Elections 2010 Uzinduzi wa Kampeni Za CCM - from ITV

Mbaazi zikikosa maua husingizia jua. Kwnai mitandao ndiyo imemfanya awe raisi legelege? Ndo inamfanya anakata network kila wakati? Nadhani angetumia muda wake kushughulikia matatizo yake binafsi (ikiwemo afya yake) na uwezo wake wa kuongoza badala ya kukimbiza vivuli!
 
UNAWEZA UKADHANI UNATAMBULIKA KUMBE HUTAMBULIKI..........ni sawa na baba mwenye nyummba na watoto wake kumi.....wale watoto wote wanajua kuwa hakuna kaka baba yao au aliye zaidi...KUMBE WENGI WAPO....!
 
Sikiliza hotuba ya Kikwete pale Jangwani hapo jana (21/8/2010) hasa kuanzia dakika ya 3.40 kuendelea. Hapo utamsikia Kikwete akiponda message za kwenye mitandao. Je ame-target JF specifically? Na Je, alichosema ni kweli? Na kama ni kweli kama tunajisumbua, kwa nini amepoteza muda kutuzungumzia kwenye hotuba yake? Mimi binafsi nahisi tumemgusa na tunamtisha. Wewe waonaje?

"...kwenye mitando huko kuna message nyingi,.... hivi, hivi, hivi,...wanajisumbua...wanajisumbua! Watanzania hawa hawadanganyiki...."
Ukirusha jiwe na ukasukia Mamaaaa weeeeeh ujue limempata
 
mdharau mwiba......

Mkuu umesema vema kabisa. Kama mpaka amesema kwenye hotuba basi mitandao inampa headache. Na mungu alivyokuwa mkubwa, ni katika youtube tumeona tukio zima la kuanguka kwa JK lilivyokuwa. Nina uhakika bila kuwa na mtandao tusimgeweza kuona lolote zaidi ya picha zenye kuficha tukio halisi lilivyokuwa.
Mwenye macho haambiwi ona. Hii ya kwenye youtube ni kivuli tu cha ukubwa wa effect za mitandao kwenye maisha yetu ya leo. Kama tukiendelea kubisha tutajariwa na kuona na mwanga halisi wa mitandao jinsi unavyokuwa. Hatutakuwa na wa kumlaumu. Katika hili la mitandao, njia nzuri si kuipinga.!!!
 
Huyu mtu amesha'panic aachie ngazi tu,mi nahisi akiendelea na hiyo kazi ngumu anayoifanyia mzaa ataendelea kuanguka sana kwan mengi atayasoma yatakayomchoma maadam anaendelea kuvurunda madarakani.Kwan akiacha huo urais nchi itafungwa?
 
Simply; Kikwete amelaani mitandao inayo eneza chuki na ukabila yenye malengo ya kuwatenganisha watanzania, kamwe watz hawatdanganyika. Hii ni message ya ku promote umoja kwa watanzania

Mavuvuzela wanashindwa kuelewa simple message, je mtakuwa na akili za kudadis complex data na messages? JF imeingiliwa!!!
 
JK anakasirikia mitandao maana anajua kuna njia ya kuthibiti yanayojadiliwa.

Mitandao ina nguvu kuliko magazeti maana wachache wanaochangia katika mitandao wako huru kuliko waandishi wa magazeti ambao ni waoga.

Wapo ambao wanasoma habari kupitia mitandao hali inayosaidia kupata habari;
 
Hata kama kuna mitandao ya chuki na udini etc, mbona hajatoa solution ya namna ya kukwepa uwepo wa mitandao?? Hizo complex data unazoongelea ziko wapi? Hizi za uchumi kukua na maisha bora kwa kila mtanzania au nyingine?? Maana inawezekana wote ni mavuvuzela ila kwenye stage na malengo tofauti tofauti. Think about it.
 
Nani alimusaidia kufungua kompyuta? maana siamini kama bado anakumbuka abonyeze wapi, tangu siku ile aliyokuwa akifungua huduma ya mkongo wa taifa.

Hata hivyo ndo maana sikupendezwa sana na kitendo cha viongozi wa JF kuanza kuwasogelea akina Sita bungeni na kutambulishwa. Ukisha wasogelea lazima wakutumie na hasa kwa hali hizi za kimaskini tulizonazo. Sisi hapa JF tungependa tubaki tulivyo bila kuegemea na kuwasalimia kila wakati hawa waheshimiwa.

Tusingependa mijadala ya aina fulani izuiliwe kwa sababu ya urafiki wa watu fulani tu maana wanasiasa wetu hawako tayari kuwa challenged.

Tuendelee kusema, wakiguswa watoe majibu. Watajikinga mpaka lini wakati elimu ya kompyuta siyo mali ya chama tawala?
 
Hata kama kuna mitandao ya chuki na udini etc, mbona hajatoa solution ya namna ya kukwepa uwepo wa mitandao?? Hizo complex data unazoongelea ziko wapi? Hizi za uchumi kukua na maisha bora kwa kila mtanzania au nyingine?? Maana inawezekana wote ni mavuvuzela ila kwenye stage na malengo tofauti tofauti. Think about it.

Moja kati ya solution nikuwata wananchi wa ignore mitandao inayo chochea, Kikwete ni kiongozi anaetoa uhuru wa habari kuliko kiliko viongozi wengine wlio pita, hakusema hapendi mitandao au wananchi wasisome mitandao, bali aliwanasii wasruhusu uchochezi.

Tuwe na hekima ktk kujadili htuba pamoja na data za uchumi na mengineyo, mafano, kama unapinga maelezo yalitolewa na Rahisi kuhusu kupunguza bajeti tegemezi toka 49% to 28% you are most welcome kama utatukinaisha lakini sio kujungle aroung na kupotosha hotuba za rahisi
 
Simply; Kikwete amelaani mitandao inayo eneza chuki na ukabila yenye malengo ya kuwatenganisha watanzania, kamwe watz hawatdanganyika. Hii ni message ya ku promote umoja kwa watanzania

Mavuvuzela wanashindwa kuelewa simple message, je mtakuwa na akili za kudadis complex data na messages? JF imeingiliwa!!!

kama wewe umeelewa hivyo...kazi tunayo!
 
Anashukru kwa kupewa heshima ya kupeperusha bendera ya CCM. anadai hawatawaangusha. Watatumia uwezo wao woote kufanya kampeni

HIZI NI MOJA YA HOSPITAL CCM INAJIVUNIA KUJENGA KILA KATA, JIOONEENI WENYEWE NA MUAMUE MNAYOAMBIWA NA MNACHO KIONA

Atawaambia nini hawa mama zetu, dada zetu, angalieni jamani kweli ni nchi hii hii anayozungumzia kikwete kuwa ameleta maendeleo??? ni dhambi kubwa sana, vilio vyao hawa akina mama Mungu anaviona

attachment.php
 
JK anakasirikia mitandao maana anajua kuna njia ya kuthibiti yanayojadiliwa.

Mitandao ina nguvu kuliko magazeti maana wachache wanaochangia katika mitandao wako huru kuliko waandishi wa magazeti ambao ni waoga.

Wapo ambao wanasoma habari kupitia mitandao hali inayosaidia kupata habari;

Ndio maana na yeye kaanzisha mtandao wa kwake. Sasa anaisaga mitandao wakati na yeye ameanzisha wa kwake? JK anaiga kampeni sytle ya Obama, kutumia website, wanafunzi wa vyuo, celebrities uchwara wa Tanzania etc. Hiyo strategy inaweza kuback fire kwa kuwa watanzania wengi sio wajuvi kwenye mambo hayo
 
HURUMA KWA WAGONJWA. Hivi CCM huwa ina huruma kwa hawa dada/wake/mama zetu?

610x.jpg

Temeke+Hostital

Sasa bwana Sikonge, CCM wameshindwa kutoa huduma bora za afya kwa kina mama na dada zetu. Hebu tuambie Chadema wana sera gani specific kuhusu ku-improve huduma ya afya? Wana mkakati gani wa kuongeza quality, while maintaining equity and improving access?
 
Back
Top Bottom