Elections 2010 Uzinduzi wa kampeni wa CUF jimbo la Bukoba Mjini

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Wakuu jumatatu tarehe 30.08.2010. chama cha CUF walizindua kampeini za uchaguzi mkuu jimbo la Bukoba mjini wakiongozwa na mgombea mwenza Mh. Duni kwenye uwanja maarufu wa mashujaa mjini Bukoba.

Yaliyowakuta inabaki ni historia kwani walisuswa na wale waliodhani kuwa ni wanachama wao katika jimbo hilo. Maana waliohudhulia mkutano huo hawakuwa zaidi 100, pamoja na kwamba hata waliohudhulia wengi wanafahamika kama wanachama wa vyama vya sisi M na Chadema.

Kwa uthibisho naunganisha picha zilizochukuliwa katika mkutano wenyewe.
DSC_1061.JPG
Picha hii inaonyesha Jukwaa lililo na waheshimiwa

DSC_1062.JPG
Picha hii inaonyesha jukwaa la waheshimiwa

DSC_1063.JPG
Hawa ndio walikuwa wasikilizaji wa hotuba ya mh Duni

DSC_1064.JPG
Hawa ni watu waliojiegemeza pembeni mwa ukuta unaozunguka uwanja wenyewe

DSC_1065.JPG
Na hii ni sehemu nyingine ya ukuta unaozunguka uwanja.

Ebu angalia picha hizi hapa chini zikionyesha nini kilitokea siku Dr Slaa alipokwenda kutafuta wadhamini katika uwanja huo huo mwezi jana.
DSC_2316.JPG DSC_2306.JPG
 
Haki Sawa Kwa Wote!
Peoples Power!

Kwa kuwa inaatuhumiwa kuwa CUF = Chama Cha Waislamu + Chama Cha Visiwani.
Na kwa Kuwa Inatuhumiwa kuwa CHADEMA = Chama Cha Ukabila + Chama Cha Waislamu.

Ni Miuhimu vyama hivi vifikirie kuungana hasa kwa 2015 ili waweze kushinda.

Wakiungana CHADEMA + CUF = Chama Cha Wananch Wote Bila Kujali Dini wala Kabila, kitakachokubalika bara na Visiwani.

Simple!
 
Malunde-Malundi;1059389]Au umebana picha maana sidhani k ama mgombea mwenza anastahili adhabu hiii jamani ehheee

 
Wanavuna walichopanda. Hivi CUF hakuna mtu mwingine mwenye mvuto zaidi ya Lipumba na Seif, Hawa watu washachoka ila wanashindwa kusoma alama za nyakati. Alipoulizwa kwa nini anagombea mara ya nne Lipumba alijibu kwamba anafuata nyayo za Abdulay Wade wa Senegal, sasa sijui anaona mazingira ya Tanzania na Senegal ni sawa au namna gani. Their influnce are fading
 
Mkuu Mchukia Ufiasai mbona mimi naona vijipicha vidogo, inawezekana kuvimaximize ili nione fresh
 
Au umebana picha maana sidhani k ama mgombea mwenza anastahili adhabu hiii jamani ehheee
Si kweli kwamba nimebana picha lakini hali ndivyo ilivyokuwa.

Nimeletewa picha hizo hata mimi nilishangaa sana. Kafu kwa jimbo hilo ilikwisha alipoondoka Wilfred Munganyizi Lwakatare.
 
Mkuu Mchukia Ufiasai mbona mimi naona vijipicha vidogo, inawezekana kuvimaximize ili nione fresh
NYU, sina utaalam mkubwa wa kuzifanya kubwa wakati na upload. Hata hivyo zina resolution kubwa. Asante Mchungaji Masa kwa msaada wako. Labda nitumie utaalam huo kwa PM ili next time niweke vizuri zaidi.
 
NYU, sina utaalam mkubwa wa kuzifanya kubwa wakati na upload. Hata hivyo zina resolution kubwa. Asante Mchungaji Masa kwa msaada wako. Labda nitumie utaalam huo kwa PM ili next time niweke vizuri zaidi.

attachment.php


Ni rahisi, click hiyo picha ndogo, the copy image location halafu insert image from from Url
 
Rev. Masa naona najaribu bila mafanikio. Give me more instructions please
71898-uzinduzi-wa-kampeni-wa-cuf-jimbo-la-bukoba-mjini.html
 
Ningekuwa mimi ndio mgombea, ningeamua kubwaga manyanga mapema nisubiri 2015.

Ushauri kwa wale wanaotaka kugombea kwenye uchaguzi wa 2015, wanatakiwa kuanza mikakati mwaka kesho Januari ikiwa ni pamoja na recruitment ya wanachama, kufungua matawi ya kutosha kwenye Jimbo wanalotaka kugombea na ikiwezekana kuanzisha sensitization programs plus civic education. Nina hakika after 5 yrs unapeta kuanzia kura za maoni mpaka uchaguzi mkuu (hapa ninaongelea vyama upinzani na hasa kwenye majimbo ambayo hayana matawi ya kutosha wala mwamko wa upinzani).

May be tatizo linaweza kujitokeza iwapo vikao vya juu vinaweza kukata jina la mhusika. Maana sometime huwa kuna free riders wengi sana, wakishaona jimbo fulani lina mwamko wa kutosha wataanza kujikomba makao makuu ili wapitishwe majina yao kugombea na ilihali mtu aliyefanya kazi ya kukiimarisha chama jimboni anatupwa pembeni.
 
Back
Top Bottom