambacho naamini mtumishi yeyote wa wizara ya utalii wahapa Arusha angeweza kufanya..shame on the owner, shame on washauri wa rais!
 
Nikipita barabarani inaonekana ni hotel yenye vyumba kama 50 tu,nikashagaa sana kusikia Muungwana anaacha shughuli za maana na kwenda kufungua kijihotel kidogo tena kilichovunja sheria za nchi sijui ni kwanini mkuu wa mkoa wa Arusha asijiuzulu kwasababu hii ni mara ya pili Muungwana anadhalilishwa.

Muungwana aliwekwa kwenye mtego wa kukabidhi pikipiki zilizonunuliwa na watuhumiwa wa EPA.Watu wa system wanafanyakazi gani hapa na meneja wa TANROAD mkoa wa Arusha alikuwa anasubiri hotel izinduliwe na rais wa JMT ndipo aanze kuvunjaa.Ipo haja ya kuchunguza sakata zima kwasababu vitendo vya namna hii si vidogo lazima kuna jambo hapa.
 
Hata mimi nimeshangaa kukuta uzio wa chuma (sio ukuta) umevunjwa, sina uhakika kama ni Tanroads wameuvunja ingawa kila dalili inaonyesha kwamba umevunjwa na tanroad au chombo cho chote chenye mamlaka.

Ni aibu nyingine kwa kweli.
 
Yu neva noo, labda ana hisa zake pale mtajuaje??
 
Heri huyo aliyeamuru ubomolewe.

____________________________________________
"And where the offence is, let the great axe fall.”
William Shakespeare
 
Hawa jamaa walikwisha pewa notice siku nyingi sana ya kubomoa ukuta, mwishowe wakaomba kwa Tanroad waachiwe hadi baada ya hoteli kufunguliwa rasmi watabomoa wenyewe..wakati hili likiendelea wakata kucheza dili Regional Engeneer wa Tanroad aahamishwe..actually alikwishahamishwa ila transfer ikasimamishwa..
 
Leo nimepita maeneo ya Snow crest hotel aliyozindua Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete siku ya ijumaa nakukuta uzio[ukuta] umebomolewa.
Nimejiuliza maswali mengi bila kupata majibu,inakuwaje hotel iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais imevunjwa ukuta siku tatu baada ya kuzinduliwa.
Wakuu wa vyombo vya usalama walishindwa kumfahamisha rais kwamba hotel ilikuwa imejengwa eneo la hifadhi ya barabara ?.

Nadhani hii ni aibu nyingine ambayo ingeweza kuepukwa kama wanausalama wangezingatia maadili ya kazi yao.

Naomba kuwasilisha.


Period!!!!!

Duh!! piata ati nasikia tetesi katika hotuba alio itowa pale snow crest Hotel siku ya ufunguzi alisema kuwa wazawa tunatabia ya udokozi na ndio maana experts wengi wanaajiliwa kwa Hotels na kwingineko?

Kama kweli Rais alitamka hicho kitu kuna haja ya kuhoji Utawala wake wote!!

Napenda toa mfano michache tu Kwenye Hotels Utakuata;
GM=Mhindi from India
FC=Mhindi from India
Exct-Chef=Mhindi from India
Stores Manager=Mhindi from India
Exct-Housekeeper=Mhindi from India
FOM=Mhindi from India

Sasa cha ajabu nenda Immigration na uwaulize vibaliwa walivyovitoa kwa hawa watu vina vyeo gani na kazi aifanyayo inaendana na cheo kilicho andikwa kwa working permit(Resident Permit classb) The Immigration Act,1995 (section 20)
*(b)the holder shall not engage in any employment,trade,business or profession other than....... na wana muda gani wakifanya kazi ndani ya nchi katika eneo hilo hilo mmoja? mtashangaaaaaa wenyewe

Mishahara wanayo pewa na facilities zinginezo mtashangaaaa,

Alafu leo unaseama wazawa wasiwe wadokozii?? wakati kihalisia mtanzania huyo huyo ndie anayesota kazi usiku na mchana mishahara ni mara 4 hadi 5 kuwafikia hao wahindi na hakuna facilities wapatazo zaidi ya kutibiwa hospitali basi

hata managers wengine wa kitanzania mishahara yao ni mara 2 au 3 kwa hao experts nao wanachopata ni usafiri wa kufuatwa na kurudishwa na kwenda hospital ila hao wahindi wanalipiwa nyumba,umeme,maji,garina kulipiwa service zake,hospital tena nzuri kusomeshewa watoto,

Leo wasema mzawa asiwe na tabia ya udokozi wakati mazigira tu ya kufanya kazi ndi hayo amewekewa. Mwategemea nini??

Basi nao serikali waajiri wahindi na ma experts kwenye wizara zao basi maana nao wana scandal kila kukicha


 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom